Seleman Mwalimu (-)Seleman Mwalimu (-)
  • Simba SC vs Azam FC utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Meneja Mkuu, Dimitar Patev kukaribishwa katika Ligi ya NBC
  • Matokeo ya Simba SC 2025/26, ratiba na wafugaji wote tumekuletea karibu.
  • Sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Gaborone ilikuwa ni rekodi ya kwanza kwenye CAF Champions League msimu mpya.

Matokeo ya Simba SC kwa mechi zilizopita 2025/26 za ushindani tumekusogezea hapa. Kikosi hicho kinafundisha na Kocha Mkuu, Dimitar Pantev mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ambaye ameajiriwa Raja Casablanca. Mechi iliyopita mnyama alipata ushindi wa magoli 3-0 Namungo FC, NBC Premier League.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Matokeo ya Simba SC mechi zilizopita

Matokeo ya Simba SC
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Simba SC kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC. Source: Simba SC.

Hapa tunakuletea matokeo ya Simba SC mechi zilizopita za ushindani iliposhuka uwanjani. Rekodi zinaoyesha kuwa katika mechi 6, ilipoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga SC. Ilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1 dhidi ya Gaborone United. Ushindi ilikuwa kwenye mechi nne.

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.

Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

SOMA HII: Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC itakayochezwa Septemba 16 | H2H, vikosi, matokeo, wafungaji

image

Ratiba ya mechi zijazo kwa Simba SC

kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia
Dimitar Pantev, Meneja Mkuu wa Simba SC mrithi mikoba ya Fadlu Davids 2025/26. Source: Simba SC.

Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.

Simba SC vs Azam FC, Novemba 2 2025, NBC Premier League.

JKT Tanzania vs Simba SC, Novemba 5 2025, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, NBC Premier League.

Yanga SC vs Simba SC, Desemba 13, 2025, Uwanja wa Mkapa, NBC Premier League.

Simba SC vs Mashujaa FC, Februari 19, 2026, Uwanja wa KMC, Complex Dar.

Vinara wa ufungaji wa magoli

Ligi Kuu Bara

Rushine De Reuk magoli 2 alifunga mchezo wa Fountain Gate na mchezo dhidi ya Namungo FC.

Jean Ahoua goli 1

Chamou Karabou goli 1

Seleman Mwalimu goli 1

Jonathan Sowah goli 1

Wafungaji CAF Champions League

Ellie Mpanzu goli 1

Jean Ahoua goli 1

SOMA HII: Mechi ya kirafiki: Simba SC 2-0 Kahraba Ismailia| Jonathan Sowah na Bajaber wafunga magoli

image

Mabao ya kufungwa

Rushine Kambini
Beki wa kikosi cha Simba SC 2025/26 Rushine. Source: Simba SC.

Katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC baada ya mechi mbili Simba SC haijafungwa. Imekusanya jumla ya pointi sita kwa ushindi kwenye mech izote mbili. Inaongoza ligi 2025/26.

Idadi ya magoli ambayo imefunga ni 6. Kipa namba moja ni Moussa Camara ambaye alipata maumivu mchezo dhidi ya Gaborone United. Kipa namba mbili ni Yakoub Suleman.

Katika anga la kimataifa, Simba SC baada ya kucheza mechi mbili imeruhusu goli moja. Ni dhidi ya Gaborone United. Mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Hitimisho

Matokeo ya Simba SC iliyoanzishwa 1936 yamekuwa yakibadilika kila mchezo unaofuata kulingana na aina ya mechi. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika haijapoteza sawa na Ligi ya NBC kwenye mechi za mwanzo. Je wataendelea na mwendo huo katika mechi zijazo? Tutaendelea kukujuza taarifa za matokeo kwenye site ya SportPesa.

Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17

image
Share this: