- Wananchi wanajiandaa na mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika ya Yanga SC vs Silver Strikers.
- Huku mchezo huo ukisubiriwa, uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kukamilisha mchakato wa kumpata kocha mpya.
- Ali Kamwe afunguka mazito, aitaja CV ya kocha Patrick Mabedi.
Wananchi wanajiandaa na mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika ya Yanga SC vs Silver Strikers. Huku mchezo huu ukitarajiwa kupigwa keshokutwa Jumamosi, uongozi wa Yanga SC umeibuka na kuweka wazi mchakato wa kumtangaza kocha wao mkuu mpya. Hii ni baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu Roman Folz.
SOMA HII PIA: Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League 2025 | Highlights, goal
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Umecheza na hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kocha mpya Yanga ni yupi?

Dili limetiki ndivyo unavyoweza kusema, hii ni baada ya taarifa kutoka ndani ya Yanga SC kueleza kuwa kwa asilimia 90 tayari mchakato kumtangaza kocha mpya umekamilika. Makocha kadhaa wanataja kufanya mazungumzo na Yanga. Baadhi ya makocha hao ni pamoja na João Paulo Mota Maria, Romuald Rakotondrabe na Sead Ramovic.
Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa, kocha Romuald Rakotondrabe ndiye anapiwa nafasi kubwa kuiongoza Yanga SC. Kocha huyo anapigiwa chapuo ya kuinoa Yanga SC, baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na timu ya Taifa ya Madagascar. Hii ni baada ya kuifikisha timu hiyo hatua ya fainali ya michuano ya Chan, mwaka huu.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni bure Oktoba 25 2025| Taarifa kuhusu Mzize, H2H
Mjue kwa ufupi, Kocha mpya Yanga SC, Romuald Rakotondrabe

Kocha Rakotondrabe ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Madagascar. Kwa sasa ana umri wa miaka 60, na tangu aanze kuifundisha Madagascar amekuwa na mafanikio makubwa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni, kuipeleka Madagascar fainali kwenye michuano ya CHAN mapema mwaka huu.
Mpaka sasa inaelezwa kuwa kwa 90% Yanga na kocha Rakotondrabe wamekubaliana kila kitu, kilichobaki ni kocha huyo kusaini mkataba na kutangazwa. Hii ni kwa mujibu wa gwiji wa Habari za usajiri Tanzania, Hans Raphael. Hivyo inatarajiwa muda wowote kutoka sasa kocha huyo atatua Bongo kusaini mkataba wa miaka miwili.
Alichosema Ali Kamwe ishu ya kocha mpya, Je atakuwepo Jumamosi mechi ya Yanga SC vs Silver Strikers
“Wengi mmekuwa mkiniuliza kuhusu Kocha mpya, niwaeleze tu, kuwa Uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato mzuri wa kumpata kocha mpya. Ndani ya siku tatu hizi mchakato huu utakuwa umekamilika, kwa mantiki hiyo Mchezo wetu wa tarehe 25 tutaongozwa na ‘Care taker’ wetu, Patrick Mabedi, na hatuna shaka kabisa na yeye kwani tunaamini kwenye uwezo wake na CV yake”
Kuhusu kocha Roman Folz kufukuzwa Yanga SC

Romain Folz alipewa nafasi ya kuwa kocha wa Yanga mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, akichukua nafasi ya Miloud Hamdi. Kocha huyo alipewa malengo ya kudumisha utawala wa ndani, pamoja na kuifikisha mbali Yanga SC katika michuano ya Afrika. Ilikuwa mapema kupima malengo haya, lakini, kulikuwa na dalili zinazoonyesha kutoridhika kwa baadhi ya mashabiki na uongozi juu ya mwenendo wa timu yao.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025| Lineup, H2H
Sababu nyingine zilizomng’oa folz Yanga SC?
Ukiachana na kiwango cha timu kuelezwa kushuka na matokeo ya sare mchezo dhidi ya Mbeya City, inaelezwa kuna sababu kadhaa zilizopelekea kumtimua Folz. Hii ni pamoja na matatizo ya mambo ya ndani. Hii ikimaanisha kufanya marekebisho katika benchi la ufundi, wasaidizi na wataalamu wengine.
Matokeo ya Yanga SC chini ya kocha Romain Folz

Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii)
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Silver Strikers 1-0 Yanga SC (CAFCL)

Hitimisho
Wakati Yanga SC vs Silver Strikers ukiwa mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa. Uongozi wa Yanga SC unaonekana kupania kufanya maboresho makubwa ya benchi la ufundi. Ikumbukwe katika kipindi hiki cha mpito kikosi kitaongozwa na kocha msaidizi, Patric Mabedi Hivyo ujio wa kocha mpya Yanga SC, unatarajia kuamsha tena ari ya ushindani ambayo itasaidia kutimiza malengo yao.

