Ubingwa YangaUbingwa Yanga
  • Rayon Sports FC 1-3 Yanga SC, wananchi washinda ubingwa Rwanda.
  • Pacome, Boyeli na Mwamnyeto waizamisha Rayon Sports.
  • Kituo kinachofuata Ngao ya Jamii na Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2025/26.

Wakicheza katika ardhi ya ugenini nchini Rwanda, kikosi cha Yanga SC kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa Rayon Sports Cup. Yanga SC wameshinda ubingwa huo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports. Ni mastaa Pacome, Boyeli na Bakari Mwamnyeto waliosimamia shoo.

Shinda mamilioni sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa

SEO Banner LV

Huku ukiendelea kuhabarika na makala hii, unangoja nini kushinda sasa? Shinda mamilioni kupitia mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege, kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Cheza sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

 Rayon Sports FC 1-3 Yanga SC mchezo ulikuwaje?

Matokeo
Matokeo

Kama ambavyo ilitarajiwa na wengi, mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa. Ukipigwa kwenye Uwanja wa Amahoro Kigali, Rwanda ulivutia mashabiki wengi wa timuzoe mbili. Mchezo huu ulikuwa sehemu ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’ kwa timu zote mbili.

SOMA HII PIA: Yanga SC kuitikisa Rwanda Pre-Season kuvaana na Rayon

Uchambuzi wa mchambuzi Hans Raphael

Rayon Sports FC 1-3 Yanga SC: Highlights, magoli yote
Balla Conte

Mara baada ya mchezo huo mchambuzi wa michezo Hans Raphael alikuwa na haya ya kusema: “Achana na magoli ya Pacome, Boyeli na Mwamnyeto. Achana na kasi ya umeme ya Ecua na Chikola. Naomba tuzungumzie soka la kocha mpya wa Yanga “Romain Folz Ball.”

“Mechi ya kwanza ya ushindani ya Folz wote tumeiona. Anataka timu yake iwe compact wakati wa kuzuia na wakati wa kushambulia. Anahitaji kudumisha upana, huku akiwataka mawinga wake (Pacome & Ecua) waanzie mikimbio pembeni. Baada ya hapo wafanye mikato ya haraka ya wembe kuingia kwenye box la timu pinzani (Razor-sharp movements).

“Katikati ya uwanja Folz anahitaji fluidity (Free flowing football). Wale viungo watatu wanatakiwa kutengeneza umbo la pembe tatu (triangle), huku muda wote wakibadilishana nafasi. Folz anamtaka namba 6 kucheza kama namba 8.

“Kisha namba 8 kuchezakama namba 10 na namba 10 kucheza kama namba 6. Wale watatu (Balla Conte, Maxi na Doumbia) wanabadilishana sana nafasi. Tayari Idea ya Folz imeonekana kilichobaki ni kutafuta “Chemistry” baina ya mchezaji na mchezaji. Hii nahisi huenda itachukua miezi miwili hadi mitatu, baada ya hapo hakuna timu Tanzania itatamani kukutana na Yanga.”

SOMA HII PIA: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Walichosema Yanga baada ya ubingwa

Boyeli (-)
Boyeli

Mara Baada ya ushindi huo uongozi wa Yanga SC ulikiri kuwa na furaha kubwa ya kushinda fainali, kufanikisha malengo. Lakini kocha wat imu hiyo Folz aliweka wazi bado wana kazi kubwa mbele. Hii ikihusisha safari ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26.

Akizungumzia kwa furaha mara baada ya kuifungia Yanga bao moja kwenye ushindi huo Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema: “Ulikuwa mchezo mgumu, tunawapongeza Rayon Sports kwa kuonyesha ushindani mzuri. Hii ndio maana ya fainali na jambo jema kwetu ni kuwa tumeshinda ubingwa.

“Malengo yetu yalikuwa kufanikisha na kutwaa ubingwa na tulijua wazi kuwa mchezo hauwezi kuwa rahisi. Tunajivunia maandalizi makubwa ambayo tumeyafanya yametusaidia kupata matokeo chanya.”

SOMA HII ZAIDI: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Maandalizi siri ya ubingwa

Viongozi Yanga
Viongozi Yanga

Baada ya kushinda ubingwa huo, benchi la ufundi la Yanga SC limeelezea furaha yake. Kocha wa Yanga SC, Folz amesema kuwa Yanga SC kuwa mabingwa wa Rayon Sports Cup ni matokeo ya maandalizi mazuri na ushirikiano. Benchi hilo limetamba na kuongeza kuwa ubingwa huo unawapa jeuri na ari ya kufanya vizuri katika michezo yao ya mashindano mengine ambayo wanashiriki.

Mashabiki Yanga watamba kuzoa makombe

Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kwenye Uwanja wa Amahoro, Rwanda walitoa sapoti kubwa kwa kushangilia timu yao kwa nguvu. Hata baada ya ubingwa huo, wametamba kuendeleza kasi ya kuzoa makombe. Sehemu ya mashabiki hao walisema kwao hatua hiyo ni ya kujivunia.

Hitimisho: Kituo kinachofuata Ligi Kuu ya NBC 2025/26 na Ngao ya hisani

Baada ya ushindi huo, Yanga SC wanatarajia kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mashindano ya Ligi Kuu na taji la Ngao ya Jamii. Michezo hiyo inatarajiwa kuanza punde.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.