Utatu wa ushambuliaji Simba SCUtatu wa ushambuliaji Simba SC
  • Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC, kuunda safu ya utatu mkali wa ushambuliaji.
  • Utatu huo utawahusisha Mwalimu, Jonathan Sowah na Steven Mukwala.
  • Mabosi Simba SC wahamishia kambi Cairo, Misri kwa ajili ya ‘Pre-season’.

Simba wamepania! Ndivyo unavyoweza kusema. Hii ni baada ya tetesi kuthibisha kuwa, uongozi wa timu hiyo umekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco, Selemani Mwalimu. Staa huyo anatajwa kuwa muda wowote atajiunga na kikosi kwa ajili ya Pre-season nchini Misri.

Paisha ‘Kindege’ cha Sportpesa ushinde mamilioni sasa

Wakati ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Kuhusu usajili wa Mwalimu Simba

Sele Mwalimu Gomez
Sele Mwalimu Gomez

Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Simba vimethibitisha kuwa timu hiyo imemsaini Mwalimu kwa usajili wa mkopo wa mwaka mmoja. Nyota huyo sasa anatarajiwa kuunda safu kali ya utatu katika ushambuliaji. Mwalimu sasa anaungana na Sowah na Mukwala kwenye ushambuliaji Simba.

SOMA HII PIA: Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City ya Guardiola

Kuhusu safari ya kwenda Misri

Tayari kundi la kwanza na la pili la kikosi cha Simba yamewasili na yanaendelea na mazoezi nchini Misri. Mazoezi haya ni sehemu ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre-season’ ambayo tayari yamefikisha wiki zaidi ya wiki mbili. Kambi hii ya maandalizi ya kabla ya msimu wa mashindano (Pre Season), inatarajiwa kuwa ya mwezi mmoja.

Inatazamiwa, Mwalimu ataungana na kundi la tatu ambalo linawahusisha mastaa wote, ambao wanaendelea na majukumu ya timu za Taifa kwenye mashindano ya Chan 2024. Ikumbukwe kambi hiyo ya Misri ilitumiwa na Simba pia msimu uliopita.

Semaji Ahmed afunguka kuhusu timu kuwasili kwa makundi kambini Misri

Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC
Ahmed Ally

Ahmed akizungumzia kambi yao amesema: “Sehemu ya kikosi chetu tayari iko nchini. Hii inahusisha Kundi la kwanza na Kundi la pili, ambapo mpaka sasa wachezaji wanaokosekana ni wale wenye majukumu ya timu za Taifa. Hawa wanatarajia kuwa wa mwisho kuripoti kambini.

“Mwisho tunatarajia kambi itakuwa na nyota wetu wote, hususani baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa kuhusiana na michuano ya CHAN. Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 28, mwaka huu. Mara baada ya kurudi Simba tutaanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.”

SOMA HII ZAIDI: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Wabadilisha kambi kutoka Ismailia hadi Cairo

Baada ya kuweka kambi kwa siku 15 katika mji wa Ismailia, kikosi kimehamia jijini Cairo. Hii ni kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2025/2026. Wakati kikiwa katika kambi ya Ismailia kikosi kimefanikiwa kucheza mechi moja ya kirafiki, dhidi ya Karhaba Ismailia SC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Baada ya kufika Cairo kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi kwa siku nyingine 15, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam. Kikiwa kambini jijini Cairo kikosi kinatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki, ili kuliwezesha benchi la ufundi kuona jinsi wachezaji walivyoshika mafunzo wanayopewa. Kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu, tayari kuanza msimu mpya wa Ligi.

Zoezi la kutambulisha mashine mpya linaendelea

Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC
Morice

Kuhusu zoezi la kutambulisha mastaa wapya waliowasajili kwenye dirisha hili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC bado haijamaliza utambulisho na imepania kufanya usajili mkubwa. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa na wametamba kuendelea kushusha vyuma.

“Viongozi wanaendelea kuhakikisha kambi yetu ya Misri inaenda vizuri. Ili kufanikisha hili usimamizi mkubwa unafanyika. Pamoja na hayo pia bado hatujamaliza kutangaza mastaa wetu wapya, huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana nitaacha watu waone wenyewe.

Hawa hapa wamepigwa chini Simba SC mpaka sasa

Kuhusu maboresho ya kikosi chao, Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thank you’, Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni Che Malone aliyetimkia USMA, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein na Lionel Ateba nao baibai. Listi hii inatarajiwa kuongezeka.

Hitimisho: Simba Day yatangazwa

Simba Day
Simba Day

Huku taarifa ya Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC ikipamba moto. Uongozi wa timu hiyo umetangaza rasmi siku ya Simba yaani ‘Simba Day’. Hili ni tamasha rasmi la Simba ambalo hutumika kutambulisha mastaa wapya na kikosi cha msimu mpya, ambalo huambatana na burudani kadha wa kadha.

SOMA HII ZAIDI: Simba Day Septemba 10 2025 | Ali Kiba kutumbuiza | Ubaya ubwela pasua kichwa

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.