- Al Ahly vs Yanga SC CAF Champions League kituo kinachofuata Januri 23,2026 hatua ya makundi
- Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika
- Kariakoo Dabi inanunikia Machi Mosi 2026, Uwanja wa Mkapa
Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League katika msako wa ushindi. Wababe hao wanafundishwa na Kocha Mkuu Pedro Goncalves imeendeleza ubabe wake kuvuna pointi. Mchezo wa funga 2025 kwenye ligi ilikuwa ugenini ikishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Coastal Union. Katika CAF Champions League ipo hatua ya makundi inakibarua cha kukabiliana na Al Ahly ya Misri.
SOMA HII: Ligi Kuu Bara NBC: Yanga SC haikamatiki, Azam yaichakaza Simba SC
Je hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League matokeo haya hapa

Ni wazi kuwa Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League yenye ushindani mkubwa. Mshambuliaji Prince Dube alifunga goli pekee la ushindi dhidi ya Coastal Union. Hapa tunakuletea matokeo na ratiba kwa Yanga SC namna hii:-
Matokeo ya Yanga SC NBC Premier League
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, Septemba 24, 2025
Mbeya City 0-0 Yanga SC, Septemba 24,2025
Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Oktoba 28,2025
Yanga SC 4-0 KMC FC, Novemba 9,2025
Yanga SC 2-0 Fountain Gate, Desemba 4,2025
Coastal Union 0-1 Yanga SC, Desemba 7,2025
SOMA HII: Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Ratiba ya mechi zijazo Jangwani

CAF Champions League hatua ya mtoano
Wiliete SC 0-3 Yanga SC, Septemba 19,2025
Yanga SC 2-0 Wiliete SC, Septemba 26,2025
Silver Strikers 1-0 Yanga SC, Oktoba 18,2025
Yanga SC 2-0 Silver Strikers, Oktoba 25,2025

CAF Champions League Group Stage
Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat, Novemba 22,2025
JS Kabylie 0-0 Yanga SC, Novemba 28,2025
Ratiba za mechi za Yanga SC
Al Ahly vs Yanga SC, CAF Champions League, Januari 23,2026
Azam FC vs Yanga SC, Januri 29,2026 NBC Premier League
Tabora United vs Yanga SC, Februari Mosi 2026, NBC Premier League
Yanga SC vs JKT Tanzania, NBC Premier League itapangiwa tarehe
AS FAR RABAT vs Yanga SC, Februari 6 2026, CAF Champions League
Mtibwa Sugar vs Yanga SC, Februari 9 2026, NBC Premier League
Yanga SC vs JS Kabylie Februari 13,2026, CAF Champions League
Yanga SC vs Dodoma Jiji, Februari 25,2026, NBC Premier League
Yanga SC vs Mashujaa, Februari 26,2026, NBC Premier League.
Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi 2026, NBC Premier League.
SOMA HII: Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League/ Prince Dube afunga goli la ushindi New Amaan Complex

Rekodi za Yanga SC 2025/26

Yanga SC 2025/26 haijapoteza mchezo kwenye mechi za ligi ilizoshuka uwanjani kati ya 6. Ni ushindi kwenye mechi 5 ikiambulia sare katika mchezo mmoja. Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya magoli 12 huku ukuta ukiruhusu kufungwa goli moja.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ina pointi 16. Vinara ni JKT Tanzania katika ligi namba nne kwa ubora Afrika. JKT Tanzania wamekusanya pointi 17 baada ya kucheza mechi 10.
Magoli yakufunga
Yanga SC imefunga magoli 12 katika mechi 6 ambazo ni dakika 540. Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga goli moja kila baada ya dakika 45 ndani ya uwanja. Hati safi ni 5 kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
Mchezo ujao kwa Yanga SC ni dhidi ya Al Ahly ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Januari 23,2026. Utakuwa ni mchezo wa 3 hatua ya makundi ambapo Yanga SC watakuwa ugenini.
CAF Champions League 2025/26
Katika kundi B CAF Champions League ushindani umekuwa mkubwa huku Yanga SC ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo zimepata natokeo katika mechi za mwanzo.

Msimamo wa kundi B
1. Al Ahly pointi 4, mechi 2.
2. Yanga SC pointi 4, mechi 2
3. AS FAR RABAT pointi 1, mechi 2
4. Js Kabylie pointi 1, mechi 2
Hitimisho
Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League ikiwa na kazi kutetea taji la ubingwa. Timu nyingine ambayo haipoteza mechi ni Azam FC. Je wababe hawa wataendeleza rekodi mpaka mwisho wa msimu? Tusubiri na tuone matokeo yatakuwa hapa.

