- Moto utawaka leo Jumanne pale washindi wa pili wa AFCON iliyopita, Nigeria watakapovaana na Tanzania.
- Nigeria vs Tanzania AFCON 2025 Mchezo huu unaosubiriwa kwa hamu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Fez, nchini Morocco.
- Huku Osimhen na Lookman, kule Samatta na Msuva nani kuondoka na tabasamu.
Leo ndio leo, hatumwi mtoto dukani. Washindi wa pili wa AFCON iliyopita, Nigeria leo Jumanne watafungua pazia la kampeni yao ya mashindano ya mwaka huu kwa kuvaana na timu ya Taifa ya Tanzania. Mchezo huu unaosubiriwa kwa hamu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Fez.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Umeona? Timu zatambiana Morocco kwa mavazi makali
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Nigeria vs Tanzania AFCON 2025
Fomu ya Nigeria kwenye michezo yao 6 iliyopita ya mashindano yote, inaonekana kuwa bora kulinganisha na wapinzani wao. Katika mechi hizo 6 Nigeria wameshinda mechi 3, wamepoteza mechi 2 na kutoa sare mchezo mmoja. Hivyo hii ni nafasi kuongeza ubora wa namba zao.
Kwa upande wa Tanzania Fomu ya Tanzania hali ni mbaya kwani katika mechi 6 hawana ushindi wowote. Wamepoteza mara 5 na kutoa sare mechi moja pekee. Hii ina maana mchezo huu unabeba maana kubwa kwao.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza leo

Kwa upande wa Nigeria;
Kipa: Nwabali
Walinzi: Sanusi, Bassey, Ajayi, Osayi-Samuel
Viungo: Ndidi, Iwobi, Chukwueze, Lookman
Washambuliaji: Osimhen, Adams
Kwa upande wa Tanzania

Kipa: Suleiman
Walinzi: Kaponbe, Mwamnyeto, D. Job, M. Husseini
Viungo:N Miroshi, F Salum, Msuva, M’Mombwa, Allarakhia
Mshambuliaji: Samatta
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Morocco vs Comoros mchezo wa ufunguzi/ Ratiba hii hapa
Habari za timu
Nigeria ambao walichapwa 2-1 na wenyeji Ivory Coast katika fainali ya michuano iliyopita na kumaliza nafasi ya pili, sasa wameazimia kupiga hatua moja zaidi na kulisaka kombe. Mabingwa hao wa zamani wana hasira zaidi hasa baada ya kushuhudia wakipoteza nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la dunia mwakani.
Kupoteza huko kulizua sura isiyohitajika katika historia ya taifa hilo. Nigeria wanauendea mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri. Kipigo hiko kilihitimisha mfululizo wa mechi saba za ushindi kabla. Nigeria ambao wamewahi kuwa nafasi ya 38 kwenye msimamo wa viwango vya Fifa, inahitaji ushindi.
Hata hivyo, bado Nigeria itahitaji kucheza kwa tahadhari kubwa hasa kwa kuwa wana mfano wa hivi karibuni kubanwa mbavu na timu za Daraja la kati. Hii ni ikiwemo sare ya 1-1 dhidi ya Equatorial Guinea. Nigeria wanaendelea kusubiri kwa mara ya kwanza taji la Afrika tangu 2013.
Tanzania, kinyume chake, inawasili ikiwa na presha ndogo sana, huku wakitarajia kuandaa mashindano ya 2027, ambayo watashirikiana na Uganda na Kenya. Taifa Stars inasaka kwa mara ya kwanza nafasi ya kuvuka hatua ya makundi, ya mashindano haya. Vipigo mfululizo katika michezo yao iliyopita huenda vikawapa hali ya hofu.
Habari za majeruhi

Beki wa timu ya Brentford Benjamin Fredrick alikuwa katika kiwango bora katika kampeni ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, lakini atakosekana kufuatia jeraha la goti. Ola Aina pia anatarajiwa kusalia nje ya uwanja kufuatia tatizo la misuli ya paja, aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Afrika Kusini mnamo Septemba.
Nahodha mwandamizi wa Nigeria, William Troost-Ekong, alistaafu soka la kimataifa hivi karibuni. Hii inamaanisha kwamba Wilfred Ndidi atavaa kitambaa hicho, na anatarajiwa kuimarisha safu ya kati ndani ya mfumo wa almasi wa 4-4-2 unaopendwa na Chelle.
Bassey na Semi Ajayi wanapendekezwa kuunda safu ya ulinzi ya kati, huku Bright Osayi-Samuel na Zaidu Sanusi wakielekea kulia na kushoto, mtawalia. Kitengo ambacho kinapaswa kumlinda Stanley Nwabali kipa chaguo la kwanza. Maduka Okoye atakosekana na kupunguza ushindani wa nafasi ya kipa.
Tanzania haijaripoti majeruhi yoyote na kocha Gamondi amechagua kundi la wanaume 28 linalochanganya vijana na wenye uzoefu. Fowadi mkongwe, Simon Msuva anarejea baada ya kukosekana. Akiwa na mabao 24 ya kimataifa, Msuva pia amebakisha bao moja ili alingane na Mrisho Ngasa mfungaji bora wa muda wote wa Tanzania.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Joto lapanda Morocco, Jeshi la Tanzania laweka kambi Misri
Hitimisho
Nigeria vs Tanzania ni karata ya kwanza ya Kundi C la mashindano ya AFCON 2025. Ni mchezo ambao unatarajiwa kutoa matokeo ya kushangaza, hasa kutokana na mwenendo wat imu zote mbili. Swali ni je, nani ataondoka na tabasamu leo?

