BarakatBarakat
  • Azam FC imefanya usajili wa kimkakati kwa kiungo Feisal Salum ambaye alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC na Simba SC zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania.
  • Sadio Kanoute kiungo mgumu aliyewahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba SC ndani ya viunga vya matajiri wa Dar.
  • Kwenye anga la kimataifa Azam FC kuanzia ugenini kuwakabili wapinzani wao Al Merriekh Bentui ya Sudan Kusini, 

 Azam FC wamedhamiria kufanya kweli msimu mpya wa 2025/26. Hilo linatokana na usajili wa kimkakati kwa kumuongeza mkataba Feisal Salum na kutambulisha wapya wengine. Mbali na usajili timu ya Azam FC imeweka kambi Rwanda kwa maandalizi ya mashindano ya ndani ikiwa ni ligi ya NBC na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mamilioni yanakusubiri, paisha kindege ushinde

Kuna mamilioni ambayo yanakusubiri sasa hivi. Rahisi sana, paisha kindege ushinde. Cheza Aviator upate mgao wako bila kipengele.

Aviator banner

Usajili wa kimkakati kwa Feisal Salum

Fei utambulisho
Fei kiungo wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Rasmi Feisal akubali kusaini mkataba wa kufuru

Moja ya usajili wa kimkakati ni kubaki na kiungo Feisal Salum. Ilikuwa inaelezwa kuwa Feisal yupo kwenye rada za Simba SC na Yanga SC ambao walikuwa wanahitaji saini yake. Mwisho nyota huyo bado atasalia kwenye viunga vya Azam Complex.

 Inaelezwa kuwa Feisal ameongeza mwaka mmoja kubaki Azam yupo hapo mpaka 2027. Feisal alibakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC. Kutokana na kuwa katika ubora jambo hilo lilifanya timu nyingi kuwania saini yake.

Kwa msimu wa 2024/25 Feisal alikuwa namba moja kwa watengeneza pasi za magoli. Alitengeneza jumla ya pasi 13 na alifunga mabao manne. Jumla alihusika kwenye 17 ndani ya kikosi hicho ambacho kilimaliza msimu kikiwa nafasi ya tatu.

Inaelezwa kuwa Azam FC wamempa Feisal hela binafsi ya kusaini mkataba mpya (Sign on fee ya Tsh 800m cash). Mshahara wa Tsh 50m (take home), kwa mwezi hii ni baada ya makato na kodi. Ubalozi wa Azam Pesa ambapo kwa mwaka atalipwa Tsh 200m.

Hawa hapa wachezaji wapya Azam FC

Lameck Lawi

Lameck Lawi, alitambulishwa Julai 3 2025 kwa kandarasi ya miaka miwili. Huyu ni beki alikuwa ndani ya Coastal Union. Coastal Union ilikuwa ndani ya tano bora kwa timu ambazo zilifungwa mabao machache msimu wa 2024/25. Baada ya dakika 2,700 kwenye mechi 30 ni mabao 31 timu hiyo ilifungwa.

Malima

Muhsin Malima alitambulishwa Azam FC Julai 7 2025. Huyu ni kiungo ambaye alitokea Zed FC ya Misri. Msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya viunga vya Azam Complex.

Air Manula

Aishi Manula ----
Aishi Manula kipa mpya wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC i

Aishi Manula Julai 8 2025 alitambulishwa ndani ya Azam FC akiwa mchezaji huru akitokea Simba SC. Nyota huyo ni dili la miaka mitatu alisaini. Atadumu hapo mpaka 2028.

Himid

Himid Mao, Ninja alitambulishiwa ndani ya Azam FC, Julai 9 2025 kuwa ingizo jipya ndani ya timu hiyo. Ni dili la mwaka mmoja. Atadumu Azam FC mpaka 2026.

Pape

Pape Doudou, alisaini mkataba wa miaka miwili, ndani ya Azam FC. Ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Generation Foot. Msimu uliopita wa 2024/25 alicheza kwa mkopo Linguère de Saint-Louis. Alitambulishwa Julai 30 2025.

Kitambala

Agosti 10 2025 Azam FC ilimtambulisha mshambuliaji Jepht Kitambala. Huyu ni raia wa DR Congo atakuwa hapo mpaka 2026. Alisaini dili la mwaka mmoja.

Baraket

Baraket Ihmid huyu ni winga aliyekuwa anacheza Klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Ni Agosti 15 2025 alisaini dili la miaka miwili. Yupo Azam FC mpaka 2027.

Zitoun

Taieb Ben Zitoun huyu ni mshambuliaji alikuwa anacheza Al Hilal ya Sudan. Msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Azam FC. Ni dili la miaka miwili alisaini. Alitambulishwa rasmi Agosti 15 2025.

Manyama

 Edward Manyama ni beki alitambulishwa Azam FC Agosti 12 2025. Ni kadarasi ya mwaka mmoja alisaini. Yupo hapo mpaka 2026.

Sadio Kanoute

Sadio
Sadio Kanoute kiungo mkabaji wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Azam FC 2025: Kikosi, Mafanikio na Urithi wa Klabu

Kiungo mkabaji mzee wa mikato ya kimyakimya alitambulishwa ndani ya Azam FC. Anaitwa Sadio Kanoute ambaye aliwahi kucheza Klabu ya Simba SC. Ni Agosti 11 2025 alitambulishwa kuwa ndani ya Azam FC. Kandarasi yake ni miaka miwili.Yupo hapo mpaka 2027.

Kambi Rwanda

Matajiri wa Dar, Azam FC kambi yao itakuwa Rwanda.Tayari kikosi kipo Kigali Agosti 15 kilitia timu huko. Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi hicho ni Sadio Kanoute ambaye ni ingizo jipya. Tepsi Evance, Sospeter Bajana, Himid Mao.

Mpinzani wao kimataifa huyu hapa

Azam FC imepangwa kucheza dhidi ya Al Merriekh Bentui ya Sudan Kusini. Itakuwa ni kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC 1st Preliminary Round). Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 19-21.

Mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Septemba 26-28 2025. Ikiwa itapenya raundi hiyo itakutana na mshindi wa jumla wa mechi nyingine kati ya AS Port ya Djibout dhidi ya KMKM ya Zanzibar. Ikishinda hapo itakuwa imetinga hatua ya makundi.

Hitimisho

Azam FC msimu wa 2024/25 ilipishana na mataji yote iliyokuwa inayasaka. Hesabu kubwa kuelekea msimu mpya ni kufanya mapinduzi. Msimu mpya unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote.

image
Share this: