- Man United vs Arsenal ‘live’ Old Trafford, moto utawaka Jumapili hii.
- Huu sio tu ni mchezo wa Ligi Kuu England bali ni ‘Clash of Titans’ yaani vita ya wakuu wawili.
- United wameshinda mechi 99 kati ya 243 dhidi ya Arsenal, katika mashindano yote (Sare 55, Vipigo 89).
Vita ya Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa vikosi vya Manchester United na Arsenal, inatarajiwa kuanza rasmi kesho Jumapili. Hii ni kufuatia mchezo mkali ambao unasubiriwa kwa hamu kati ya timu hizo. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa klwenye Uwanja wa Old Trafford, ambapo Man United watakuwa nyumbani kusaka ubingwa wao wa kwanza msimu huu.
Bado haujashinda? Haya hapa mamilioni ya ‘Kindege’ cha SportPesa
Ukiendelea kuhabarika na makala hii je, bado haujashinda na kindege cha Sportpesa? unangoja nini kushinda sasa? Shinda mamilioni kupitia mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege, kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Cheza sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu Man United vs Arsenal: Takwimu muhimu

Licha ya timu zote kufanya maboresho kwa usajili mkubwa, lakini bado wengi wanaipa Arsenal nafasi kubwa ya kuibuka washindi. Hii ni mara ya pili tu, katika historia ya ligi Kuu England ambapo Manchester United wataikaribisha Arsenal kwenye mechi yao ya kwanza ya msimu. Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa msimu wa 1989/90. Katika mchezo huo Man United walishinda 4-1.
Wakati Man United wakijivunia rekodi hiyo, Arsenal ya Mikel Arteta nao wanajivunia rekodi ya kucheza mechi 14 mfululizo za ugenini kwenye Ligi Kuu England bila kupoteza. Hii rekodi ni tangu Novemba mwaka jana. Manchester United na Arsenal walikuwa na hali tofauti kabisa msimu wa mwaka 2024-25.
SOMA HII PIA: PSG 2-1 Arsenal UEFA Champions League: Fainali ni PSG vs Inter Milan
Msimu Uliopita kwa Pande Zote
United walikumbwa na msimu wao mbaya zaidi kwenye Ligi Kuu England wakimaliza nafasi ya 15. Ukiachana na mwenendo huo kwenye ligi, United pia walipoteza fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham. Arsenal waliukaribia ubingwa lakini wakaishia nafasi ya pili kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Ni wazi Arsenal watakuwa na lengo la kutwaa ubingwa msimu huu. Huu ukiwa ni msimu wa 100 mfululizo kwenye ligi kuu ya England. Ikiwa ndiyo timu ambayo imeshiriki mfululizo mara nyingi zaidi ya timu yoyote.
Arsenal wakali wa kushinda mechi za ufunguzi

Takwimu zinaonyesha Arsenal wamekuwa wakishinda mechi ya kwanza ya msimu, katika misimu mitano kati ya sita iliyopita (W5 K1), ikiwemo mitatu mfululizo. Rekodi yao bora zaidi ilikuwa kati ya 2001-02 na 2005-06 (ushindi mitano mfululizo). Msimu uliopita, walikuwa na rekodi imara ya ugenini – haswa nusu ya pili ya msimu.
SOMA HII ZAIDI: Tetesi za soka usajili Gyokeres kwenda Arsenal, Man United kufanya ‘ubaya ubwela?’
Usajili Mpya na malengo ya Arteta
Arteta ameimarisha kikosi chake majira haya ya joto kwa kuwasajili: Viktor Gyökeres, Martín Zubimendi na Noni Madueke. Gyökeres aliyefunga mabao 68 katika misimu miwili iliyopita, anapewa nafasi kubwa ya kuongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal. Ikumbukwe, Arsenal wamefunga katika kila moja ya mechi zao 11 zilizopita za Ligi Kuu kwenye uwanja wa Old Trafford (jumla ya mabao 14).
Ruben Amorim na Kikosi Kipya cha United

Amorim anatarajia kutoa mshangao katika msimu wake wa kwanza kamili akiwa kocha wa United. Amorim na kikosi chake wanaanza msimu wakiwa nyumbani, kwa mwaka wa tisa mfululizo. United wameshinda mechi yao ya kwanza ya msimu mara 22, hii ni zaidi ya timu yoyote nyingine. Pia wana kiwango bora zaidi cha ushindi siku ya kwanza (67%), kati ya timu zote zilizoshiriki misimu zaidi ya mmoja.
Msimu uliopita, United hawakushinda mechi mbili mfululizo za ligi hata mara moja. Lakini baada ya kuwafunga Aston Villa siku ya mwisho ya msimu. Wanaweza kufanikisha hilo kwa mara ya kwanza tangu walipoifunga Fulham 1-0, siku ya kwanza ya msimu uliopita. Kama ilivyo kwa Arsenal, United wamewekeza sana kwenye kikosi, wakiwasajili: Matheus Cunha, Bryan Mbeumo na Benjamin Sesko.
Hata hivyo, macho bado yanatarajiwa kuwa kwa nahodha wao Bruno Fernandes. Hii ni kwa sababu huyu ni nyota aliyekuwa mchezaji pekee wa United, kufunga nyumbani dhidi ya timu sita bora msimu uliopita ikiwemo na mkwaju wa adhabu dhidi ya Arsenal.
SOMA HII PIA: Tottenham 1-0 Manchester United mabingwa wa Europa League wapatikana, ukame wa miaka 17 wafutwa
Historia ya Man Utd vs Arsenal
Manchester United wamepoteza mechi mbili tu, kati ya 18 za mwisho za Ligi Kuu dhidi ya Arsenal wakiwa nyumbani (W10 S6). Hata hivyo, vipigo vyote viwili vilikuwa chini ya kocha Arteta (1-0 Novemba 2020 na Mei 2024).
United wameshinda mechi 99 kati ya 243 dhidi ya Arsenal katika mashindano yote (Sare 55, Vipigo 89). Wamewashinda Aston Villa pekee mara nyingi zaidi (107). Ikiwa watawafunga Arsenal Jumapili, watakuwa timu ya kwanza kuwafunga Gunners mara 100.
Utabiri wa Mechi: Man Utd vs Arsenal

Arsenal licha ya kucheza ugenini wanapewa nafasi kubwa ya ushindi kwa angalau asilimia 45.1, huku United wakipewa nafasi ya 29.5% ya kushinda. Utabiri was are ni 25.4% hii ni kwa mujibu wa utabiri wa Kompyuta za Opta.
Vikosi tarajiwa – Man Utd vs Arsenal
Man Utd: André Onana, Leny Yoro, Harry Maguire, Ayden Heaven, Amad Diallo, Casemiro, Bruno Fernandes, Bryan Mbeumo, Matheus Cunha, Benjamin Sesko.
Arsenal: David Raya, Jurriën Timber, William Saliba, Gabriel Magalhães, Riccardo Calafiori, Martin Ødegaard, Martín Zubimendi, Declan Rice, Bukayo Saka, Viktor Gyökeres, Gabriel Martinelli.
Hitimisho
Kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanyika kwa timu zote mbili, mchezo wa Man United vs Arsenal ‘live’ Old Trafford unatarajiwa kuwa mgumu nawa aina yake. Kila timu itatoa majibu sahihi

