- Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yamefikia patamu nchini Morocco.
- Mashindano hayo yameingia raundi ya pili 16 bora (Round of 16), leo Jumamosi.
- Mashindano haya yamekuwa na msisimko mkubwa huku vita ya kufunga mabao ikinogesha zaidi.
- Makala hii inaangazia mastaa wanaoongoza listi ya ufungaji bora AFCON 2025 Je, Msuva na Feisal wapo?
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanazidi kunoga nchini Morocco. Mashindano hayo yameingia raundi ya pili 16 bora (Round of 16). Mashindano haya yamekuwa na msisimko mkubwa, huku vita ya kufunga mabao ikinogesha zaidi. Makala hii inaangazia mastaa wanaoongoza listi ya ufungaji bora AFCON 2025.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 hawa hapa vinara mabao hatua ya makundi

Nahodha wa Algeria, Riyad Mahrez ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaoongoza listi ya ufungaji bora mpaka kumalizika kwa hatua ya makundi. Mahrez atashukuru mabao yake mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Sudan. Katika listi hiyo, Mahrez anaungana na washambuliaji wawili wa Morocco Brahim Diaz na Ayoub El Kaabi.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 hatua ya 16 bora ratiba/ Morocco vs Tanzania kuwashangaza wengi, msimamo
Hawa hapa wana mabao 2 kila mmoja

Jackson alifunga mabao 2 katika ushindi wa Senegal dhidi ya Botswana na Achouri alifunga mabao mawili wakati Tunisia ilipoiangamiza Uganda. Hii inawafanya mastaa hao, waongoze listi ya mastaa wenye mabao mawili mpaka sasa. Jackson ana nafasi ya kuongeza bao leo wakati Senegal itakapovaana na Sudan.
Mastaa wengine wenye mabao mawili ni; Raphael Onyedika (Nigeria), Ademola Lookman (Nigeria), Amad Diallo, Lyle Foster (S.A), Mohamed Salah (Egypt), Lassine Sinayoko (Mali).
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Hizi hapa nchi 5 zilizotolewa mapema
AFCON 2025: Msuva, Feisal waongoza listi ya waliofunga bao 1 kila mmoja

Baadhi ya wachezaji wengine kadhaa pia wamefanikiwa kufunga angalau bao moja hatua ya makundi. Mastaa hao ni Pamoja na; Simon Msuva (Tanzania), Semi Ajayi (Nigeria), Feisal Salum (Tanzania), Marvin Anieboh, Wilfred Ndidi (Nigeria), Charles Mmombwa (Tanzania), Omar Marmoush (Misri), Paul Onuachu (Nigeria), Victor Osimhen (Nigeria).
Hitimisho
AFCON 2025 imeanza rasmi kupigwa hatua ya 16 bora, kila timu ikiweka kila ilichonacho kusaka tiketi ya Robo Fainali. Bado mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni nani ataendeleza moto wa kufunga mabao, na hatimaye kuibuka mshindi wa Kiatu cha Dhahabu mwishoni mwa shindano hilo. Ikumbukwe mashindano haya Makala ya 2023 kule Ivory Coast straika na nahodha wa Equatorial Guinea, Emilio Nsue aliibuka mfungaji bora.

