FolzFolz
  • Silver Strikers 1-0 Yanga SC mchezo wa mwisho kwa kocha mwenye CV kubwa Jangwani kukaa kwenye benchi la ufundi.
  • Romain Folz amefukuzwa Yanga SC mrithi wake akitajwa kuwa ni Kocha Mkuu wa Madagascar mwenye miaka 60.
  • Mbeya City 0-0 Yanga SC uliwasha taa nyekundu, Patrick Mabedi kuwafundisha kwa sasa mchakato ukiendelea kusaka kocha mpya.

Romain Folz amefukuzwa Yanga SC mara baada ya mchezo wa CAF Champions League kumalizika. Folz aliongoza mchezo uliosha kwa Yanga SC kufungwa goli 1-0 dhidi ya Silver Strikers ambaoni hatua ya pili. Taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa timu hiyo imebainisha kuwa imevunja mkataba na kocha huyo.

SOMA HII: Deal done! Roman Folz ‘out’, kocha mpya Yanga SC huyu hapa

Marubani huwa wanakuwa na mamilioni wikiendi

Wikiendi kwa marubani huwa inakuwa bomba kutokana na mamilioni mfukoni. Paisha ndege sasa uvune mkwanja wako. Hakuna kwenda kinyonge, mgao upo wakutosha ukicheza Aviator. Bofya hapa chini.

image

Romain Folz amefukuzwa Yanga SC matokeo yake ya mwisho yalikuaje?

Romain Folz amefukuzwa Yanga SC
Romain Folz aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Ni mechi saba ameongoza kocha huyo rai awa Ufaransa mwenye CV kubwa. Romain Folz amefukuzwa Yanga SC akipata ushindi katika mechi 5, sare 1 na kupoteza mchezo 1. Kwenye mechi za hatua ya awali CAF Champions League alishinda nje ndani.

Alikiongoza kikosi cha Wananchi kupata ushindi wa jumla ya magoli 5-0 dhidi ya Wiliete ya Angola. Mchezo wa ugenini ilikuwa ushindi wa goli 3-0 ule uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa goli 2-0. Mchezo wake wa mwisho ni ugenini akiambulia kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Silver Strikers. Katika mechi hizo ni goli moja amefungwa.

Taarifa kutoka Yanga SC hii hapa

Taarifa Folz
Taarifa kutoka Yanga SC kuvunja mkataba wa Folz.

“Uongozi wa Young African Sports Club unapenda kuutarifu Umma kuwa, umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.

“Uongozi wa Young African Sports Club unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.

“Katika kipindi hiki kikosi chetu kitakuwa chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta kocha mkuu ukiendelea,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA HII: Roman Folz kufukuzwa Yanga SC, kocha mpya huyu hapa

image

Matokeo ya mechi za Romain Folz Yanga SC

Romain Folz (-)
Romain Folz aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki).

Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).

Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika

Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).

Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).

Oktoba 18, 2025, Silver Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

Mechi zijazo kwa Yanga SC bila Folz

Yanga Tena
Mchezo ujao kwa Yanga SC ni dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga SC.

Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.

Yanga SC vs Mtibwa Sugar, Oktoba 29 2025, Uwanja wa KMC, Complex.

Yanga SC vs KMC FC, Novemba 4 2025, Uwanja wa KMC Complex.

Coastal Union vs Yanga SC, Desemba 10 2025, Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga SC vs Simba SC, Desemba 13 2025, Uwanja wa Mkapa

Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex, Februari 18 2026

SOMA HII: Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Ratiba ya mechi zijazo

image

Hitimisho

Romain Folz amefukuzwa Yanga SC huku jina la Romuald Rakotondrabe mwenye miaka 60 likitajwa. Huyu anaifundisha timu ya taifa ya Madagascar. Aliipeleka timu ya taifa ya Madagascar fainali ya CHAN 2024. Je atakuwa mrithi wa Folz Jangwani? Tutakupa taarifa zote kwenye SportPesa site.

Share this: