Tottenham vs Manchester UbitedTottenham vs Manchester Ubited
  • Vigogo wa soka England wanashuka tena Uwanjani wikiendi hii.
  • Mechi kadhaa zinasubiriwa kwa hamu, ikiwemo mbungi la Tottenham vs Manchester United.
  • Hii inatajwa kuwa vita ya kusaka nafasi 4 bora kwenye msimamo, Je United wataendeleza ubabe pale Kaskazini mwa London, Uwanja wa Tottenham Hotspurs.

Vigogo was soka England watakabiliana kwenye pambano kali la Tottenham vs Manchester United. Hii inatajwa kuwa vita ya kusaka nne bora, kwenye msimamo wa ligi hiyo inayozidi kupamba moto. Mechi hii itapigwa Kaskazini mwa London, katika Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Ushindi mzito wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

- x

H2H Tottenham vs Manchester United

Kikosi cha Spurs
Kikosi cha Spurs

Timu hizi zimekutana mara 205 katika historia yao, ambapo Tottenham wameshinda mechi 58. Man United wao wamefanikiwa kushinda mechi 96. Mechi 51 kati ya hizo zilimalizika kwa matokeo ya sare.

SOMA HII PIA: Manchester United vs Tottenham: Premier League’s Epic Showdown

Mechi 5 zilizopita za Tottenham

Tottenham vs Manchester United
Spurs

4 Nov Tottenham 4-0 FC København

1 Nov Tottenham 0-1 Chelsea

29 Oct Newcastle United 2-0 Tottenham

26 Oct Everton 0-3 Tottenham

22 Oct Monaco 0-0 Tottenham

Mechi 5 zilizopita za Man United

1 Nov Nottingham Forest 2-2 Manchester United

25 Oct Manchester United 4-2 Brighton

19 Oct Liverpool 1-2 Manchester United

4 Oct Manchester United 2-0 Sunderland

27 Sep Brentford 3-1 Manchester United

Kikosi cha Spurs kinachotarajiwa kuvaana na Man United

Tottenham (4-2-3-1)

Kipa: Vicario

Walinzi: Spence, van de Ven, Romero, Porro

Viungo: Palhinha, Bentancur, Odobert, Simons, Kudus

Washambuliaji: Kolo Muani

Kikosi cha Man United kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Tottenham

Kikosi cha UNITED
Kikosi cha UNITED

Man Utd (3-4-2-1)

Kipa: Lammens

Walinzi: Shaw, Maguire, de Ligt, Dalot.

Viungo: Casemiro, Fernandes, Diallo

Washambuliaji: Cunha, Mbeumo Sesko

SOMA HII ZAIDI: Tottenham 1-0 Manchester United mabingwa wa Europa League wapatikana, ukame wa miaka 17 wafutwa

Habari za timu Tottenham vs Manchester United

Kikosi cha Thomas Frank kimerudi kwenye mstari wa ushindi, baada ya kuwakanda Copenhagen mabao 4-0 kwenye Ligi ya Mabingwa. Hii ni baada ya vipigo viwili dhidi ya Newcastle, kwenye Kombe la Carabao na Chelsea wiki iliyopita. Ikumbukwe kipigo cha Newcastle kiliwafanya Spurs watolewe kwenye Kombe la Ligi, katika Uwanja wa St James’ Park.

Tottenham wamekuwa na msimu wa matokeo yasiyoridhisha tangu Frank achukue mikoba, japo raia huyo wa Denmark amewaongoza hadi nafasi ya sita kwenye msimamo. Kwa upande wa Manchester United, wako nafasi ya nane. Hii ni baada ya kuvuna pointi moja dhidi ya Nottingham Forest.

Sare hiyo iliwaondoa United kwenye mwenendo wa ushindi wa mechi tatu mfululizo. Ikumbukwe Man United waliwafunga Brighton, Liverpool na Sunderland. Kikosi cha Ruben Amorim kinaonekana kupiga hatua.

Taarifa za majeruhi

Kwa upande wa Tottenham walipata pigo kabla ya mchezo wa Copenhagen katikati ya wiki, baada ya Mohammed Kudus kushindwa kucheza kutokana na jeraha dogo. Kudus pia yupo hatarini kuwakosa United. Djed Spence amerudi uwanjani na alicheza kama mchezaji wa akiba dhidi ya Copenhagen, akichukua nafasi ya Destiny Udogie upande wa kushoto.

Lucas Bergvall atakosa mchezo huu kutokana na mtikisiko wa ubongo, anaendelea kuwa chini ya ulinzi wa timu ya matabibu. kizingatia taratibu za kitabibu. Wachezaji kadhaa kama Dominic Solanke, Kota Takai, Radu Dragusin, Archie Gray, Yves Bissouma, na Ben Davies bado wako nje, lakini wanatarajiwa kurudi baada ya mapumziko ya kimataifa.

Kwa upande wa Manchester United, Lisandro Martinez yuko karibu kumaliza muda wake wa kupona baada ya jeraha la ACL. Amorim alithibitisha kuwa Muargentina huyo alitaka kucheza dhidi ya Forest, lakini benchi la ufundi lilimzuia kwa tahadhari.

Huenda akarudi kwenye mchezo huu, ingawa kurejea kwake kamili kunatarajiwa baada ya mapumziko ya kimataifa.

Utabiri wa Tottenham vs Manchester United

Amad akishangilia bao
Amad akishangilia bao

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili. Hii ni kutokana na mwenendo wao wa kusuasua. Spurs wameonyesha dalili za ubora katika vipindi fulani, huku United wakianza kuonekana wenye muundo bora kadri mfumo wa Amorim unavyozidi kukomaa. Safu ya mbele ya United yenye Matheus Cunha, Bryan Mbeumo na Benjamin Sesko inaanza kuelewana vizuri, huku Bruno Fernandes akizoea zaidi nafasi yake mpya katikati.

Hata hivyo, Spurs nao wamekuwa na safu bora ya kiungo chini ya, Rodrigo Bentancur na Joao Palhinha na huenda wanaweza kuwapa wenyeji faida ya nyumbani. Hivyo bado Spurs anapewa nafasi kubwa kupata matokeo nyumbani.

SOMA HII PIA: Manchester United vs Tottenham: Preview, Team News & Prediction

Hitimisho

Kutokana na namna EPL ilivyopamba moto, mechi ya Tottenham vs Manchester United inatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa. Uwanja wa Tottenham Hotspurs haujawahi kuwa eneo rahisi kwa wageni. Ubora wa United katika majuma ya karibuni unazidi kutoa taswira ya ushindani mkubwa kusubiriwa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.