- Mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids 2025/26 alikuwa anaifundisha Gaborone United ya Botswana.
- Kocha mpya Simba SC CV yake inalitambua soka la Afrika ikitajwa kuwa sababu yakupata ajira.
- Ratiba inaonyesha kuwa Oktoba ana mechi mbili za CAF Champion League, Azam FC kuwakabili Novemba.
Kocha mpya Simba SC CV yake inaonyesha kuwa analitambua soka la Afrika. Hiyo inatajwa kuwa sababu ya kupewa majukumu kuifundisha timu hiyo. Anaitwa Dimitar Pantev mwenye umri wa miaka 49 atakuwa akiwafundisha vijana wa msimbazi. Alitambulishwa rasmi Oktoba 3 2025 kuwa mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids aliyeajiriwa Raja Casablanca.
SOMA HII: Unamfahamu, Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC? Hizi hapa rekodi zake, mifumo na mafanikio

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.
Kocha mpya Simba SC CV yake hii hapa

Amezaliwa Juni 26 1976 ana umri wa miaka 49. Ni rai awa Bulgaria ana leseni ya UEFA Pro ambayo ni ngazi ya juu ya ukocha barani Ulaya. Alianza kazi ya ukocha katika kikosi cha Varna City ambayo ni timu ya vijana.
Alipata nafasi ya kufundisha Klabu ya Flamengo, Victoria United, Johansen, Orapa na Gaborone United. Katika soka la Afrika amekuwa na uzoefu nalo. Ni timu tano ambazo alipata kuzifundisha. Miongoni mwa hizo ni Victoria United ya Cameroon, FC Johansen ya Sierra Leone, Orapa United na Gaborone United hizi za Botswana.
Kwa miaka ambayo amefundisha Afrika amekuwa na mafanikio ya kutwaa mataji. Ni mataji mawili ya ligi akiwa Cameroon na Botswana. Kwa sasa atakuwa ndani ya ligi ya Ligi Kuu ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
SOMA HII: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

Ratiba ya mechi za Pantev akiwa Simba SC
Oktoba kuna mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya pili dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya nchini Eswatini. Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 17-18 ugenini na ule wa pili Oktoba 24-25, Dar, Uwanja wa Mkapa. Kwenye ligi mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa dhidi ya Azam FC, Novemba 2 2025, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mechi za CAF Champion League Simba SC inasaka hatua ya makundi. Timu hiyo ilitinga hatua ya pili kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1 dhidi ya Gaborone United. Timu ambayo ilifungashiwa virago na Simba SC ilikuwa inafundishwa na Pantev ambaye sasa atakuwa unyamani.
Ikumbukwe kwamba goli la Simba SC ugenini lilifungwa na Ellie Mpanzu akitumia pasi ya Shomari Kapombe. Mshambuliaji ambaye alikuwa ndani ya 18 kwenye mchezo huo alikuwa ni Seleman Mwalimu. Katika mchezo wa Uwanja wa Mkapa ni kiungo Jean Ahoua alifunga goli.
Semaji Ahmed Ally kuhusu sababu za kumpa kazi Pantev

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi sababu za kumpa kazi Pantev. Ally alibainisha kuwa haikuwa rahisi kumpata. Hiyo yote inatokana na uzoefu alionao na aina ya soka analofundisha.
“Kumpata Pantev ilikuwa ni vita kidogo kwa kuwa kuna timu nyingine kutoka Tanzania zilikuwa zinamuhitaji. Uzoefu wake wa kufundisha soka la Afrika ni sababu ambayo inamfanya awe hapa. Unajua kufundisha Afrika na kutwaa mataji katika nchi mbili tofauti sio jambo jepesi.
“Kwa muda mfupi aliokuwa katika timu hizo zilipata mafanikio. Tulimuona akiwa na Gaborone United. Wachezaji walikuwa na uwezo wakawaida lakini walitusumbua. Tukafuatilia tukajua kwamba huyu Pantev yupo nyuma yao tukamchukua,”.
SOMA HII: Jonathan Sowah atoa ahadi nzito Simba SC / Magoli aliyofunga / Kambi Misri kinachoendelea
Hitimisho
Kocha mpya Simba SC CV inambeba kutokana na mafanikio aliyopata. Licha ya kwamba alitwaa mataji katika nchi mbalimbali bado kuna mtihani kwenye ligi namba nne Afrika. Mbali na ligi atakuwa na kazi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

