- Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza kutimua vumbi rasmi wikiendi hii.
- Huko viziwani Zanzibar kutakuwa hapatoshi, ambapo kutapigwa mchezo mkali wa Yanga SC vs AS FAR.
- Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Jumamosi ya Novemba 22, 2025.
- Kuelekea mchezo huo, uongozi wa Yanga umetoa tamko zito.
Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025 mchezo utakaopigwa Jumamosi 22 Novemba 2025, visiwani Zanzibar tayari umekuwa gumzo. Mchezo huu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex. Kuelekea mchezo huo uongozi wa Yanga SC leo umetoa tamko zito.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025, Wananchi kutua Zanzibar kesho Jumanne

Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe umesema kikosi chao kitasafiri kesho Jumanne kwenda Zanzibar. Kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuwa na mastaa wote, isipokuwa baadhi ambao bado hawajarudi kutoka kwenye majukumu ya timu za taifa.
“Yanga SC itaelekea Zanzibar hapo kesho Jumanne kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FAR Rabat. Timu itaondoka saa tatu asubuhi kwa njia ya boti. Baadhi ya wachezaji kama Prince Dube, Celestine Ecua, Lassine Kouma waliokuwa bado kwenye majukumu ya timu zao za taifa hawatakuwepo kwenye safari hii ya kesho.
“Lakini tayari uongozi umeshaweka taratibu zote vizuri, ili wachezaji hawa wasafiri na kuungana na timu Zanzibar moja kwa moja. Wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Tanzania wamesharejea na ni sehemu ya safari ya kesho. Niwaombe Wazanzibar kujitokeza kwa wingi, kuipokea timu kesho,” amesema Ali Kamwe.
SOMA HII ZAIDI: Habari za usajili wa NBC – Kocha Pitso Mosimane ajiunga na Yanga SC U11, 13 & 15
Kuhusu jezi mpya za Yanga SC hatua ya makundi
Kuhusu jezi zitakazotumika kwenye hatua ya makundi, Kamwe amesema: “Jezi mpya za Yanga kwa ajili ya msimu wa Ligi ya Mabingwa zitazinduliwa na kuanza kuuzwa siku ya Alhamisi. Nawakumbusha kuwa jezi hizi ni maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa, hivyo mzigo hautakuwa mkubwa sana. Wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajipatia jezi zao mapema.
Yanga SC vs AS FAR tiketi zimeanza kuuzwa
Kuhusu utaratibu wa tiketi za kushuhudia mchezo huo, Kamwe ameendelea kusema: “Hakikisha unapata Tiketi yako mapema, tayari zimeshaanza kuuzwa Leo kwenye vituo mbalimbali na kwa njia ya mtandao. Kwa ambao mko Zanzibar, kadi zenu mtatumia zilezile, kama ulipoteza, kesho pale nje ya uwanja wa New Amaan Complex kadi zitakuwepo. Njoo mapema nunua tiketi yako mapema, usikose burudani hii kubwa Afrika.”
Yanga wamepangwa dhidi ya timu gani makundi

Katika droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26, ambayo yalipangwa nchini Afrika Kusini Novemba 3, mwaka huu. Yanga SC walipangwa kwenye Kundi B, pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.
SOMA HII PIA: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu
Makundi mengine ni kama ifuatavyo:
Kundi A
RS Berkane kutoka Morocco
Pyramids FC kutoka Misri
Rivers United kutoka Nigeria
Power Dynamos kutoka Zambia
Kundi C
Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini
Al Hilal kutoka Sudan
MC Alger kutoka Algeria
St Eloi Lupopo ya Congo
Kundi D
ES Tunis ya Tunisia
Simba SC kutoka Tanzania
Petro Luanda ya Angola
Stade Malien ya Mali
Yanga SC kuisaka Robo Fainali Zanzibar

Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wake, Ali Kamwe umeutangazia Umma wa soka na mashabiki wake kuwa mechi zao zote tatu za kimataifa hatua ya makundi zitapigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Huu ndio unatarajia kuwa uwanja wao wa nyumbani. Yanga SC vs AS FAR ndiyo karata ya kwanza kwa Yanga Novemba 22, mwaka huu.
Ratiba kamili ya Yanga SC hatua ya makundi CAF Champions League

Yanga SC vs AS FAR inatarajiwa kuchezwa Novemba 22, 2025
JS Kabylie vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Novemba 28, 2025
Al Ahly vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Januari 23, 2026
Yanga SC vs Al Ahly inatarajiwa kuchezwa Januari 30, 2026.
AS FAR vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa 6, Februari 2026.
Yanga SC vs JS Kabylie inatarajiwa kuchezwa Februari 13,2026.
Yanga SC vs AS FAR, Kocha Pedro awaandalia Waarabu dozi
Hitimisho
Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025 CAF ni mechi ya kufa na kupona. Licha ya ubora wa AS FAR ambao wanauonyesha katika ligi ya Morocco, bado umadhubuti wa Yanga SC kimataifa umezidi kuimarika. Misimu miwili iliyopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mashabiki wao wanatamani kuona timu inaandika rekodi nyingine kubwa zaidi msimu huu, hasa baada ya kuishia makundi msimu uliopita.

