• Taarifa mpya zimefichua kuwa nyota wa kikosi cha Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah amewaomba radhi nyota wenzake.
• Hii ni kufuatia mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kugeuka gumzo.
• Salah kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kwenye mashindano ya (AFCON).
Imefichuka kuwa nyota wa kikosi cha Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah amewaomba radhi nyota wenzake kufuatia mahojiano aliyofanya na kugeuka gumzo. Salah kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kwenye mashindano ya (AFCON). Nyota huyo alilazimika kuachwa kikosini katika mchezo mmoja na kupigwa benchi kwenye michezo mingine minne.
SOMA HII PIA: Premier League Table & Standings 2025-2026 Season
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Curtis afichua ishu ya Salah kuomba radhi
Akizungumza na kituo cha michezo cha Sky Sport nyota mwenzake wa Liverpool, Curtis Jones amesema: “Mo alituomba radhi na akasema ikiwa nimewaathiri mtu yeyote, au kuwafanya mjisikie vibaya kwa namna yoyote, naomba radhi. Huyo ndiye alivyo, ni mtu anayesimamia maneno yake. Naweza kuzungumza tu, kwa kumjua Mo jinsi alivyo nasi na jinsi alivyotenda kuhusu hilo.
“Alikuwa chanya. Alikuwa yuleyule Mo, alikuwa na tabasamu kubwa usoni na kila mtu alikuwa sawa kabisa akiwa naye. Nadhani ile interview ni sehemu tu ya kutaka kuwa mshindi. Aliomba radhi, tunaendelea mbele, tunaendelea kusonga.”
Arejeshwa kikosini, atoa asisti ya bao

Baada ya vita ya maneno ya muda kati ya Salah na kocha wake, Arne Slot hatimaye staa huyo alirudishwa kikosini kwenye mchezo uliopita dhidi ya Bournemouth. Katika mchezo huo Salah alitoa asisti ya bao moja kati ya mawili yaliofungwa na Hugo Ikitike. Asisti hiyo ilimfanya kuandika rekodi ya kuwa miongoni mwa mastaa waliotoa asisti nyingi zaidi.
SOMA HII ZAIDI: MANCHESTER UNITED VS LIVERPOOL WEKA MKEKA SPORTPESA KINAWAKA OLD TRAFFORD LEO
Hizi hapa takwimu za Mohamed Salah
Wasifu binafsi;
Jina: Mohamed Salah
Umri: 15/06/1992 (33)
Mahali: Misri Nagrig, Basyoun
Uraia: Misri
Urefu: 1,75 m
Nafasi: Winga
Mechi za timu ya Taifa/magoli 107 / 61
SOMA HII PIA: Premier League kumechangamka Aprili 26, Chelsea vs Everton
Tuzo binafsi

Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya x1
Ligi Kuu England x2
Uefa Supercup 1
Takwimu zake msimu huu

Ligi Kuu England: Mechi 20, magoli 5, asisti 4
UEFA: Mechi 5, asisti 1

