Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier LeagueE-Mpanzu
  • Matokeo ya Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar yanabaki kwenye rekodi ya ushindi mkubwa walipokutana Tanzania Premier League.
  • Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League saa 10:00 jioni Uwanja wa Mej. Isahmuhyo.
  • Tangu 2016 Simba SC imeshinda mechi 12 Mtibwa Sugar ikipata ushindi mechi moja wakitoshana nguvu mechi 3.

Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba 2025/26. Hii ni baada ya ligi kusimama kutokana na mashindano ya AFCON 2025, Morocco. Burudani inarejea Jumapili, Januari 18, 2026, Uwanja wa Mej. Gen. Isamuhyo.

SOMA HII: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League nani atashinda?

Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League
Chasambi Ladack nyota wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Wapinzani hawa wawili Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League wanatarajiwa kuwa na mchezo wa ushindani. Hii inatokana na maandalizi ambayo yanaendelea kufanywa. Mnyama anapewa nafasi kubwa kupata matokeo kwenye mchezo ujao.

Uwepo wa Kocha Mkuu Steve Barker ambaye ni mpya unatajwa kuongeza nguvu. Licha ya timu hiyo kupoteza mchezo uliopita kwenye ligi. Ikumbukwe kwamba 2025 mnyama mchezo wa mwisho ilikuwa Simba SC 0-2 Azam FC.

Mtibwa Sugar sio timu ya kubeza kutokana na matokeo inayopata. Ni timu inayotumia wachezaji wengi wazawa wenye uwezo. Hivyo lolote linaweza kutokea. Unakuwa mchezo wa kwanza kwenye ligi ndani ya 2026 kwa wababe hawa wawili kukutana uwanjani.

Msimamo wa NBC Premier League

TeamPositionMPWDLGFPts
Simba SC554011112
Mtibwa S.78242410

Simba SC kwenye msimamo ni nafasi ya 5 ikiwa na pointi 12 baada ya mechi 5. Inakutana na Mtibwa Sugar nafasi ya 7 pointi 10 baada ya mechi 8. Vinara kwenye msimamo ni JKT Tanzania wakiwa na pointi 17 baada ya kucheza mechi 10. Tangu 2026 rekodi zinaonyesha kuwa wamekutana mara 16. Simba SC ushindi mechi 12, Mtibwa Sugar ushindi mchezo mmoja sare 3.

SOMA HII: NBC Premier League table 2025/26

image

H2H Simba SC vs Mtibwa Sugar

Baja B
Kiungo wa Simba SC Bajaber. Source: Simba SC.

03/05/2024- Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar
17/08/2023 – Mtibwa Sugar 2-4 Simba SC
11/03/2023- Mtibwa Sugar 0-3 Simba SC
30/10/2022- Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar
23/06/2022- Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar

Mechi zilizopita kwa Simba SC

Azam FC 1-0 Simba SC, 08/01/2026
Fufuni 1-2 Simba SC, 05/01/2026
Simba SC 1-0 Mwembe Makumbi City, 03/01/2026.

Mechi zilizopita za Mtibwa Sugar

3/12/2025- JKT Tanzania 0-0 Mtibwa Sugar
29/11/2025- Mtibwa Sugar FC 2-1 TRA United
25/11/2025-KMC 0-0 Mtibwa Sugar

Kikosi cha Simba SC huenda kikawa namna hii

Abel
Duchu
Mligo
Chamou
De Reuck
Kagoma
Ahoua
Camara
Mukwala
Maema
Mpanzu

Kikosi cha Mtibwa Sugar vs Simba SC kinachotarajiwa kuanza

Mtibwa Sugar
Nyota wa Mtibwa Sugar wakiwa kwenye uwanja wa mazoezi. Source: Mtibwa Sugar.

Costa
Victor
Lyawatwa
Nyangi
Imoro
Marungu
Chicharo
Raizin
Manga
Chota
Kiziwa

SOMA HII: Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League KMC Complex | Highlights, magoli, Zimbwe Jr mchezaji bora

image

Hitimisho

Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya unyamani. Kwenye mechi tatu ambazo Steve Barkier aliongoza ilikuwa NMB Mapinduzi Cup. Je ataanza kwa ushindi, sare ama atapoteza? Matokeo yake yatakuwa hapa mara baada ya mchezo kukamilika.


Share this: