- Al Ahly kutoka Misri ambayo ni ligi namba moja kwa ubora Afrika wamepangwa kundi moja na Yanga SC kutoka Tanzania.
- Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 yamepangwa baada ya droo kufanyika Novemba 3 2025 Johannesburg, Afrika Kusini.
- Simba SC kwenye CAF Champions Leagues mikononi mwa waarabu, ratiba yake inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21,2025.
Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 imefanyika nchini Afrika Kusini. Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) liliendesha droo hiyo katika studio za SuperSport. Ni Nassar Khaled Mkuu wa Idara ya mashindano akishirikiana na gwiji Alex Song wa Cameroon na Christopher Katongo wa Zambia.
SOMA HII: Droo ya Caf Champions League 2025/26
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF Yanga SC na Simba SC zipo wapi?
Makundi manne yenye timu bora yamepatikana. Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF tayari imefanyika na inatarajiwa kuwa na mechi tatu kali ugenini na nyumbani. Simba SC na Yanga SC zipo mikononi mwa waarabu.

Mashindano yataanza kutimua vumbi lini?
Mashindano haya makubwa ya CAF Champions League yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21,2025. Februari 2025 yanatarajiwa kufika tamati. Katika mechi hizo za nyumbani na ugenini katika kila kundi zinatafutwa timu mbili ambazo zitasonga hatua ya robo fainali. Tayari baada ya droo kuchezwa kila timu imetambua mshindani wake atakuwa nani.
Haya hapa makundi ambayo yamepangwa namna hii:-

Kundi A
RS Berkane kutoka Mali
Pyramids FC kutoka Misri
Rivers United kutoka Nigeria
Power Dynamos kutoka Zambia
Kundi B
Al Ahly ya Misri
Yanga SC ya Tanzania
AS FAR kutoka Mali
JS Kabylie ya Algeria
Kundi C
Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini
Al Hilal kutoka Sudan
MC Alger kutoka Algeria
St Eloi Lupopo ya Congo
Kundi D
ES Tunis ya Tunisia
Simba SC kutoka Tanzania
Petro Luanda ya Angola
Stade Malien ya Mali
SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champion League 2025

Yanga SC ilifikaje hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika?
Yanga SC kutoka Tanzania ilianzia katika hatua ya awali. Ni mechi nne ilicheza, mbili ugenini na mbili ikiwa nyumbani. Hatua ya kwanza ilianza dhidi ya Wiliette SC vijana wa Angola. Hapailipita kwa jumla ya magoli 5-0. Katika mchezo wa kwanza ugenini ilishinda kwa 3-0 na ule wa pili ikashinda 2-0.
Hatua inayofuata kwa Yanga SC iliyokuwa inanolewa na kocha Romain Folz ilikuwa dhidi ya Silver Striker ya Malawi. Ugenini ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0 ikawa ni mwisho wa Folz kukaa benchi. Kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Mkapa ilipata ushindi wa magoli 2-0 na ikasonga mbele hatua ya makundi.
Simba SC ilifikaje hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika?

Mnyama alianza kuunguruma ugenini dhidi ya Gaborone United alipopata ushindi wa goli 1-0. Katika mchezo wa Uwanja wa Mkapa ilikuwa 1-1. Ushindi wa jumla ya magoli 2-1 ukampeleka hatua inayofuata.
Katika hatua ya mtoano ya pili ilikuwa dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatin. Mchezo wa ugenini Simba SC ilipata ushindi wa goli 3-0 ule wa nyumbani Uwanja wa Mkapa ilikuwa 0-0. Ilitinga hatua ya makundi kwa jumla ya magoli ya ugenini.
SOMA HII: Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champion League 2025

Hitimisho
Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF ni mwanzo wa kutafuta timu zitakazokwenda hatua ya robo fainali. Baada ya kutoka hatua ya awali hii ni hatua nyingine yenye ushindani mkubwa. Simba SC na Yanga SC zinakibarua kigumu kutafuta nafasi kupenya robo fainali.
Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17


