Everton vs ArsenalEverton vs Arsenal
  • Vinara wa msimamo wa Ligi Kuu England (EPL), Arsenal kesho Jumamosi wanatarajia kukiwasha tena ugenini.
  • Hii ni kuelekea mchezo mkali wa Everton vs Arsenal utakaopigwa kwenye Uwanja wa Hill Dickinson.
  • H2H Arsenal wamekuwa na nyakatio njema wakiibuka na ushindi mara 35 kati ya 57.

Vinara wa msimamo wa EPL Arsenal kesho Jumamosi wanatarajia kukiwasha tena ugenini. Ni katika mchezo mkali wa Everton vs Arsenal. Kiungo wa zamani wa Everton, Mikel Arteta anatembelea uwanja mpya wa Everton Hill Dickinson, kwa mara ya kwanza Jumamosi usiku. Hii ni vita ya timu inayosaka ubingwa wa EPL msimu huu, dhidi ya timu iliyo kwenye hali mbaya kwa sasa.

SOMA HII PIA: Premier League Games: A Season of Drama, Decisions, and Destiny

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Everton vs Arsenal

Huu unakuwa mchezo wa 58 kwa timu hizi kukutana kwenye michezo ya ushindani. Katika michezo 57 iliyopita Arsenal wamesimika ubabe wao, wakishinda mechi 35. Everton wao wameshinda mechi 11 tu, huku mechi 11 zikisha kwa matokeo ya sare.

Mechi 5 zilizopita za Everton

Mastaa Everton
Mastaa Everton

Chelsea 2-0 Everton

Everton 3-0 Nottingham Forest

Bournemouth 0-1 Everton

Everton 1-4 Newcastle United

Manchester United 0-1 Everton

Mechi 5 zilizopita za Arsenal

Arsenal 2-1 Wolverhampton Wanderers

Club Bruges 0-3 Arsenal

Aston Villa 2-1 Arsenal

Arsenal 2-0 Brentford

Chelsea 1-1 Arsenal

Vikosi tarajiwa vya Arsenal na Everton

Kikosi Everton
Kikosi Everton

Everton

Kipa: Pickford

Walinzi: O’Brien, Keane, Tarkowski, Mykolenko

Viungo: Garner, Iroegbunam, Dibling, Alcaraz,

Washambuliaji: Grealish, Barry

Arsenal

Kipa: Raya

Walinzi: Timber, Saliba, Hincapie, Calafiori

Viungo: Odegaard, Zubimendi, Rice, Saka

Washambuliaji: Gyokeres, Trossard

Habari za timu

Goli la Saka
Goli la Saka

The Gunners kwa Bahati waliibuka washindi dhidi ya Wolverhampton Wanderers wikiendi iliyopita. Kwa upande wa kikosi cha David Moyes kilishindwa kabisa, kuwahimili mabingwa wa Kombe la Dunia la Klabu, Chelsea. Ikumbukwe Arsenal iliyokuwa imara awali imepata clean sheet moja tu katika michezo yao sita ya mwisho ya Ligi Kuu.

SOMA HII ZAIDI: Premier League Games Were on Fire: How Did Arsenal Address Their Goalkeeping Conundrum?

Arsenal na sikukuu za Krismasi

Ushindi kwa Arsenal angalau utawahakikishia kubaki kileleni mwa msimamo, mpaka Krismasi. Lakini kihistoria hilo limekuwa ishara mbaya kwao kwani katika kila moja ya misimu minne ya Ligi Kuu ambapo walikuwa kileleni mpaka tarehe 25 Desemba, walishindwa kutwaa taji. Kwa Everton kama matokeo yatawaendea vibaya, basi kuna uwezekano mdogo sana kwamba wataingia tano bora ya msimamo.

Everton walioko nafasi ya tisa wana upungufu wa pointi mbili tu, kuzipata Crystal Palace, Sunderland, Manchester United na Liverpool. Shukrani kwa mfululizo mzuri wa ushindi wa mechi 4 na vipigo viwili katika michezo yao sita ya mwisho. Kupoteza 2-0 dhidi ya Chelsea katika Stamford Bridge wikiendi iliyopita kuliwazuia Everton kujipenyeza kwenye kusaka nafasi za Ulaya.

Taarifa za majeruhi Everton vs Arsenal

Kikosi cha Arsenal (-)
Kikosi cha Arsenal

Arsenal wanatarajia kumkosa mlinzi wao, Ben White, hii ni kufuatia jeraha la lazima lilitokea ndani ya kipindi cha kwanza. Katika mchezo huo wa ushindi siku ya Jumamosi Wolves, Ben White alitoka nje akiwa na tatizo la misuli ya paja. Taarifa za kitabibu zimeeleza kuwa anatarajiwa kukaa nje kwa angalau mwezi mmoja.

White anaungana na Cristhian Mosquera (kifundo cha mguu), Gabriel Magalhaes (paja), Kai Havertz (goti) na Max Dowman (kifundo cha mguu). Katika chumba cha wagonjwa cha Arsenal ni kama mmoja anaingia, mmoja anatoka kwenye safu ya ulinzi ya Gunners, kwani Riccardo Calafiori amerudi baada ya kusimamishwa kwa mchezo mmoja. Hivyo basi, Jurrien Timber, William Saliba na Piero Hincapie wote watahamia nafasi moja kulia, huku Martin Odegaard na Leandro Trossard wakitarajiwa kurejea zaidi mbele.

Moyes na aliyekuwa mlinzi wake Arteta wanaweza kuelewana upande wa majeraha. Nguzo ya Everton, Kiernan Dewsbury-Hall alilazimika kutoka dakika ya 16 mechi dhidi ya Chelsea akiwa na tatizo la misuli ya paja. Taarifa za awali zimeeleza kuwa atakosa mchezo huu.

Pamoja naye, wapo Nyota wawili muhimu, Iliman Ndiaye na Idrissa Gueye ambao wameenda kwenye majukumu ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Moyes angalau amethibitisha kuwa Jack Grealish yuko fiti na yupo tayari, baada ya taharuki ya jeraha la paja. Merlin Rohl (kinena) pia amefanya mazoezi na yuko njiani kupatikana, lakini Jarrad Branthwaite (paja) na Seamus Coleman (paja) hawatashiriki katika mchezo huu.

SOMA HII PIA: Premier League kumechangamka Aprili 26, Chelsea vs Everton

Hitimisho

Everton vs Arsenal, mchezo huu utaamuliwa zaidi na ubora na uzoefu wa kimbinu kwa kuwa unawakutanisha makocha bora. Moyes wa Everton ni kocha mzoefu na mkongwe ambaye atakutana na mchezaji wake wa zamani, Mikel Arteta anayeinoa Arsenal kwa sasa. Arsenal wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka na ushindi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.