- ‘Manchester Derby’ ndio stori kubwa wikiendi hii katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu England.
- Ni Mchezo mkali wa mahasimu wawili wakubwa England, Manchester United vs Manchester utaopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
- Kocha mpya wa muda wa Manchester United, Michael Carrick kwa mara ya kwanza msimu huu anatarajia kuanza majukumu yake rasmi.
‘Manchester Derby’ ndio stori kubwa wikiendi hii katika Ligi Kuu England. Ni Mchezo mkali wa mahasimu wawili wakubwa England, Manchester United vs Manchester City. Mchezo huu utashuhudia Kocha mpya wa muda wa Manchester United, Michael Carrick kwa mara ya kwanza msimu huu akianza majukumu yake. Mchezo huu wa kukata na shoka utapigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
SOMA HII PIA: ‘MANCHESTER DERBY’ NI MAN UNITED Vs MAN CITY KINAPIGWA LEO JUMAPILI
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Manchester United vs Manchester City

Historia ya soka la ushindani kati ya Manchester United vs Manchester City inaonyesha timu hizi zimekutana mara 197. Man United imeshinda 80, huku Man City wakishinda mechi 62. Mechi 55 zilizosalia zilimalizika kwa matokeo ya sare, hivyo hii ni nafasi nyingine kwa timu hizi kuandika rekodi mpya.
Fomu ya Manchester United kwenye mechi 6 zilizopita
L W D D D L
Fomu ya Ligi Kuu ya Manchester City mechi 6 zilizopita
W D D D W W
Vikosi tarajiwa Manchester United vs Manchester City
Manchester United
Kipa: Lammens
Walinzi: Dalot, Maguire, Martinez, Shaw
Viungo: Casemiro, Mainoo, Mbeumo, Fernandes
Washambuliaji: Cunha, Sesko
Manchester City

Kipa: Donnarumma
Walinzi: Nunes, Khusanov, Alleyne, O’Reilly
Viungo: Rodri, Bernardo, Cherki, Foden, Semenyo
Mshambuliaji: Haaland
SOMA HII ZAIDI: The Manchester United vs. Manchester City’s Tactical Battle & Predictions
Habari za timu
Hii itakuwa ni mara ya 198, kwa timu hizi kuvaana katika mchezo wa dabi. Mashabiki wa pande zote mbili watakuwa na matumaini ya pambano kali zaidi, la Premier League.
Zimepita siku nane baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuuwa United, Ruben Amorim, ambapo Man United ilimtangaza nahodha wao wa zamani Michael Carrick kuwa kocha mkuu wa muda. Carrick atahudumu kwa mkataba hadi mwisho wa msimu. Hii itakuwa mara ya pili kwa mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44, kuiongoza United baada ya kufanya hivyo mnamo Novemba/Desemba 2021. Katika mechi tatu alizoiongoza United hapo awali, Carrick alishinda 2 na kusare mechi 1.
Carrick anarejea ikiwa ni miezi saba baada ya kutimuliwa kutoka Middlesbrough, ambako alishinda 46.3% ya mechi 136 alizoongoza. Man United kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Tofauti ya pointi 3 tu, ndiyo inawatenganisha kati yao na nne bora licha ya kwamba wameshinda mechi moja tu, kati ya sita zilizopita.
Taarifa ya majeruhi

Man United bado wanalazimika kucheza bila mlinzi, Noussair Mazraoui aliyepo AFCON, huku mlinzi mwingine, Matthijs de Ligt akiuguza majeraha. Straika kinda, Shea Lacey atakosekana pia kufuatia kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Brighton. Hata hivyo, Carrick amepata ahueni baada ya kurejea kwa washambuliaji wawili, Bryan Mbeumo na Amad Diallo ambao mataifa yao yaliishia Robo Fainali ya AFCON 2025.
Kwa upande wa Man City wanaotarajiwa kukosekana ni; Josko Gvardiol (amevunjika mfupa wa tibial), Mateo Kovacic (kifundo cha mguu/kisigino), John Stones (paja). Ruben Dias, Oscar Bobb (wote wawili) na Savinho (haijatajwa), wote wako nje ya uwanja kutokana na majeraha. Omar Marmoush bado yuko kusubiria mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa mashindano ya AFCON 2025 nchini Morocco.
SOMA HII PIA: Manchester United’s Epic 5-Star Derby Clash vs City
Hitimisho

Manchester United vs Manchester City ni zaidi ya mechi, mchezo huu unatathimini ufalme wa jiji la Manchester. Ni wazi kuwa mchezo huu utakuwa mgumu sana kutokana na umuhimu wa pointi 3 kwa kila timu. Swali ni Je, kocha mpya wa muda wa Man United ataweza kuandikisha hati safi kwenye mchezo huu, au Guardiola ataendeleza ubabe?

