- Rasmi Feisal akubali kusaini mkataba wa kufuru, hii ni baada ya vuta nikuvute nzito ya timu vigogo.
- Swali kubwa kwenye vijiwe vya soka limekuwa je, Feisal kucheza Simba SC, Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26?
- Simba SC, Yanga SC na Azam FC zimekuwa zikipigana vikumbo na hatimaye Feisa amefanya maamuzi.
Kwenye soko la uisajili kuna tetesi nyingi zinaendelea, lakini kubwa ya yote ni kuhusu wapi Feisal atacheza msimu ujao. Hii ni baada ya timu vigogo za Simba SC, Yanga SC au Azam FC kuwa vitani kuwania sani yake. Baada ya vita ya muda mrefu, taarifa za kikachero zimethibitisha kuwa hatimaye Feisal amefanya maamuzi.
Shinda mamilioni sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa

Ukiendelea kuhabarika na makala hii, unangoja nini kushinda sasa? Shinda mamilioni kupitia mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege, kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Cheza sasa kwa kubonyeza picha hii chini.
Feisal kucheza Simba SC, Yanga SC au Azam Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu ikoje?
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zimethibitisha kuwa ni kweli Simba SC, Yanga SC na Azam FC zimezungumza na Feisal. Kila timu ilipeleka ofa mezani ambayo walihisi inaweza kumshawishi nyota huyo wa Zanzibar. Taarifa za kuaminika ni kuwa, mpaka sasa Azam FC wamefanikiwa kumshawishi staa huyo kusaini mkataba mpya.
Ibenge atoa msimamo mzito kuhusu Feisal

Kufuatia michakato hiyo ya Yanga SC na Simba SC kumng’oa Feisal Chamazi. Kocha mpya wa Azam FC, Florent Ibenge amewambia viongozi wake wasimuuze Fei Toto ndani ya dirisha hili. Kocha huyo amewambia wamzuie kiungo huyo kwa gharama yoyote kwani kikosi chake kipya kitajengwa kupitia Feisal.
SOMA HII PIA: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?
Feisal kuondoka huru Azam?
Ikumbukwe kabla ya kusaini mkataba mpya, Feisal alikuwa amebakiza mwaka mmoja tu, ndani ya kikosi hiko cha Azam FC. Kama ingesalia hivyo basi Feisal angeondoka huru kujiunga na timu yoyote ambayo angefikia makubaliano nao. Lakini taarifa zinaeleza kuwa, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kusalia Chamazi.
Dondoo kuhusu mkataba mpya wa Feisal na Azam FC
Mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael amefafanua ofa hiyo mpya ya Azam kwa Feisal ambapo amesema: “Feisal ameongeza mwaka mmoja kubaki Azam hadi 2027. Feisal alibakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC. Jumanne wiki hii Feisal ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na sasa ana mkataba wa miaka miwili.
“Kila kitu kimekamilika Feisal amesaini na tayari picha za utambulisho wake zimepigwa. Mkataba huo ni wa rekodi ambapo Feisal sasa atakuwa mchezaji mzawa ambae analipwa hela nyingi kuliko wote.
Gharama za ofa ya mkataba ni kama ifuatavyo;
Azam wamempa Feisal hela binafsi ya kusaini mkataba mpya (Sign on fee ya Tsh 800m cash). Mshahara wa Tsh 50m (take home), kwa mwezi hii ni baada ya makato na kodi. Ubalozi wa Azam Pesa ambapo kwa mwaka atalipwa Tsh 200m. Lakini pia Azam wame-activate kipengele cha mauzo yake ‘buyout clause’ yake kutoka $500,000 na saaa inatajwa ni $800,000.
Kwanini ni ngumu Simba SC na Yanga SC kumnasa Feisal

Taarifa ambazo zinasalia kuwa tetesi ni kuwa kilichowafelisha Simba SC na Yanga SC ni thamani ya Feisal sokoni. Hans anaendelea kusema: “Ilikuwa ngumu kwa wababe wa Kariakoo kwani, ili kumpata Fei Simba na Yanga walitakiwa kuwa na angalau Billion 2.1. Hapo unalipa billion 1.3 ya kuvunja mkataba wake na Azam. Baada ya hapo unahitaji kumpatia Tsh 800m Fei kama hela ya Sign on fee.”
“Ukimaliza na hayo bado unasalia kupaswa kumlipa mshahara wa Tsh 80m kwa mwezi hiyo ni kabla ya makato. Tsh 80m x miezi 12 utagundua kwa mwaka inabidi umlipe Fei mshahara wa Tsh 960m. Ukichukua 2.1B + 960m utapata kitu kama 3B.”
SOMA HII ZAIDI: Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu yake iko hivi
Hitimisho: Mchezaji muhimu wa Stars CHAN 2024

Nyota njema inaendelea kumuwakia Feisal, ambapo ukiachana na ukweli kuwa ni rasmi Feisal akubali kusaini mkataba wa kufuru na Azam, kwa sasa akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachoshiriki mashindano ya Chan 2024 amekuwa nyota muhimu. Feisal amehusika kwa kiasi kikubwa na ushindi wa mechi 3 za kwanza walioupata Stars, huku akishinda tuzo binafsi moja ya mchezaji bora.

