Msimamo wa LigiMsimamo wa Ligi
  • Msimamo wa ligi Kuu NBC baada ya mechi za Alhamisi hii unazidi kushtua watu.
  • Msimu wa 2025/26 umeanza kwa ushindani mkali, timu kadhaa ikiwemo JKT Tanzania zinaonekana kuanza kwa kishindo.
  • Yanga SC na Simba SC nao unaweza kusema gari limewaka!

Msimamo wa ligi Kuu NBC baada ya mechi za leo Alhamisi, unaonyesha kuwa msimu huu wa 2025/26 umeanza kwa ushindani mkali. Timu kadhaa zimejipanga vizuri kushindana kwa nguvu zote. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hivi sasa, JKT Tanzania inaongoza msimamo huku Yanga SC na Simba SC zikija kwa kasi. Makala hii inachambua kwa ufupi mambo muhimu kwenye msimamo huo.

SOMA HII PIA: Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League 2025/26/ Highligts, magoli, msimamo

Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

JKT Tanzania vinara

Kikosi cha JKT
Kikosi cha JKT

JKT Tanzania ndio inaongoza msimamo, baada ya kukusanya pointi 17 katika michezo 10 waliyocheza. Kwa Daraja la timu yao unaweza kusema hii ni hatua kubwa, lakini huenda wakaanguka kutoka walipo pale kila timu itakapocheza mechi 10. JKT Tanzania imekuwa timu yenye utulivu na nidhamu, na huenda wana jambo lao msimu huu.

Pamba Jiji, Mashujaa nao hawavumi lakini wamo

Tangu kuanza kwa msimu huu, timu hizi nazo zimetoa ishara kuwa wanaweza kuingia katika mzunguko wa kushindania nafasi za juu. Mpaka sasa Pamba wako nafasi ya 2 na pointi zao 15, huku Mashujaa wakishika nafasi ya nne na pointi zao 13 sawa na Yanga SC.

SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 hii hapa | Mechi za Dabi, kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani

Simba SC na Yanga SC gari limewaka

Sowah akishangilia bao
Sowah akishangilia bao

Vigogo wawili wa soka nchini Simba SC na Yanga SC zinaonekana kuzidi kuimarika. Licha ya kuanza kwa mwendo wa tofauti, na kubanwa na mashindano ya kimataifa lakini kila timu sasa inazidi kuweka nguvu kushinda mechi zake. Simba SC mpaka sasa wameandikisha asilimia 100 ya ushindi, huku Yanga wakiangusha pointi 2 pekee.

Ingawa zimecheza mechi chache mfano, Young Africans wamecheza mechi 5 tayari wamekusanya pointi 13. Simba SC, licha ya kucheza mechi chache ambazo ni 4 tu, lakini tayari wamekusanya pointi 12. Huu moto unaonekana utazidi kuwaka siku za usoni.

Inatabiriwa msimamo kuwa na mabadiliko makubwa

Msimamo wa Ligi Kuu NBC
Dube X Pacome

Kwa kuwa mechi ni chache ambazo zimechezwa msimu huu, hii ina maana msimamo unaweza kubadilika sana. Ni uwezekano mkubwa kuona mabadiliko makubwa. Mabadiliko haya yanatarajiwa kwa timu ambazo zina mechi nyingi mbele.

SOMA HII PIA: JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26/ Highlights, goal

KMC hali yao ni tete

Kikosi cha KMC wanapumulia mashine kwani wameambulia pointi 4 tu, katika michezo 9 waliyocheza mpaka sasa. Takwimu hizo zinawafanya kuwa timu ya mwisho kwenye msimamo. Hii ni wazi inawasha kengele kwa mabosi wa timu. Tayari kumeripotiwa uwezekano wa mabadiliko ya benchi la ufundi.

Hitimisho

Kwa kuangalia msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, utaona kuwa msimu huu wa 2025/26 unaashiria ligi itakuwa na ushindani mkubwa. Mpaka sasa timu kama JKT Tanzania, Young Africans, Simba, Pamba Jiji na Mashujaa FC zinaonekana kuonesha nguvu ya kushindana. Hata hivyo, bado ni awamu ndogo ya ligi imechezwa. Hivyo mafanikio ya sasa hayahakikishi chochote ila inaweza kutoa dondoo za awali.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.