Al Ahly vs YangaAl Ahly vs Yanga
  • Mashindano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho Afrika CAFCC, yataendelea tena kutimua vumbi wikiendi hii.  
  • Kati ya michezo mikubwa inayosubiriwa kwa hamu ni ule wa Al Ahly vs Young Africans.
  • Mchezo huu wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) unatarajiwa kupigwa jijini Alexandria, Misri.

Mashindano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, yataendelea tena kutimua vumbi wikiendi hii.  Kati ya michezo mikubwa inayosubiriwa ni ule wa Al Ahly vs Young Africans. Mchezo huu wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, Misri. Makala hii inadadavua dondoo muhimu za mchezo huu.

SOMA HII PIA: Kumekucha Al Ahly vs Young Africans SC CAFCL: Wananchi  kuwafuata Waarabu usiku huu

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Al Ahly vs Young Africans

Al Ahly vs Young Africas
Al Ahly vs Yanga

Al Ahly vs Yanga SC kwenye historia ya soka la ushindani, wamekutana katika michezo 8 katika siku za karibuni. Mpaka sasa Al Ahly wamekuwa bora, ambapo Katika michezo 8 waliyokutana waarabu hao wameshinda mechi 5. Yanga wameshinda mechi moja tu, huku mechi 2 zikimalizika kwa sare.

Vikosi tarajiwa Al Ahly vs Young Africans

Timu hizi mbili hazitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa ya vikosi kwakuwa hakuna majeraha mapya yalioripotiwa. Kwa Yanga kama sehemu ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo, hatimaye mlinda mlango namba 1 Djigui Diarra amejiunga na kikosi. Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Mali, ambacho kilikuwa kikishiriki AFCON 2025 nchini Morocco na kuifikisha Robo Fainali.

SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya mechi za CAF Champions League 2025/26/ Matokeo na magoli

Walichosema Young Africans kuhusu kuwavaa Al Ahly

Kocha Yanga- Pedro
Kocha Yanga- Pedro

Akizungumzia mchezo huo kocha, Pedro Goncalves amesema: “Tunatambua kuwa tunacheza dhidi ya klabu kubwa zaidi Afrika, klabu ya karne na hilo linahitaji heshima. Lakini kama tunataka kuwa sehemu ya historia ya soka la Afrika, si suala la kuwa na hofu ni suala la kucheza mpira. Mwisho wa siku tunakuja kucheza na kujaribu kuwashinda wapinzani wetu, huo ndio mpango wetu wa kesho.

Ili ufikie kiwango cha juu lazima ucheze dhidi ya timu bora. Tunaamini kikosi chetu kina ubora, wachezaji wana kiwango na wana hamu ya kutoa kila kitu kwa ajili ya timu. Tunawaamini wachezaji wetu na tunaamini kuwa kesho tutapata matokeo tunayoyataka.

“Kundi letu ni gumu sana. Tunawaheshimu wapinzani wetu wote kwa sababu wana historia kubwa na wametwaa mataji mengi barani Afrika. Lakini ukweli ni kwamba sisi pia tuna mipango ya muda mrefu ya kuwa miongoni mwa timu bora Afrika. Tuna pointi nne na bado tuna nafasi nzuri ya kuvuka hatua ya makundi.

Naye kiungo mshambuliaji mpya wa Young Africans, Allan Okello amesema: “Kesho tunacheza dhidi ya timu yenye uzoefu mkubwa, yenye wachezaji wa kiwango cha juu na benchi lenye nguvu. Hivyo ni muhimu kwa sisi wachezaji kuwa na mshikamano, na kupambana kwa dakika zote. Katika soka la leo kila timu ina wachezaji wazuri. Kinachofanya tofauti ni jinsi unavyotumia nafasi zako na jinsi unavyopunguza makosa.”

SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC

Al Ahly vs Young Africans, Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Al Ahly vs Young Africans
Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Yanga SC

Yanga wanatarajiwa kuwa na michezo miwili migumu, itakayofuatana dhidi ya Al Ahly. Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa nchini Misri Ijumaa ya Januari 23, mwaka huu na mchezo wa marudiano ukipigwa Januari 30, mwaka huu. Ikumbukwe michezo hii ni mwendelezo wa mechi za hatua ya Makundi ya Caf Champions League. Ikumbukwe kwenye mashindano hayo ni Young Africans na Simba SC zinaiwakilisha Tanzania.

Al Ahly SC vs Young Africans, Wananchi waiteka Misri  

Pacome mazoezini Misri
Pacome mazoezini Misri

Kuelekea ratiba ya mechi hizo, uongozi wa Yanga SC umethibitisha kuwa tayari kikosi chao kimewasiri Misri. Kikosi kimeendelea na mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa Mafarao kesho Ijumaa. Taarifa njema kwa Young Africans ni kuwa hakuna majeruhi aliyeongezeka.

Hitimisho

Al Ahly vs Young Africans unatarajiwa kuwa zaidi ya mchezo, hii ni vita ya thamani ya kuisaka Robo Fainali. Kila timu itajaribu kuboresha takwimu za kukutana kwao, ambapo mpaka sasa Al Ahly amekuwa bora. Katika michezo 8 waliyokutana waarabu wameshinda mechi 5, Yanga wameshinda mechi moja tu, huku mechi 2 zikimalizika kwa sare.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.