Tetesi usajili mpyaTetesi usajili mpya
  • Harakati za usajili wa dirisha dogo kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/26 zinaendelea kushika kasi. Tayari kuna madili ambayo yamekamilika, na Tetesi usajili mpya nyingine zimeripotiwa.
  • Hatimaye Wananchi Yanga SC wamemtambulisha rasmi straika wao mpya, Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu ‘Depu’.
  • Wakati Yanga ikimtambulisha rasmi Depu, upande wa pili Simba nao inatajwa kumalizana na kiungo mshambuliaji wa Senegal, Gueye.
  • Makala hii inakuletea kwa ufupi baadhi ya tetesi za usajili mpya wa Ligi Kuu Bara.

Hatimaye Wananchi Yanga SC wamemtambulisha rasmi straika wao mpya, Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu ‘Depu’. straika huyo amesaini mkataba wa miaka miwili Jangwani, ambapo sasa amekuja kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga SC. Wakati Yanga ikimtambulisha rasmi Depu, upande wa pili Simba nao inatajwa kumalizana na kiungo mshambuliaji wa Senegal, Gueye. Makala hii inakuletea kwa ufupi baadhi ya tetesi usajili mpya wa Ligi Kuu Bara.

SOMA HII PIA: Clatous Chama kumalizana na Simba SC sababu zatajwa/ Awesu katambulishwa Police FC Kenya

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu Tetesi usajili mpya wa Depu Yanga SC

Depu na Dube
Depu na Dube

Kocha mkuu mpya wa Yanga SC, Pedro anatajwa kuwa kiungo muhimu cha usajili huu kutokana na mahusiano yake na mchezaji. Kwa mujibu wa mchambuzi wa Habari za michezo, Hans Raphael amefichua kuwa dili la Depu limeigharimu Yanga kiasi cha zaidi ya bilion 1.2 ya Tanzania. Fedha hizi zinahusisha pesa ya kukamilisha usajili na malipo binafsi.

Inaelezwa kabla ya dili la Kwenda kucheza soka Ulaya, Depu alikuwa mchezaji bora x2 wa COSAFA, pia alikataa ofa ya Al ahly Cairo, Orlando Pirates na Kaizer Chiefs. Staa huyo anauzoefu mkubwa akiwahi kucheza ligi ya Ureno, ligi ya Serbia na Ligi ya Poland. Depu ni sehemu ya maboresho ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA HII PIA: Usajili mpya Simba SC 2025/26 gumzo | Wachezaji wawili tegemeo watambulishwa | Orodha kamili

Tetesi usajili mpya wa Ligi Kuu Bara ndani ya Simba SC

Gueye
Gueye

Simba nao hawako nyuma katika heka heka za usajili kwani, taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa tayari wamekamilisha usajili wa Nyota wa kimataifa Gueye na Toure. Kwa mujibu wa Hans Raphael nyota, Libasse Gueye Tayari yuko Tanzania na aesaini mkataba wa miaka mitatu na Simba. Wakati huo huo Mnyama amekamilisha usajli wa beki wa kati wa zamani wa Stellenbosch, Osmail Olivier Touré (28), nyota huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu. Nyota huyo ambaye inaelezwa ni pendekezo la kocha mkuu tayari yupo Tanzania.

Ahoua apigwa bei, Diaw bado hakijaeleweka Simba SC

Beki wa kushoto wa zamani wa Al hilal, Khadim Diaw (27) inaelezwa yuko Tanzania kumalizana na Simba. Mpaka sasa bado hajamwaga wino, lakini mazungumzo yanaendelea kuona ikiwa pande hizo mbili zitaafikiana. Kuhusu kiungo wao, Jean Charles Ahoua (23), Simba SC wamemuuza nyota huyo kwenda Uarabuni. Inaelezwa uongozi wa Simba tayari upo kwenye mchakato wa kusaka mbadala wake kutoka Afrika Kusini.

Mukwala mmh! Gego agombaniwa na Simba SC, Azam FC

Kwa mujibu wa mchambuzi, Hans Raphael kiungo wa singida Black stars, Khalid habibu GEGO yuko kwenye mazungumzo na vilabu vya Azam FC na Simba SC kwa ajili ya kumnasa staa huyo. Nyota huyo amesaliwa na mkataba wa miezi 6 ndani ya Singida Black Stars, hivyo anaruhusiwa kuzungumza na timu yeyote. Imeelezwa dirisha kubwa lililopita Simba walikataa ofa ya $800,000 kutoka Ittihad ya Libya, lakini kocha mpya Steve Barker amewambia viongozi wamtoe Mukwala kwa mkopo kwani yeye hamuelewi.

SOMA HII ZAIDI: Allan Okello mambo fresh Yanga SC/ Orodha ya wapya waliotambulishwa

Hitimisho

Tetesi usajili mpya
Usajili tetesi

Usajili wa dirisha dogo ni nyakati muhimu ya maboresho ya vikosi kwa ajili ya nusu ya pili ya msimu. Ni wazi mashabiki na viongozi wanaposhabikia tetesi usajili mpya wanapaswa pia kuzingatia ubora wa wachezaji ambao wanasajiliwa kwa kuwa usajili huu unahitaji nyota walio kwenye ubora na sio wa majaribio. Kila la kheri kwa nusu ya pili ya msimu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.