Feisal na kocha NabiFeisal na kocha Nabi
  • Joto la usajili wa Ligi Kuu Bara limezidi kupanda, ikiwa zimebaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili.
  • Feisal Salum ni jina lililoshtua mapema tetesi hizo kwa mara nyingine tena.
  • Vigogo wazito wamwekea mezani ofa ya Bilioni 4.8 kumng’oa Azam FC.

Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kwenye Ligi Kuu Bara, joto limeanza kupanda. Miongoni mwa taarifa kubwa ya kushtua ni ile ya kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’. Taarifa kutoka nchini Libya zimethibitisha kuwa, klabu ya Al Ahli Tripoli imetuma ofa nzito kumng’oa Chamazi.

SOMA HII PIA: Azam FC na usajili wa kimkakati kwa Feisal Salum 2025/26 | Orodha ya wachezaji wapya hii hapa

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu Feisal Salum ‘feitoto’ na uhamisho kwenda Al Ahli Tripoli

Taarifa ambazo zimethibitishwa na mchambuzi, Hans Raphael zinaeleza kuwa, Tripoli wametenga kiasi cha Bilioni 4.8 kuinasa saini ya Feisal. Akizungumzia dili hilo, Hans amesema: “Waarabu wamemuahidi Fei Toto, ofa kubwa ya ‘Sign on fee’ kubwa sana, ambayo imeambatana na mkataba wa miaka mitatu.

“Kama Feisal atajiunga na Tripoli atavuna zaidi ya bilion 10 kupitia (sign on fee na mshahara). Ikumbukwe Fei amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu, ndani ya kikosi cha Azam FC.

Tripoli yatuma ofa 2 kwa Feisal

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa uongozi wa Azam FC wametutonya kuwa, hii ni ofa ya pili ya Tripoli kwa Feisal. Awali Tripoli walituma ofa ya kwanza yenye thamani ya $800,000, sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 ambayo ilikataliwa na Azam FC. Sasa mabosi wa kikosi hicho wameongeza dau kufikia $2,000,000 sawa na Tsh 4.8 bilion. Tripoli wako tayari kulipa hela hiyo haraka sana ili kukamilisha dili hilo.

Azam kulipwa 10%

Kama sehemu ya kukamilisha dili hilo, pia Tripoli wako tayari kuweka kipengele cha Azam kupata 10% ya mauzo endapo Tripoli itamuuza Feisal huko mbeleni. Kambi ya Feisal inaeleza kuwa Nyota huyo yuko tayari kuondoka Azam, ili kutafuta maisha Libya. Tusubiri kuona je, dili hilo litafanikiwa.

Taarifa binafsi za mchezaji: Umri na takwimu za mabao kimataifa

Feisal Salum
Feisal Zanzibar

Kuzaliwa: 11/01/1998 (27)

Mahali: Zanzibar

Urefu: 1,78 m

Uraia: Tanzania

Nafasi: Kiungo

Klabu: Azam FC

Azam FC

Alijiunga: 01/07/2023

Mkataba unaisha: 30/06/2027

SOMA HII ZAIDI: Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu yake iko hivi

Takwimu

Feisal Tuzo CHAN
Feisal Tuzo CHAN

Akiwa na jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal amefanikiwa kutumikia katika michezo takribani 52. Kwa mara ya kwanza aliitwa kikosini mwaka 2018. Akiwa na kikosi cha timu hiyo amekuwa akitumia jezi namba 6.

Hitimisho

Feisal ni miongoni mwa wachezaji bora katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa. Nyota huyo amekuwa anazivutia klabu kubwa Afrika, baadhi ya timu hizo ni Simba SC, Yanga SC, Kaizer Chiefs. Kama Feisal atakubali ofa hii, huenda akaweka rekodi kubwa ya usajili ghali bongo.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC wamefungukia kuiwinda saini ya Feisal Salum kiungo wa Azam FC, Yanga SC nao vitani

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.