Wadi Degla SC --- Simba SCWadi Degla SC --- Simba SC
  • Matokeo ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao umepigwa huko Misri.
  • Wadi Degla SC 0-2 Simba SC, Makala hii inakupa uchambuzi ulioshiba wa magoli yote, vikosi, highlights, h2h.
  • Mpanzu, Kibu waendeleza balaa lao la kufyumania nyavu

Dakika 90 zimekamilika na ubao umeonyesha Wadi Degla SC 0-2 Simba SC, Ndiyo Wekundu wa Msimbazi wamemchapa Mwarabu. Huu unakuwa ushindi wa tatu kati ya michezo minne ambayo Simba imecheza, tangu kuanza kwa kambi yao ya Misri. Kambi hiyo ni ya kujiandaa na msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26.

Cheza na shinda mamilioni sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

SEO Banner LV

Kuhusu Wadi Degla SC 0-2 Simba SC

Kama ilivyotarajiwa kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davis aliuanza mchezo huo huku kukiwa na mabadiliko kadhaa ya kikosi chake. Kikosi cha Simba SC kilichoanza mchezo wa le oni kama ifuatavyo;

Moussa Camara, Ladack Chasambi, Naby Camara, Rushine De Reuck, Chamou Karaboue, Morrice Abraham, Kibu Denis, Jean Ahoua, Neo Maema, Elie Mpanzu na Steven Mukwala.

Wachezaji wa Akiba:

Hussein Abel, Alexander Erasto, David Kameta, Anthony Mligo, Saleh Karabaka, Alassane Kante, Mohammed Bajaber, Jonathan Sowah, Bashiru Salum, Joshua Mutale, Awesu Ally, Mzamiru Yassin, Valentino Mashaka, Semfuko Charles, Hussein Mbegu

Mpanzu, Kibu mashujaa magoli ya Simba SC

Mpanzu na Kibu
Mpanzu na Kibu

Baada ya kuwa na kipindi cha kwanza cha mashambulizi ya timu zote mbili bila kupata bao, hatimaye dakika ya 73 Elie Mpanzu aliipa Simba goli la uongozi. Mpanzu aliifungia Simba bao akiwa nje ya 18 mbele ya duara la katikati mwa uwanja. Mpanzu alitandika shuti kali lililomshinda kipa wa Wadi aliyebaki anashangaa mpira huo ukitinga moja kwa moja nyavuni.

Baada ya bao hilo, Simba SC waliendelea kulishambulia lango la Wadi Degla, dakika 79 mashambulizi hayo yalizaa bao la pili lililofungwa na Kibu Denis. Kibu alifunga bao hilo akitumia assist ya kiungo Jean Ahoua. Mfungaji alifunga bao hilo akiwa ndani ya 18 na kuunganisha kwa mtindo wa tikitaka.

SOMA HII PIA: Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC: Aungana na Sowah, Mukwala kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Kuhusu kambi ya Simba SC nchini Misri

Ikumbukwe Simba SC iliwasili nchini Misri mwanzoni mwa mwezi Agosti 2025, kwa ajili ya kambi thabiti ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya 2025/26. Hii ni sehemu ya kuiandaa timu kwa ajili ya mashindano ya ndani na ya kimataifa. Maandalizi ya kambi hiyo yalifanyika jijini Dar es Salaam ambapo mastaa wote walikusanywa na kupitishwa vipimo vya afya kabla ya safari kwenda Misri.

Programu hii inaongozwa na kocha Fadlu Davids, ambaye msimu uliopita alikaribia kuipa timu hiyo taji la Kombe la Shirikisho Afrika. Malengo makubwa ya kambi hiyo ikiwa ni, kuwapa nafasi mastaa wapya kuzoeana na wale waliopo. Ikumbukwe kuwa kupitia dirisha kubwa la usajili Simba imefanya mkubwa.

Hawa hapa mastaa wapya Simba SC

Wadi Degla SC 0-2 Simba SC
Camara Simba SC

Baadhi ya mastaa wapya ambao wamesaini Simba SC ni Pamoja na; Jonathan Sowah (mashambuliaji) kutoka Singida Black Stars. Alassane Kanté (kiungo wa kati, ulinzi) kutoka Tunisia. Rushine De Reuck (beki wa kati) aliyewahi kukipiga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Yakoub Suleiman Ali, Wilson Nangu na Morris Abraham.

SOMA HII ZAIDI: Simba Day Septemba 10 2025 | Ali Kiba kutumbuiza | Ubaya Ubwela pasua kichwa

Kambi yahusisha miji miwili Misri

Ili kupata asilimia 100 ya ambacho walikihitaji kupitia kambi hiyo, Simba SC ilianza kwanza kujikita kwenye jiji la Ismaillia. Baada ya mazoezi ya wiki mbili kikosi hiko kilihamisha kambi mpaka jijini Cairo. Kempu hiyo imepangwa kuendelea kwa takriban mwezi mzima hadi Agosti 28, mwaka huu.

Mechi za Kirafiki za kujipima

Mpanzu vs Wadi Degla
Mpanzu vs Wadi Degla

Ili kupima maendeleo ya kambi hiyo Simba imepanga kucheza kucheza mechi 4, au 5 za kirafiki dhidi ya klabu za Ligi Kuu ya Misri. Kupitia mechi hizi, kocha Davids anapima mwelekeo wa kikosi chote na pia uwezo wa watu walioko zamani na wapya. Hii inafanyika ili kutengeneza muunganiko ‘Chemistry’ ya timu.

SOMA HII PIA: Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC: Mashine nyingine 6 kutangazwa tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Hitimisho

Kambi hii na mechi za majaribio ikiwemo Wadi Degla SC 0-2 Simba SC zinatoa eneo salama kwa ujenzi wa utamaduni wa ushindani. Utamaduni ambao ni msingi muhimu kwa Simba katika malengo yake ya kusaka ushindi wa taji la Ligi Kuu ya NBC na Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano mengine. Hili linaonekana kuwa chaguo la busara.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.