- Simba SC 2025/26 mwendo wake ni wa kuchechemea ikipoteza mchezo wa kwanza kwenye ligi dhidi ya Azam FC.
- Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SC, Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa, Machi Mosi, 2026.
- Zijue mechi tano ambazo wachezaji hao watakosekana na ratiba kamili ilivyo.
Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SC kutokana na kufungiwa mechi 5. Wachezaji hao Desemba 16,2025 walipewa adhabu hiyo kutokana na makosa ya kinidhamu. Taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) ilieleza wachezaji walifanya matukio mchezo wa Simba SC 0-2 Azam FC, Uwanja wa Mkapa, Desemba 7, 2025.

Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SC, Kariakoo Dabi

Kutona na adhabu hiyo Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SC ikiwa hakutakuwa na mabadiliko ya ratiba. Ratiba ya ligi namba nne kwa ubora Afrika inaonyesha kuwa Dabi ya Kariakoo inatarajiwa kuchezwa Machi Mosi 2025.
Zipo mechi nyingine ambazo hazijapangiwa tarehe nazo wachezaji hao watazikosa. Kupungua kwa mechi za ligi itategemea kama kutakuwa na mechi za Kombe la CRDB Federation Cup. Mshambuliaji namba moja wa Simba SC Sowah na kiungo wa Kante watakuwa jukwaani na wanatakiwa kulipa faini milioni moja kwa kila mmoja.
SOMA HII: Jonathan Sowah atoa ahadi nzito Simba SC / Magoli aliyofunga / Kambi Misri kinachoendelea

Hizi hapa mechi za ligi watakuwa jukwaani Sowah na Kante
Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa Mkapa, Machi Mosi, 2026.
Simba SC vs Mashujaa FC, Februari 25,2026, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo.
Machi 5 2026, Simba SC vs Coastal Union, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo.
Dodoma Jiji vs Simba SC hii itapangiwa tarehe, Uwanja wa Jamhuri.
Pamba Jiji vs Simba SC hii itapangiwa tarehe, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
SOMA HII: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya

Mtambo wa mabao Simba SC jukwaani
Ndani ya kikosi cha Simba SC, Jonathan Sowah ni kinara kwa kufunga mabao mengi. Ni mabao 3 amefunga kwenye ligi ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuvaa uzi wa mnyama. Uwezekano mkubwa akaukosa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kukosekana kwake kuna uwezekano nafasi yake akacheza Steven Mukwala ama Seleman Mwalimu ambaoni washambuliaji. Adhabu hii ni mara ya kwanza kwa Sowah akiwa na uzi wa Simba SC. Ikumbukwe kwamba alisajiliwa na timu hiyo akitokea Singida Black Stars.
Kiungo wa kazi Kante

Kante ni miongoni mwa viungo tegemeo ndani ya kikosi cha Simba SC. Uwezo wake katika kuzuia hatari na kutimiza majukumu kwa wakati utakosekana kwenye mechi 5 zijazo. Benchi la ufundi litakuwa na kazi kumtafuta mbadala halisi kwa muda ambao atakosekana.
Licha ya kuwa na uwezo mkubwa kwenye eneo la ukabaji nidhamu yake haijawa imara. Kuna kazi nyingine kwa benchi kuzungumza na wachezaji wote kuhusu umuhimu wa kuwa waungwana. Ni Yusuph Kagoma anapewa nafasi kubeba mikoba ya Kante.
Kuhusu adhabu zao
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Sowah alimpiga kiwiko mchezaji Himid Mao. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Kante alimpiga teke kwa makusudi mchezaji Feisal Salum wakati wa mchezo huo. Katika mchezo huo Simba SC ilipoteza pointi 3 muhimu.

Ujumbe wa TPLB
TPLB imevikumbusha vilabu kuwaambia wachezaji wanapaswa kuwa waungwana uwanjani. Ukumbusho huo unakuja kutokana na mfululizo wa matukio ya wachezaji kufanya vitendo visivyo ya kiuanamichezo kwa wanamichezo ikiwemo kupiga. Pamoja na kuhatarisha usalama wa wachezaji, matukio hayo yamekuwa yakileta taswira mbaya kwa ligi jambo ambalo linaweza kuishusha hadhi.
Hitimisho
Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi, Uwanja wa Mkapa. Simba mweusi Sowah utakuwa mchezo wa pili kuikosa Yanga SC alikosekana katika Ngao ya Jamii. Kante yeye utakuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya msimu wa 2025/26.

