- Baada ya michezo 50 kupigwa tangu kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025, hatimaye mashindano hayo yatafikia tamati siku ya Jumapili.
- Hii ni katika AFCON 2025 Final kali itayowakutanisha Senegal vs Morocco.
- Joto limezidi kuwa juu kuelekea mchezo huo kutokana na ubora wa timu zote mbili. Je ni Ashraf Hakimi, au Sadio Mane kubeba ubingwa?
- Makala hii inakuletea dondoo muhimu za mchezo huo.
Baada ya michezo 50 kupigwa tangu kuanza kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, hatimaye mashindano hayo yatafikia tamati siku ya Jumapili kwa AFCON 2025 Final kali kati ya Senegal vs Morocco. Fainali hii itaandikisha mchezo wa 52 na wa mwisho. Joto limezidi kuwa juu kuelekea mchezo huo kutokana na ubora wa timu zote mbili. Je ni Ashraf Hakimi, au Sadio Mane kubeba ubingwa? Makala hii inakuletea dondoo mihimu za mchezo huo.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba ya Robo Fainali, hizi hapa timu zilizofuzu
Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, AFCON 2025 Final Senegal vs Morocco

Historia ya soka la ushindani katika mashindano yote kati ya Senegal na Morocco inaonyesha timu hizi zimekutana mara 31 Senegal imeshinda mechi 6 tu, huku Morocco wakiwa wababe kwa kushinda mechi 18. Mechi 7 zilizosalia zilimalizika kwa matokeo ya sare.
Fomu ya Senegal kwenye mechi 5 zilizopita
DWWWW
Fomu ya Morocco katika mechi 5 zilizopita:
DWWWW
Vikosi tarajiwa Senegal vs Morocco

Senegal
Kipa: Edouard Mendy
Walinzi: Krepin Diatta, Mamadou Sarr, Moussa Niakhate, El Hadji Malick Diouf
Viungo: Pape Gueye, Idrissa Gueye, Lamine Camara
Washambuliaji: Sadio Mane, Iliman Ndiaye, Nicolas Jackson.
Morocco
Kipa: Yassine Bounou
Walinzi: Achraf Hakimi, Nayef Aguerd, Adam Masina, Noussair Mazraoui
Viungo: Bilal El Khannouss, Neil El Aynaousi, Ismael Saibari
Washambuliaji: Brahim Diaz, Abde Ezzalzouli, Ayoub El Kaabi
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Habari za timu na safari ya kufuzu Fainali

Senegal itavaana na wenyeji Morocco katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025, kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah. Hii ni vita ya Simba wawili, yaani Simba wa Milima ya Atlas (Morocco), na Simba wa Teranga (Senegal). Kwa sasa timu hizi ndizo timu mbili zinazoorodheshwa juu kwenye viwango vya ubora barani Afrika. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kuleta mvuto na ushindani mkubwa.
Senegal wameingia fainali, baada ya kuwafunga mabingwa wa zamani Misri bao 1-0 katika nusu fainali. Bao la Sadio Mane dakika ya 78 ndilo lilileta utofauti wa matokeo. Senegal walitawala mechi hiyo, huku Misri wakicheza kwa kujihami zaidi mpaka pale walipotanguliwa kwa bao la Mane.
Senegal wanajivunia safu bora ya ushambuliaji, ambayo imeshika nafasi ya pili nyuma ya ile ya Nigeria. Senegal imefunga mabao 12 na kutengeneza nafasi 20 kubwa. Morocco wao wametinga fainali baada ya kuifunga Nigeria 4-2 kwa mikwaju ya penalty.
Kikosi hicho cha kocha, Walid Regragui kilifanikiwa kuzima mashambulizi ya kuogofya ya Nigeria kwa dakika 120. Nigeria walimaliza mchezo huo wakiwa wamepiga shuti moja tu, ambalo lililenga lango. Morocco pia walifanikiwa kutengeneza mashambulizi yaliyoonekana kuwa ya kutisha zaidi.
Taarifa ya majeruhi na watakaokosekana

Senegal itamkosa nahodha wao mashuhuri na mlinzi, Kalidou Koulibaly na kiungo Habib Diarra kutokana na kufungiwa. Kwa upande wa Moroco bado, Azzedine Ounahi na Romain Saiss wako nje ya uwanja kutokana na majeraha. Kwa kiasi kikubwa timu zote mbili zinasaliwa na Kundi kubwa la wachezaji waliofiti kukiwasha kwenye fainali hiyo.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC
Hitimisho
Mashindano ya AFCON 2025 yamekuwa na msisimko mkubwa mwaka huu, tukielekea katika mchezo mkali wa Fainali kati ya Senegal vs Morocco. Maswali makubwa ni je, nani kuvishwa ubingwa wa Afrika baada ya Ivory Coast kuvuliwa? Fainali ya AFCON 2025 inatarajiwa kuwa yamoto sana hasa kutokana na ubora wa kila timu. Tusubiri kuona dakika 90 za fainali zitakuja na majibu gani? Je, ni Ashraf Hakimi au Sadio Mane?

