- CAF Champions Leagues Yanga SC imepangwa kundi B ikiwa na wababe Al Ahly ya Misri.
- Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League ni bandika bandua kutokana na mechi ngumu zinazowakabili.
- Ali Kamwe athibitisha mechi zote tatu kimataifa Uwanja wa New Amaan Complex utakuwa maalumu kwa mechi za nyumbani
Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto wa kuotea mbali kutokana na mechi ambazo zinawakabili. Timu hiyo inapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa CAF Champions League ikiwa imetinga hatua ya makundi. Yanga SC vs AS FAR huu unatarajiwa kuwa mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
SOMA HII: Matokeo ya Yanga SC 2025/26, ratiba, wafungaji magoli
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza link hii:-SportPesa TZ, Michezo ya Ubashiri Tanzania, Tovuti bora ya ubashiri
Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League
Ipo wazi kuwa ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League ni bandika bandua kutokana na mechi zinazotarajiwa kuchezwa. Mbali na NBC Premier League, Yanga SC imetinga hatua ya makundi CAF Champions League ikiwa ipo kundi B. Kuna mechi 3 za ugenini na 3 za nyumbani kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.
Hizi hapa mechi zinazofuata kwa Yanga SC
Yanga SC vs KMC FC, Novemba 9 2025, Uwanja wa KMC Complex.
Namungo FC vs Yanga SC, Desemba 4,2025, Uwanja wa Majaliwa.
Coastal Union vs Yanga SC, Desemba 10 2025, Uwanja wa Mkwakwani.
Yanga SC vs Simba SC, Desemba 13 2025, Uwanja wa Mkapa.
Azam FC vs Yanga SC, Januari 29,2026, Uwanja wa Azam Complex.
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex, Februari 18 2026.
CAF Champions League hatua ya makundi
Yanga SC vs AS FAR inatarajiwa kuchezwa Novemba 21,2025
JS Kabylie vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Novemba 28,2025
Al Ahly vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Januari 23,2026
Yanga SC vs Al Ahly inatarajiwa kuchezwa Januari 30,2026.
AS FAR vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa 6, Februari 2026.
Yanga SC vs JS Kabylie inatarajiwa kuchezwa Februari 13,2026.
Matokeo ya Yanga SC
Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki). Mfungaji alikuwa ni Celestin Ecua dakika ya pili. Mchezo ulichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii). Goli la ushindi lilifungwa na Pacome Zouzoua. Mchezo ulichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika). Magoli yalifungwa na Aziz Andambwile, Edmund John na Prince Dube.
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC). Magoli yalifungwa na Kouma, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya.
Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika). Wafungaji walikuwa ni Aziz Andambwile na Pacome.
Septemba 30,2025-Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC 2-0 Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025. Magoli yalifungwa na Pacome na Dickson Job.
Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Oktoba 28 2025, Uwanja wa KMC, Complex. Magoli yalifungwa na Mohamed Hussen, Ecua.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kariakoo Dabi ni mchezo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa. Wababe hao watacheza na Simba SC ambao ni watani wao wa jadi.
Hitimisho
Ratiba ya Yanga SC 2025/26 haijapoa hata kidogo kwa kuwa wachezaji watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi uwanjani. Pedro Goncalves ni mrtihi wa mikoba ya Romain Folz mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar. Je kwenye mechi zijazo matokeo ya Yanga SC na ratiba itakuaje? Hapa tutakupa taarifa zote.

