Al Ahly vs Yanga SCPacome vs Mashujaa FC
  • Tanzania Premier League 2025/26 Depu ameanza kazi
  • Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League, Januari 19,2026
  • Mudathir Yahya achaguliwa kuwa mchezaji bora, Allen Okelo kwenye majukumu mapya

Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League matokeo rasmi ya mchezo wa mzunguko wa kwanza. Wababe hawa wawili walikuwa wakitafuta pointi Uwanja wa KMC Complex. Magoli ya Yanga SC yamefungwa na  Mohamed Damalo dakika ya 8, Duke Abuya dakika ya 28, Pacome Zouzoua dakika ya 35, Prince Dube dakika ya 79, Mudathir Yahya dakika ya 80 na Depu dakika ya 89.

SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi

Je hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League yaandika rekodi

Yanga SC 6-0 Mashujaa FC
Dukevs Mashujaa FC

Ushindi wa Yanga SC 6-0 Mashujaa FC NBC Premier League umeandika rekodi mpya ndani ya 2026. Unakuwa ni ushindi mkubwa kwa mabingwa hao watetezi wa taji la NBC Premier League. Mshambuliaji mpya Depu akicheza mchezo wa kwanza amefungua ukurasa wa magoli.

Mbali na Yanga SC kuvuna pointi tatu, wanaandika rekodi kuishusha kileleni JKT Tanzania iliyofunga 2025 ikiwa namba moja. Kufikisha pointi 19 kunawapa nafasi kupanda mpaka namba moja. Wajeda JKT Tanzania wanachukua nafasi ya pili wakiwa na pointi 17, tofauti ya pointi moja.

Huu hapa msimamo

TimuPWDLPGF
1.Yanga SC76101918
5. Mashujaa FC10343135

Mudathir mchezaji bora

Muda tuzo
Mudathir kiungo wa Yanga SC akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora na wadhamini NBC. Source: Ligi Kuu.

Kiungo wa Yanga SC, Mudathir Yahya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Baada ya dakika 90 alikabidhiwa tuzo yake kutoka kwa wadhamini wa ligi. Hiyo yote imetokana na kutimiza majukumu yake kwa umakini.

Kwenye ushindi wa magoli 6-0 waliyopata watoto wa Jangwani, Mudathir alifunga goli moja. Kamati imepitisha jina la nyota huyo ambaye alikuwa kwenye kiwango bora. Inakuwa ni tuzo ya kwanza kwa Mudathir 2026.

SOMA HII: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC

image

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza vs Mashujaa FC

Langoni

Aboutwalib Mshery

Mabeki

Bakari Nondo

Dickson Job

Kibwana Shomary

Chadrack Boka

Viungo

Maxi Nzengeli

Pacome

Allan Okelo

Mohamed Camara

Duke Abuya

Mshambuliaji

Prince Dube

Wachezaji wa akiba

Balla Conte

Zimbwe Jr

Yao

Hussen Masalanga

Emmanuel Mwanengo

Abdulnassir Mohamed

Frank Assinki

Laulindo

George Mzungu

Kikosi cha Mashujaa FC vs Yanga SC

Erick Johola

Mpoki Mwakinyuke

Samweli Onditi

Abdulnassir Assa

Salum Kihimbwa

Hassan Alli

Mundhir Vuai

Jafari Kibaya

Yusuf Dunia

Mohamed Salum

Samson Madeleke

Wachezaji wa akiba

Daniel Lyanga

Mapinduzi Balama

Mgandila Shaban

Frank Magingi

Lameck Kanyonga

Abdul Bakari

Mudathir Said

Razakc Hussen

Seleman Bwenzi

SOMA HII: Yanga SC haina utani kuwapa mikataba mastaa hawa wa kazi 2025/26

image

Hitimisho

Yanga SC 6-0 Mashujaa FC rekodi imeandikwa Uwanja wa KMC Complex. Mashujaa FC wamekwama kuangusha Mbuyu kama ambavyo walibainisha awali. Wachezaji wapya wa Yanga SC tayari wameingia kwenye mfumo kutokana na kupata nafasi kwenye mchezo wa leo.

Share this: