Atletico vs InterAtletico vs Inter
  • Carlso Martin wa Atletico Madrid nyota wa kwanza kufunga goli kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Inter Milan kwenye ardhi ya Afrika.
  • Atletico Madrid 1-1 Inter Milan matokeo yenye hadhi ya dakika 90 za kazi na mshindi akipatikana kwa mikwaju ya penati 4-2.
  • Juan Musso kipa wa Atletico Madrid alikuwa ni shujaa kwa kuokoa penati mbili kwenye mchezo huo mkubwa.

Atletico Madrid 1-1 Inter Milan ni matokeo ya dakika 90 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa nchini Libya. Atletico Madrid ilipata ushindi wa penati 4-2 Inter Milan. Goli la ufunguzi lilifungwa dakika ya 34 kupitia kwa Carlos Martin, Inter Milan walisawazisha dakika ya 58 kupitia kwa Yann Bisseck kwenye mchezo huo.

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

SOMA HII: Atletico Madrid vs Inter Milan: Madrid out to topple in-form Italians in 23/24 UCL battle for glory

Atletico Madrid 1-1 Inter Milan, walihudhuria mashabiki wangapi?

Atletico Madrid 1-1 Inter Milan
Musso kipa aliyeokoa penati mbili dhidi ya Inter Milan. Source: Atletico Madrid.

Wakati ubao wa Uwanja wa taifa Benghazi ukisoma Atletico Madrid 1-1 Inter Milan ni mashabiki 42,000. Mwamuzi Mustafa Al Darsi hakuongeza dakika zilipokamilika 90 ambapo kila timu ilikuwa imefunga goli 1-1 kwenye muda wa kawaida. Maamuzi yake ilikuwa moja kwa moja mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati.

Wajue wapigaji penati wa Atletico Madrid

Antoine Griezmann

 Koke (alikosa)

 Matteo Ruggeri

 Omar Janneh

Clement Lenglet  

Hawa hapa wapigaji penati wa Inter Milan

Matteo Venturini

 Matteo Lavelli

 Luis Henrique mlinda mlango Musso aliokoa

Francesco Acerbi mlinda mlango Musso aliokoa

Magoli yalivyofungwa kwenye mchezo

Carlos
Carlos Martin mfungaji wa goli la kwanza dhidi ya Inter Milan. Sourec: Atletico Madrid.

Katika dakika 15 za mwanzo timu zote zilikuwa zinacheza kwa uangalifu mkubwa. Dakika ya 14 Atletico Madrid walipoteza nafasi yakufunga wakiwa ndani ya 18 kupitia kwa Thiago Almada ambaye alikuwa na kipa. Dakikay a 34 ni Carlos Martin alifunga goli la kuongoza.

Carlos alipokea mpira na kuegukia lilipo lango akiwa katika hali ya kujiamini akapiga shuti. Hilo lilikuwa ni goli la ufunguzi katika kipindi cha kwanza. Lilidumu mpaka dakika ya 58 ya mchezo.

Inter Milan waliweka usawa kupitia Yann Bisseck dakika ya 58.Huo ulikuwa ni mpira wa pigo la kona ilipigwa na Henrikh Mkhitaryan. Pigo hilo lilimpa nafasi Bisseck kwenda hewani na kuushinda mpira akifunga goli la kuweka usawa.

H2H Atletico Madrid vs Inter Milan

Wababe hawa kwenye mechi tatu walizokutana Atletico Madrid wanaongoza kwa kushinda wakifanya hivyo mara tatu. Inter Milan wamepata ushindi mara moja. Bado Inter Milan hawajawatesa mara nyigi wapinzani wao.

Machi 13 2024, Atletico Madrid 2-1 Inter, UEFA Champions League. Mshindi alipatikana kwa penati ilikuwa Atletico Madrid 3-2 Inter Milan.

Februari 20 2024: Inter Milan 1-0 Atletico Madrid. UEFA Champions League.

Agosti 27 20210: Inter Milan 0-2 Atletico, (UEFA Super Cup)

Oktoba 10 2025:  Atletico Madrid 1-1 Inter Milan, mshindi alipatikana kwa penati, Atletico Madrid 4-2 Inter Milan.

Mechi nne zilizopita kwa Atletico Madrid

Griezman na Carlos
Nyota wa timu ya Atletico Madrid. Source: Atletico Madrid.

Celta Vigo 1-1 Atletico Madrid (LaLiga)
Atletico Madrid 5-1 Frankfurt (UEFA Champions League)
 Atletico Madrid 5-2 Real Madrid (LaLiga)
Atletico Madrid 3-2 Rayo Vallecano (LaLiga)
SOMA HII: Inter Milan Vs FC Barcelona ‘live’: Vikosi, uchambuzi, utabiri

image

Mechi nne zilizopita za Inter Milan

Inter Milan 4-1 Cremonese (Serie A)
 Inter Milan 3-0 Slavia Prague (UEFA Champions League)
 Cagliari 0-2 Inter Milan (Serie A)
Inter Milan 2-1 Sassuolo (Serie A)

Kikosi cha Inter Milan dhidi ya Atletico Madrid

J. Martinez

Bisseck

Acerbi

Palacios

Darmian

Diof

Bovo

Mkhitaryan

Luis

Henrique

Bony

Spinacce

Wachezaji wa akiba

 Raffaele Di Gennaro (mlinda mlango)
 Francesco Stante (beki wa kati)
 Tommaso Avitabile (beki)
 Simone Cinquegrano (beki)
 Dilan Zárate (kiungo)
 Iwo Kaczmarski (kiungo)
 Matteo Venturini (kiungo)
 Mattia Marello (winga)
 Richi Agbonifo (winga)
 Matteo Lavelli (mshambuliaji)

Kikosi cha Inter Milan vs Atletico Madrid

J Musso
J Musso kipa namba moja wa Atletico Madrid. Source:Atletico Madrid.

Musso

Pubill

Gimenez

Lenglet

Ruggeri

Galan

Gallager

Koke

Almada

Griezmann

Martin

SOMA HII: Atletico Madrid vs Inter Milan: Madrid out to topple in-form Italians in 23/24 UCL battle for glory

image

Atletico wachezaji wa akiba

Mario de Luis (mlinda mlango)
 Ilias Kostis (beki wa kati)
 Aleksa Puric (beki wa kati)
Carlos Giménez (beki wa kulia)
 Javi Serrano (kiungo)
Jorge Castillo (kiungo)
 Dario Frey (kiungo)
 Juan Alegre (kiungo)
Jorge Rajado (winga)
 Jesus Barrios (winga)
 Omar Janneh (mshambuliaji)

Hitimisho

Atletico Madrid 1-1 Inter Milan ulikuwa ni mchezo wa kukata na shoka kwa wababe hawa wawili. Atletico wamepata ushindi katika ardhi ya Afrika kwa mara ya kwanza. Ni Diego Simeone Kocha Mkuu wa Atletico alikiongoza kikosi cha Atletico.

image
Share this: