- Simba SC yapoteza mechi sita mfululizo mbele ya watani wao wa jadi Yanga SC kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja.
- Majibizano yatawala kwa wachambuzi goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside?
- Yanga SC waonesha utemi wao kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkapa Septemba 16 2025.
Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? Ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Septemba 16 2025. Yanga SC ilipata ushindi wa 1-0 Simba SC wakipoteza Ngao ya Jamii kwenye fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa. Wachambuzi wamezungumza kila mmoja kwa mtazamo wake.
Muda wa kukunja mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa
Kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi rubani wa Kindege cha SportPesa. Rahisa sana kupata kilicho chako kwa uhakika. Cheza Aviator muda huu upate mgao wako.

Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? Hawa hapa wachambuzi

Soma hii: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highligts, h2h magoli yote, Doumbia, Diarra waiteka shoo kwa mkapa
Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? Mjadala huo umeibua majibu tofautitofauti ambapo wapo wanaosema ilikuwa ni offside na wengine wakibainisha ilikuwa onside. Ikumbukwe kwamba mwamuzi wa kati wa mchezo alikuwa ni Ahmed Arajiga.
Goli pa Pacome lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 53. Wakati Pacome anafunga goli hilo awali alionekana kuwa kwenye mtego wa kuotea lakini hakuwa na umiliki wa mpira. Ni Maxi Nzengeli ambaye alikuwa kwenye umiliki wa mpira Uwanja wa Mkapa.
Hans Rafael kuhusu goli la Pacome

Wachambuzi kupitia mitandao ya kijamii, hasa Instagram wameandika maoni yao. Huyu hapa ni Hans Rafael ameanza namna hii: “Wakati mpira unakwenda kwa Max alikua Onside ila Pacome alikua Offside alichokifanya Pacome ni kutumia akili ya kikubwa kwa kumpisha Max kisha yeye akarudi nyuma kuiua Offside.
Max akapiga shuti mlinda mlango akaucheza kisha mpira ukarudi kwa Pacome ambaye kwa wakati huo alikua Onside kisha mwamba akafunga bao safi kabisa. Bao safi kabisa kipengele uje nacho wewe.
Jemedari vs Edo Kumwembe wajibizana
Mara baada ya mchezo mchambuzi Jemedari Said aliandika namna hii: “Mnyama kafa mara 6 mfululizo, walichofanikiwa leo ni walau kuonyesha wamefungwa lakini Yanga SC hawakuwa so dominant, vinginevyo wana safari ndefu dhidi ya Yanga SC na hawa akina Kante wao. Labda wapate wakina De. Reuick 5 ndo watawafunga Yanga.
“Bado Yanga SC ni imara mbele ya Simba SC hata kama siku hiyo hawakutawala mchezo ila wanauwezo wa kushinda. Maana yake bado Yanga SC watatawala ligi tena na ile ahadi ya ubingwa mara 10 mfululizo isidharaulike.
“Mohamed Mkono, mwamuzi msaidizi namba 1 wa mchezo ambaye ni FIFA referee amewaua Simba SC. Ile ni Offside kabisa, hakupaswa kuruhusu lile bao. Pacome alikuwa offside position akaja kufanya obstruction kwa De.Reuick ambaye alikuwa anamkimbiza Max. Kisha akaukuta mpira akafunga, kufanya obstruction ukitoka kwenye offside position ni kosa na mkono anajua hilo.
Edo Kumwembe amjibu Jemedari live bila chenga
Mara baada ya andiko hilo la Jemedari, Edo Kumwembe alidondosha ujumbe uliosomekana namna hii: “Wakati Pacome anafanya obstruction tayari alishaondoka katika offside position. Labda kama iwe faulo kama faulo nyingine lakini sio kama faulo obstruction position. Unless kama obstruction ilifanyika kabla Max hajamiliki mpira
Edo Kumwembe yeye aliandika namna hii kuhusu goli la Pacome: “Mlioniuliza kama offside mimi sijaona offside hapa. Pacome alikuwa offside awali na hakutaka kuhusika na mpira. Maxi akaupitia na Pacome akarudi nyuma kujitoa katika offside position. Wakati Camara anaupangua hakuwa katika nafasi ile ile. Alikuwa sawa na other watu wa mwisho. Mechi ilikuwa nzuri kwa timu zote,”.
Mtangazaji Pascal Kabombe kuhusu goli la Pacome
Pascal Kabombe mtangazaji kupitia Azam TV alifungukia kuhusu goli la Pacome. Kabombe alibainisha kuwa kuna wakati Pacome alikuwa kwenye mtego wa kuotea na baadaye mpango kazi wa kuotea ulikufa. Mtangazaji huyo ameongeza kwa kubainisha kuwa kulikuwa na faulo ambayo ilichezwa.

Huyu hapa: “Kwa mimi nilivyoona tukio kabla ya Pacome kumzuia yule beki tayari Maxi alikuwa mbele yake. Automatical offside ilikuwa imeshakufa. Kwa sababu ukiwa nyuma ya mpira, mpira ukiwa mbele yako hakuna offside. Wakati Maxi ameondoka na ule mpira kabla ya Maxi kuupiga kuna wakati Pacome alikuwa Offside. Baada ya Maxi kuucheza mpira offside inakufa pale.
“Refarii anaangalia mpira, Pacome anachofanya anamzuia beki hiyo ni obstarction. Wakati anamzuia hakuwa kwenye offside. Automatical Pacome hayupo offside. Sheria mpira ukishakuwa mbele inakuwa sio offside.Nikikaa kwenye usawa wa golikipa hata kama nitasimama bado nitakuwa offside.
“Movement ya Pacome ilikuwa ni kutoka kwenye Ofsside kwenda ndani. Kabla hajafanya kitendo cha kumblock beki tayari Maxi alishavunja ile offside,” alisema Kabombe.
Hitimisho
Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? Mjadala mkali kwa mashabiki wa timu zote mbili. Yanga SC kwao ni kicheko huku Simba SC ikiwa ni huzuni kupishana na taji la Ngao ya Jamii.


