Egypt vs Nigeria (-)Egypt vs Nigeria (-)
  • Vita ya kuisaka medali ya shaba ya mashindano ya AFCON 2025 itapigwa kesho Jumamosi nchini Morocco.
  • Hii ni katika mechi kali ya kumsaka mshindi wa tatu kati ya Egypt vs Nigeria.
  • Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Stade Mohammed V mjini Casablanca, Morocco.

Vita ya kuisaka medali ya shaba ya mashindano ya AFCON 2025 itapigwa kesho Jumamosi nchini Morocco. Ni mechi kali ya kumsaka mshindi wa tatu kati ya Egypt vs Nigeria. Mchezo huu mkali utapigwa kwenye Uwanja wa Stade Mohammed V mjini Casablanca, Morocco.

SOMA HII PIA: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores

Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Egypt vs Nigeria

Salah (-)
Salah

Timu hizi zimekutana mara 20 katika historia, ambapo Nigeria wamekuwa bora zaidi kwenye rekodi wakishinda mechi 9. Egypt wao wameshinda mechi 6 tu, huku mechi 5 zilizosalia zikimalizika kwa matokeo ya sare. Hivyo huu unakuwa mchezo wa 21 kwa timu hizi kuumana.

Fomu ya sasa timu zote mbili katika michezo yao 5 iliyopita;

Egypt

L-W-W-D-W

Nigeria

L-W-W-W-W

Vikosi tarajiwa Egypt vs Nigeria

Egypt

Kipa: El Shenawy

Walinzi: Hany, Ibrahim, Rabia, Fatouh

Viungo: Attia, Ashour, Fathy

Washambuliaji: Marmoush, Trezeguet, Mohamed

Nigeria:

AFCON 2025
Kikosi cha Nigeria

Kipa: Nwabali

Walinzi: Osayi-Samuel, Ajayi, Awaziem, Sanusi

Viungo: Onyeka, Ndidi, Iwobi

Washambuliaji: Lookman, Adams, Onuachu

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 final Senegal vs Morocco: Ratiba, Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Habari za timu

Timu zote 2 zinajivunia kuwa na mafanikio makubwa, kwenye mashindano ya msimu huu. Lakini ni wazi ushindi wa Medali ya shaba inaweza kutoa faraja kwa timu hizi baada ya kuikosa fainali. Ikumbukwe Misri walikuwa wakitafuta taji lao la 8 la AFCON, lakini Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Senegal kulipeperusha ndoto hiyo.

Bao la Sadio Mane dakika ya 78 lililotokana na shuti kali kutoka nje ya 18 na kumshinda kipa, Mohamed El Shenawy ndilo lilipeleka kilio kwa Mafarao. Nigeria wao waliondoshwa na wenyeji Morocco katika nusu fainali, kwa mikwaju ya penalti.

Taarifa za majeruhi

Osimhen (-)
Osimhen

Nigeria inatarajia kumkosa beki wake Calvin Bassey, ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza mechi yake ya pili. Hii inamfanya kocha wa Nigeria, Eric Chelle awe na kazi kubwa ya kufanya. Cyriel Dessers pia anatarajiwa kukosekana, lakini Habari njema ni kuwa nyota, Wilfred Ndidi anarejea kutoka kwenye adhabu ya kufungiwa.

Victor Osimhen huenda akaukosa mchezo huu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu na huenda, Akor Adams akaongoza mashambulizi kwa kushirikiana na Moses Simon na Ademola Lookman. Kwa upande wa Misri, Hossam Abdelmaguid anatumikia adhabu ya kadi kuonyeshwa kadi za njano. Mohamed Hamdy anatarajiwa kuendelea kukosekana kwa muda mrefu kutokana na jeraha la goti.

Mohamed Salah, akiwa na mabao manne naye huenda asicheze na kikosi kuongozwa na Omar Marmoush, Mostafa Mohamed, na Trezeguet kwenye safu ya ushambuliaji.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Hizi hapa nchi 5 zilizotolewa mapema  

Hitimisho

AFCON 2025 Match round 1
Marmoush

Hatimaye pazia la mashindano ya AFCON 2025 linafungwa rasmi wikiendi hii kwa michezo miwili. Egypt vs Nigeria ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu. Mshindi wa mchezo huu atatawazwa kuwa mshindi wa tatu na kubeba medali ya fedha. Je, ni Egypt au Nigeria? Dakika 90 zitatoa majibu japo Nigeria wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.