- Brahim Diaz afungua akaunti ya mabao, atwaa tuzo ya mchezaji bora Uwanja wa Prince Moulay Abdallah
- AFCON 2025 Morocco 2-0 Comoros mchezo wa ufunguzi ulioacha rekodi zakutosha
- Ayoub El Kaabil goli lake kutwaa tuzo kwenye mashindano AFCON 2025?
AFCON 2025 Morocco 2-0 Comoros ni matokeo rasmi mchezo wa ufunguzi. Wenyeji wameanza kwa ushindi katika hatua ya makundi wakiwa kundi A. Uwanja wa Prince Moulay Abdallah ulishuhudia magoli kutoka kwa Brahim Diaz dakika ya 55 na El Kaabi dakika ya 74.
SOMA HII: AFCON 2025 Morocco vs Comoros mchezo wa ufunguzi/ Ratiba hii hapa
Zamu yako kushinda sasa hivi, cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 Morocco 2-0 Comoros, Brahim Diaz mchezaji wa mchezo

Wakati AFCON 2025 Morocco 2-0 Comoros Brahim Diaz alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Nyota huyo alifunga goli la ufunguzi akitumia pasi ya N.Mazraoui. Wakiwa kwenye uongozi pasi ya Salah-Eddine ilitumiwa vizuri na El Kaabi aliyefunga goli la pili.
Ikumbukwe kwamba Brahim Diaz ni kinara wa utupiaji katika mchakato wa kufuzu AFCON 2025. Alifunga jumla ya magoli 7 nyavuni. Tayari meanza kampeni kwenye mashindano haya makubwa Afrika.
Chini ya Kocha Mkuu, Walid Regragui Morocco wamezianza vema kampeni kwa ushindi kwenye mchezo wa kundi A. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuongoza kundi ikiwa na pointi 3.
Shukrani kwa Yannick Pandor mlinda mlango wa Comoros
Ipo wazi kuwa dakika 45 za mwanzo zilikuwa ngumu kwa timu zote mbili. Wenyeji Morocco walikuwa na nafasi ya kupata goli la kuongoza dakika ya 11 kupitia mkwaju wa penalti ambao walipata. Shukrani kwa mlinda mlango wa Comoros Yannick Pandor ambaye aliokoa pigo la penalti iliyopigwa na Soufiane Rahims.
SOMA HII: Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 Morocco/ Orodha ya wachezaji, kazi imeanza

Goli bora la mashindano kutoka kwa Ayoub El Kaabi?

Licha ya ushindi huo kumekuwa na mjadala kuhusu goli bora la mashindano kupatikana mapema. Goli la pili kwa Morocco ambalo lilifungwa kipindi cha pili na Ayoub El Kaabil limekuwa gumzo. Nyota huyo alifunga goli hilo kwa mtindo wa acrobatics. Goli hilo linatajwa kuwa katika orodha ya magoli ambayo yatawania tuzo ya goli bora katika mashindano ya Afcon 2025.
Kadi za njano
Dakika ya 36, Yannick Kari wa Comoros alionyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza faulo mbaya.
Dakika ya 45+3 Brahim Diaz wa Morocco alionyeshwa kadi ya njano kwa kucheza faulo mbaya.
Dakika ya 78, Jawad El Yamiq wa Morocco alionyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 90, Sofyan Amrabat wa Morocco alionyeshwa kadi ya njano
SOMA HII: Hawa hapa wachezaji 5 wa kuchungwa AFCON 2025 Morocco

Msimamo kundi A

1. Morocco pointi 3 wamecheza mchezo nmoja
2. Mali pointi 0 hawajacheza mchezo hata mmoja
3. Zambia pointi 0 hawajacheza mchezo hata mmoja
4. Comoros pointi 0 wamecheza mchezo mmoja.
Ratiba AFCON 2025, Jumatatu, Desemba 21,2025
Mali vs Zambia, saa 11:00 jioni
Afrika Kusini vs Angola saa 2:00 usiku
Misri vs Zimbabwe, saa 5:00 usiku
Hitimisho
AFCON 2025 Morocco 2-0 Comoros huu ni mwanzo wa burudani. Kuna timu 24 ambazo zinawania taji zikiwa kwenye hatua ya makundi. Kila kundi zipo timu nne ambazo zinasaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

