- Hatima ya mwisho kwa Tanzania katika mashindano ya AFCON 2025 itajulikana rasmi Jumanne hii.
- Ni matokeo ya mchezo wa AFCON 2025 Tanzania vs Tunisia.
- Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Olympique Annexe Complexe Sportif Prince Abdellah.
- Timu yoyote itakayoshinda itajiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, huku kipigo kikimaanisha kuaga mashindano.
Hatima ya Tanzania katika mashindano ya AFCON 2025 itajulikana rasmi Jumanne hii. Ni katika mchezo wa AFCON 2025 Tanzania vs Tunisia. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Olympique Annexe Complexe Sportif Prince Abdellah. Timu itakayoshinda itajiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, huku kipigo kikimaanisha kuaga mashindano.
SOMA HII PIA: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, AFCON 2025 Tanzania vs Tunisia

Rekodi inaonyesha timu hizi mbili katika siku za karibuni, Tanzania na Tunisia zimekutana mara 2 katika mashindano mbalimbali. Tunisia wamekuwa na rekodi nzuri zaidi wakishinda mechi 1. Tanzania haijashinda mchezo wowote na mchezo mmoja umeisha kwa sare.
Mechi 5 zilizopita za Tanzania

30/12/25 Tanzania vs Tunisia
27/12/25 Uganda 1-1 Tanzania
23/12/25 Nigeria 2-1 Tanzania
15/11/25 Kuwait 4-3 Tanzania
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1
Vikosi tarajiwa Tanzania vs Tunisia
Tunisia

Kipa: A. Dahmen
Walinzi: Y. Valery, D. Bronn, M. Talbi, A. Abdi
Viungo: E. Skhiri, F. Sassi, H. Mejbri, S. Tounekti
Washambuliaji: E. Achouri, H. Mastouri
Tanzania
Kipa: Foba
Walinzi: Kapombe, Mwamnyeto, Hamad, Hussein
Viungo: Mirishi, Msanga, Msuva, M’Mbobwa, Allarkhia
Mshambuliaji: Samatta
Habari za timu

Tunisia walianza vizuri kwa ushindi dhidi ya Uganda, lakini wakajikuta wakipoteza katika mchezo wao wa pili mbele ya Nigeria kwa mabao 3-2. Hii itawafanya kuwa na hamu ya kuibuka na ushindi mbele ya Tanzania. Tunisia wana kazi kubwa kufanikisha hilo, kwani Tanzania imesaliwa na tumaini la matokeo ya ushindi tu, ili kusalia mashindanoni.
Kwa Tanzania hali ni mbaya zaidi kwani katika siku za hivi karibuni, hawajapata ushindi wowote ndani ya michezo 9 mfululizo. Wamepoteza michezo 6 na kutoa sare mechi 3 na mechi za michuano yote (D3, L6), huku mechi zao tano mfululizo zilizopita wakipata vipigo mara nne na sare 1.
Kupoteza kwao mele ya Nigeria Jumanne iliyopita na sare dhidi ya Uganda, kumefanya waandikishe mechi 11 bila ushindi kwenye mashindano ya AFCON wamefungwa mara 7 na kutoa sare 4.
SOMA HII PIA: Afcon 2025: Hawa hapa wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi
Taarifa za majeraha
Kuhusu majeraha, Uganda hawajaripoti mchezaji yoyote kabla ya mechi yao ya Jumamosi. Kwa Tanzania, Yakoub Suleiman ambaye alikosa mechi ya kwanza, huenda akarejea kikosini. Wakati ambao Feisal tayari amerejea kikosini.
Hitimisho
AFCON 2025 Tanzania vs Tunisia ni zaidi ya mechi, ni vita ya heshima juu ya nani atabaki kwenye mashindano na nani safari inamhusu. Unatarajia kuwa mchezo mgumu, hasa kwa kuwa atakayeruhusu kupoteza ataaga mashindano. Hivyo kila timu itapambana kutopoteza mchezo. Kwa kuangalia fomu yao katika siku za karibuni utabiri wa mchezo huu huenda ukaisha kwa ushindi wa Tunisia.

