- Hugo Ekitike alifunga goli la ushindi huku Alexander Alex Isak mfungaji wa goli la kuongoza akipata majera ya goti.
- Tottenham Hotspurs 1-2 Liverpool mchezo wa funga 2025 Premier League ugenini
- Arne Slot Kocha Mkuu wa Liverpool kwenye mtihani mzito
Tottenham Hotspurs 1-2 Liverpool ni matokeo rasmi ya mchezo wa Premier League uliochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspurs. Alexander Alex Isak mfungaji wa goli la kwanza katika mchezo huo alipata maumivu ya goti. Mchezaji Romero wa Tottenham alionyeshwa kadi nyekundu ikiwa muda mfupi umebaki mchezo kufika tamati.
SOMA HII: Tottenham vs Liverpool: Live score, line-ups, h2h, vikosi, utabiri
Bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Tottenham Hotspurs 1-2 Liverpool magoli yalifungwa kipindi cha pili

Mpaka ubao unasoma Tottenham Hotspurs 1-2 Liverpool, Desemba 20,2025 kasi ilianza kuonekana kipindi cha pili ambapo kipindi cha kwanza timu zote zilimaliza bila kucheka na nyavu. Magoli ya Hugo Ekitike dakika ya 66 na Alexander Isak dakika ya 56 yalikuwa ya ushindi kwa Liverpool.
Richarlison alipachika goli pekee kwa Tottenham dakika ya 83. Mchezaji huyo alianzia benchi alipoingia alifunga. Ilikuwa hivyo hata kwa Liverpool mchezaji aliyefunga goli la kuongoza alitokea benchi na alipoingia alifunga.
Kadi nyekundu mbili
Mchezo huo Tottenham walionyeshwa kadi nyekundu wachezaji wawili Xavi Simon dakika ya 33 na Romero dakika ya 90+3.
Kadi za njano

Kadi za njano zilimwaga kwa wachezaji wa timu zote mbili ambapo ni Cristian Romero alionyeshwa kadi ya njano ya kwanza dakika ya 65 na ile ya pili dakika ya 90+3 ikaleta kadi nyekundu. Micky Van den Ven dakkka ya 85 alionyeshwa kadi ya njano , Rodrigo Bentancur dakika ya 90+5 kwa Tottenham.
Ibrahim Konate alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 77, Dominik Szoboszlai dakika ya 82 na Alexis Mac Allister dakika ya 90+7 kwa upande wa Liverpool walionyeshwa kadi za njano.
SOMA HII: Mohamed Salah aomba radhi Liverpool: Takwimu zake hizi hapa EPL

Mabadiliko
Ni Conor Bradley dakika ya 46 alimpisha Alexander Isak ambaye alikuwa super sub kwa kufunga goli la uongozi dakika ya 56. Alexander Isak alitoka dakika ya 60 akimpisha Jeremie Frimpong dakika ya 90.
Andy Robertson aliingia akichukua nafasi ya Hugo Ekitike dakika ya 90+9 na Treymaurice Nyoni aliingia dakika ya 90+10 akichukua nafasi ya Florian Wirtz ilikuwa ni kwa upande wa Liverpool.
Brenna Johnson dakika ya 58 aliingia akichukua nafasi ya Mohammed Kudus, Joao Palhinha aliingia dakika ya 71 akichukua nafasi ya Archie Gray, Wilson Odobert aliingia dakika ya 71 akichukua nafasi ya Lucas Gray na Richarlison aliingia dakika ya 80 akichukua nafasi ya Randal Kolo Muani.
SOMA HII: Alexander Isak atua Liverpool: Avunja rekodi ya uhamisho Premier League, kwa £130m

Msimamo 5 bora Premier League

1. Arsenal pointi 39 baada ya mechi 17
2. Manchester City pointi 37 baada ya mechi 17
3. Aston Villa pointi 33 baada ya mechi 16
4. Chelsea pointi 29 baada ya mechi 17
5. Liverpool pointi 29 baada ya mechi 17.
Hitimisho
Tottenham Hotspurs 1-2 Liverpool ulikuwa ni mchezo wenye ubabe mwingi uwanjani. Funga kazi kwa 2025 vijana wa Arne Slot wamekomba pointi tatu ugenini. Bradley na Isak kwa Liverpool wapo chini ya uangalizi baada ya kupata maumivu.

