Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 kwa timu hizi kutupa karata uwanjani. Ni Desemba 23 wawili hawa kutoka kundi C watakuwa uwanjani kusaka ushindi. Tayari Taifa Stars imewasili inayofundishwa na Miguel Gamondi ipo Morocco kwa maandalizi ya mwisho kwenye mashindano haya makubwa.
SOMA HII: AFCON 2025: Joto lapanda Morocco, Jeshi la Tanzania laweka kambi Misri
Zamu yako kushinda sasa hivi, cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Ni Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025, ratiba ipo hivi

Nchini Morocco, Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 kwa timu hizi kutoka kundi C. Baada ya mchezo huo zipo mechi nyingine kali zitachezwa. Ratiba inaonyesha kuwa mchezo wa kwanza kwa Taifa Stars utachezwa saa 2:30 usiku. Desemba 27 itakuwa ni Tanzania vs Uganda, saa 2:30 usiku na Desemba 30 Tanzania vs Tunisia saa 1:00 usiku.
Haya hapa makundi ya AFCON 2025
Kundi A
Morocco, Mali, Zambia, Comoros
Kundi B
Misri, Afrika Kusini, Angola, Zimbabwe
Kundi C
Nigeria, Tunisia, Uganda, Tanzania
Kundi D
Senegal, DR Congo, Benin, Botswana
Kundi E
Algeria, Burkina Faso, Guinea ya Ikweta, Sudan
Kundi F
Ivory Coast, Cameroon, Gabon, Msumbiji
SOMA HII: Hawa hapa wachezaji 5 wa kuchungwa AFCON 2025 Morocco

Kambi Taifa stars ilianzia Misri

Kikosi cha Taifa Stars kabla ya kuelekea Morocco kwanza kiliweka kambi ya muda nchini Misri. Mbinu za Kocha Mkuu Miguel Gamondi zilianza kufundishwa hapo. Lengo la kambi hiyo ilikuwa ni kupata mazingira bora ya mazoezi.
Bendera mikononi mwa Stars
Desemba 18, 2025 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paramagamba Kabudi alikabidhi bendera ya Taifa kwa timu ya Taifa kwa kwa ajili ya kuelekea Morocco kwenye Fainali za AFCON 2025. Desemba 19,2025 kikosi cha Stars kiliwasili nchini Morocco kwa maandalizi ya mwisho.
Mbwana Samatta kambini
Nahodha Mbwana Samatta aliwasili kambini nchini Misri Desemba 17. Aliungana moja kwa moja na wachezaji wengine kwa maandalizi zaidi. Mbali na Samatta winga Simon Msuva naye ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi.
Mazoezi yaanza Morocco
Mara baada ya kuwasili nchini Morocco timu hiyo ilipata muda wa kufanya mazoezi. Ni kwenye Uwanja wa Academic Mohammed VI, Rabat, Morocco waliutumia kwa mazoezi. CAF Total Energies AFCON 2025 inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Mwalimu ajumuishwa fasta
Kocha Miguel Gamondi amemuita mshambuliaji Selemani Mwalimu kwenye kikosi cha wachezaji 28. Awali mshambuliaji huyo hakuwa kwenye orodha ya watakaocheza AFCON 2025 Morocco. Mwalimu alichagulikuwa kuchukua nafasi ya Abdul Suleiman wa Azam FC ambaye aliumia hiyo ilikuwa Desemba 13,2025.
SOMA HII: Yanga SC hawana utani wamerejea kazini 2025/26/ Orodha ya wachezaji waliopo AFCON

Kikosi cha Taifa Stars
Yakoub Suleiman- Simba SC
Hussen Masalanga-Singida Black Stars
Zuber Foba-Azam FC
Bakari Nondo- Yanga SC
Shomari Kapombe-Simba SC
Lusajo Mwaikenda-Azam FC
Mohamed Hussen- Yanga SC
Nickson Kibabage- Singida Black Stars
Alphonce Mabula-Shamakhi , Azerbaijan
Wilson Nangu- Simba SC
Novatus Dismas-Goztepe FC, Uturuki.
Kelvin Nashon-Pamba Jiji
Pascal Msindo-Azam FC
Ibrahim Abdallah- Yanga SC
Haji Mnoga-Salford City, Uingereza
Dickson Job- Yanga SC
Habib Idd- Singida Black Stars
Tarryn Allarakha- Rochdale AFC, Uingereza
Charles M’mombwa- Floriana FC, Malta
Yusuph Kagoma- Simba SC
Feisal Salum- Azam FC
Morice Abraham- Simba SC
Seleman Mwalimu- Simba SC
Idd Suleiman- Azam FC
Kibu Dennis- Simba SC
Mbwana Samatta- Le Havre AC, Ufaransa.
Kelvin John-Aalborg BK, Denmark
Simon Msuva-Al-Talaba, Iraq

Hitimisho
Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Wababe hawa kutoka kundi C kila mmoja anahitaji kufungua pazia kwa ushindi. Je nani ataanza kwa kicheko? Endelea kufuatilia ukurasa huu matokeo utayapata mara baada ya mchezo kutamatika.

