- Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amewaomba mashabiki kuujaza Uwanja wa Benjamini Mkapa.
- Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi katika mechi za awali.
- Petro de Luanda watakuwa ugenini kusaka pointi tatu muhimu mbele ya wenyeji wao Simba SC.
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi msimu wa 2025/26 kwenye mechi za mwanzo. Wababe wote wawili wanahitaji pointi tatu huku mnyama mwenyeji akibainisha atashinda. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC aliweka wazi hilo ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo huo Jumapili.
Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi kwa nini?

Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi katika mechi za kwanza. Kuna mechi 8 ambazo zinachezwa hatua ya makundi, mchezo wa ufunguzi ni ule wa kundi C Novemba 21,2025, Al Hilal Omdurman vs MC Alger. Mechi ya mwisho kukamilisha mechi moja kwa kila timu itakuwa Novemba 23,2025.
Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC maoni yake

“Tuna tukio letu la kihistoria siku ya Jumapili. Jumapili tuna mechi nzito, tuna kazi na shughuli pevu kwelikweli kwa maana hiyo tumekuja hapa kuomba msaada wenu wa kuja uwanjani ili tufanye vizuri kupata alama tatu na kuanza vizuri.
“Mechi ya Jumapili dhidi ya wapinzani kutoka Angola tusiwachukulie poapoa, licha ya kuvuka viunzi vigumu kwelikweli, kuvuka mechi ngumu kwelikweli lakini kama unafikiria mechi hii itakuwa nyepesi basi unafanya vibaya. Ili tupate ushindi ni muhimu kila mmoja kuja uwanjani tushinde pamoja.
“Tunahitaji kuanza vizuri hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hatuwezi kuanza vizuri kama kila mmoja hatimizi majukumu yake kwa asilimia 100. Viongozi waatimiza jukumu lao na wewe shabiki wa kawaida timiza wajibu wako na wajibu wako ni kununua tiketi na kuja uwanjani.
“Hatuna mashaka sisi tutashinda kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu lakini ili tushinde vizuri ni wewe kuja uwanjani. Kwanza unabaki nyumbani unafanya nini? Awe babu, awe bibi, awe kijana, awe mvulana hata wewe binti mdogo njoo Benjamin Mkapa. Kama huna kiingilio mfate mwenzio aokoe jahazi na wewe mwenye kipato cha kutosha mfate mwenzio ambaye hana mje Mkapa kwa pamoja.
“Tuna kila sababu ya kutamba, mjini tumebaki peke yetu. Njia rahisi zaidi ya kuja uwanjani ni kuja kwa mtindo wa tawi, mnakata tiketi na kukusanya nauli kisha mnakuja pamoja. Na Jumapili hakutakuwa na foleni maana wengine wamehama mjini hapa, tumebaki peke yetu,”.
SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025/ Taarifa kuhusu Camara na Hamza

Kundi la Simba SC kimataifa
1. Petro de Luanda
2.Esperance
3. Simba SC
4. Stade Malien
Viingilio mechi ya Simba SC Uwanja wa Mkapa

Viingilio vya mchezo ni Tanzanite – Tsh. 250,000, Platinum – Tsh. 150,000, VIP A – Tsh. 30,000, VIP B – Tsh. 20,000, VIP C – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000.
SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Live score, H2H

Jezi za kimataifa zazinduliwa rasmi
Novemba 20,2025 uongozi wa Simba SC ulizindua jezi maalumu ambazo zitatumika katika anga la kimataifa. Tayari uzi huo mpya upo madukani ili mashabiki wavae uzi huo mpya. Mchezo wa kwanza kutumika itakuwa Uwanja wa Mkapa Novemba 23,2025.
Hitimisho
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi msimu wa 2025/26. Baada ya ngwe kukamilika kila timu zitakuwa zimebakisha mechi 5 kufunga hesabu za makundi. Huu ni msako wa hatua ya robo fainali. Katika kila kundi timu mbili za juu zinakwenda hatua inayofuata.

