- Pitso Mosimane amefikia makubaliano na uongozi wa Yanga SC ili kuboresha makocha wa Tanzania.
- Kocha huyu wa zamani wa timu za Al Ahly na Mamelodi Sundowns amekuwa na uhusiano wa karibu na Yanga SC tangu mwaka 2022.
- Ikumbukwe kocha Pitso amewahi kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Klabu mbili tofauti, Al Ahly na Mamelodi Sundowns.
Uongozi wa Yanga SC na kocha Pitso Mosimane umefikia makubaliano maalum ya mashirikiano kwenye ukufunzi wa makocha wa kituo cha Yanga Soccer School. Makubaliano hayo yatamuona kocha Pitso kuchukua jukumu la kuwanoa makocha na kuwapa mbinu katika kulea vijana kwenye kituo hicho. Mkataba huu uliweza kuafikiwa siku ya Jumamosi Novemba 15, 2025.
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Je, bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu Yanga SC na kocha Pitso Mosimane

Yanga SC na kocha Pitso Mosimane wamekuwa na uhusiano wa karibu wa tangu mwaka 2022. Hii ni baada ya Yanga SC kumualika kocha huyo, kwenye tamasha lao kubwa la wiki ya Mwananchi. Ikumbukwe kuwa tamasha hilo hufanyika kila mwaka.
Akizungumzia mpango huo Rais wa Yanga, Hersi Said amesema: “Yanga soccer School ni jukwaa ambalo, linaleta watu wataaluma tofautitofauti. Vijana wanaotengenezwa hapa, wataondoka wakiwa na maarifa ya kutosha. Tunatengeneza vijana wa kesho ambao wanapenda mpira, lakini wanajua vyema na jamii ya kesho itakwenda kuupenda mpira na kuushabikia.
“Niwapongeze sana wazazi ambao wametuamini na kuleta vijana wao. Jukwaa hili ni jukwaa muhimu sana kwa ukuaji wa soka la kizazi cha kesho. Hawa watoto watakwenda kuwa msaada mkubwa kwa familia yao na kwa taifa kiujumla, kupitia soka.
Yanga SC yafungua kituo cha kulea vipaji vya vijana wadogo kwenye soka Tanzania
Katika mpango huo endelevu wa kukuza vijana, Yanga SC wameanza na kituo cha kwanza ambacho kimefunguliwa maeneo ya Upanga, Dar es Salaam. Kituo hicho kitakuwa chini ya usimamizi wa wakufunzi (makocha), ambao watanolewa na kocha Pitso Mosimane. Pitso ni miongoni mwa makocha wenye mafanikio makubwa Afrika, akiwa na rekodi ya kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu za Mamelodi Sundowns na Al Ahly.
Umri gani unapokelewa ‘Yanga Soccer School?’

Rais wa Yanga SC, Hersi ameendelea kusema: “Mradi huo ni mradi endelevu, ambapo tutachukua watoto wenye umri wa chini ya miaka 11 yaani (U-11), chini ya miaka 13 (U-13), na chini ya miaka 15 (U-15). Hatutaishia mkoa wa Dar es Salaam pekee, yake bali tutatanua wigo kwa maeneo mbalimbali Tanzania. Jukwaa hili litatusaidia sana kwenye kuinua vipaji, ambavyo tunaweza kuvitumia kwenye timu zetu za vijana.”
Kuhusu makubaliano ya Yanga SC na Kocha Pitso Mosimane
Hersi ameendelea kusema: “Tumeongea na Kocha, Pitso Mosimane, ambaye amekubali ombi letu la kutoa mafunzo kwa makocha wetu wa vijana. Lengo letu ni kutumia falsafa ya timu yake ya soka na kuimarisha falsafa yetu pia hapa. Tunamshukuru sana Kocha Mosimane kwa kukubali wito wa kujiunga nasi siku hii ya historia.”
Alichosema kocha Pitso Mosimane

“Namshukuru sana Rais wa Yanga SC, Mimi na Injinia ni marafiki wa muda mrefu sana. Niliwahi kuja hapa kwa ajili ya tamasha la siku ya Mwananchi. Ama kwa hakika ilikuwa ni siku pekee na ya kufana sana. Mashabiki wa Yanga wanaipenda sana timu yao. Hongereni sana. Nyie ni mfano wa kuigwa.”
“Siku ya mwananchi Day nilivutiwa sana na mwamko wa mashabiki. Tukiwa kwenye gari nikamwambia Rais wa Yanga anzisha Shule ya Soka. Nimefurahi sana hatimaye leo nipo kwenye uzinduzi. Namshukuru pia rafiki yangu, Arafat Haji, amenipokea vizuri. Yanga ni familia yangu kwa muda mrefu.”
“Pongezi za kipekee kwa rafiki yangu wa muda mrefu sana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine. Mtine ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika. Amefanya kazi kubwa iliyotukuka huko DR Congo, akiwa na Mazembe. Nadhani kila mtu anatambua kuwa, mafanikio ya Mazembe huwezi kusahau mchango wake. Hongera sana kwa kazi kubwa unayowafanyia wana Yanga.”
Je, kocha Rhulani Mokwena ana nini cha kusema kuhusu weledi na ubora wa kocha Pitso Mosimane?
Kocha wa kikosi cha MC Algers, Rhulani Mokwena amesema kocha Pitso Mosimane, ni muumini wa kusimamia ubora wa taaluma yake na amekuwa na ushawishi mkubwa kwa soka la Afrika. Makocha hao wawili waliwahi kuhudumu pamoja katika kikosi cha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, na kutengeneza miongoni mwa timu tishio Afrika. Rhulani amesema uthubutu na uimara wa kocha Pitso umekuwa saababu ya mafanikio ya makocha wengi wenye asili ya Kusini mwa Afrika.
Hitimisho
Makubaliano ya Yanga SC na kocha Pitso Mosimane, yanaendelea kuonyesha dhamira ya wazi ya uongozi wa Yanga SC katika uwekezaji kwenye soka. Vijana watakaotoka kwenye kituo hiki si tu, kwamba wataifaidisha Yanga SC kama klabu, bali taifa kwa ujumla. Yapo mengi ambayo timu nyingine zinaweza kujifunza kupitia hili.

