Bajaber KambiniBajaber Kambini
  • Simba SC ikiwa nchini Misri imepata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.
  • Jonathan Sowah na Bajaber wamefungua akaunti ya magoli wakiwa na uzi wa Simba SC kambini.
  • Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC abainisha mpango mzima ulivyo na wanachotakiwa kufanya kwa msimu mpya.

Kambi ya Simba SC nchini Misri imezidi kupamba moto. Agosti 11 2025 ilicheza mchezo wa kirafiki na kupata ushindi. Kwenye mchezo huo ilikuwa Simba 2-0 Kahraba Ismailia.

Ushindi unakusubiri ukicheza Aviator unavuna mamilioni

Marubani ni muda wao kuvuna mkwanja mrefu. Mgao wa mamilioni unakusubiri ukicheza Aviator ya SportPesa. Cheza sasa hivi uvune unachostahili.

SEO Banner LV

Wafungaji magoli kwenye mchezo huo

Sowah Red
Sowah Jonathan mshambuliaji mpya wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Jonathan Sowah atoa ahadi nzito Simba SC 2025/26

Wachezaji wapya walifunga magoli katika mchezo huo wa kirafiki. Ni Mohamed Bajaber aliyetambulishwa Simba SC akitokea Polisi ya Kenya. Bajaber alifunga goli hilo akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia. Na goli la pili lilifungwa na Jonathan Sowah.

Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia ulichezwa Uwanja wa Suez Canal Authority. Malengo makubwa ni utayari wa wachezaji kuelekea msimu mpya. 2025/26 unatarajiwa kuwa msimu wenye ushindani mkubwa.

Huyu hapa Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC

Kocha Simba Fadlu
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids. Source: Simba SC.

Soma hii: Mo Dewji aibua jambo Simba SC

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuwa wamefanya maboresho makubwa kwenye kikosi kwa kupata saini za wachezaji ambao watakuwa na kazi kupambana kwenye mashindano ambayo watashiriki.

Simba SC msimu wa 2024/25 ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea hatua ya fainali ikiwa nafasi ya pili na bingwa alikuwa RS Berkane. Msimu wa 2025/26 Simba SC itapeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Fadlu ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye aina tofauti ya mashindano.Kutokana na hali hiyo watakutana na ushindani mkubwa. Aliongeza kwa kubainisha kuwa licha ya kuwa malengo makubwa ni kupata matokeo kwenye mechi zao.

“Unaona kuna wachezaji ambao wamesaini kwenye kikosi. Ni aina ya wachezaji wazuri ni saini nzuri ambazo zipo kwenye kikosi. Tutakuwa kwenye mashindano tofauti msimu huu ukiachana na ligi tutakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Aina ya ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni tofauti na kwenye Kombe la Shirikisho Afrika hivyo muhimu ni kuwa imara na tayari kwa ajili ya ushindani kwenye mechi zetu ambazo tutacheza.

“Kambi ambayo ipo kwa sasa ninaona tunaendelea vizuri kuna mechi ambazo tutacheza kwa ajili ya kuwa imara zaidi hivyo bado tuna muda wakufanya maandalizi zaidi.”

Ni Misri kambi ya Simba SC

Simba SC imeweka kambi nchini Misri. Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wachezaji hao wanaendelea na maandalizi. Miongoni mwa wachezaji ni Leonel Ateba, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu, Joshua Mutale, Moussa Camara.

Budo Kambini
Joshua Mutale kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Elie Mpanzu Kibisawala ni Simba SC 2025/26

Wapo wachezaji waliokuwa na kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25. Miongoni mwa hao ni Ladack Chasambi ambaye ni kiungo mshambuliaji. Kwenye eneo la makipa yupo Hussen Abel.

Wachezaji wapya waliopo kambini ni Jonathan Sowah. Huyu ni mshambuliaji aliibuka hapo akitokea kikosi cha Singida Black Stars. Anthon Mligo huyu ni beki wa kushoto aliibuka hapo akitokea Namungo.

Wapinzani wa Simba SC kimataifa

 Katika anga la kimataifa Simba SC ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza hatua ya awali. Mpinzani wake ni Gaborone United ya Botswana. Droo ya michuano ya CAF ngazi ya klabu CAF CL na CAF CC ilifanyika Agosti 9 2025 katika studio za Azam TV, Dar.

Simba SC itaanzia ugenini na kukamilisha kete ya pili ikiwa nyumbani. Mechi ya ugenini inatarajiwa kuwa kati ya Septemba 19-21. Kati ya Septemba 26-28 itakuwa ni mechi ya pili Simba SC ikiwa Dar.

Msikie Mzamiru Yassin

Mzamiru Yassin kiungo wa kazi ndani ya Simba SC yupo Misri. Hakuwa na msimu mzuri 2024/25 kutokana na kutokuwa fiti. Kwa sasa yupo imara na anaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.

Kiungo huyo mkabaji amebainisha kuwa maandalizi yanakwenda vizuri. Aliongeza kwa kubainisha kuwa msimu mpya hautakuwa mwepesi. Ikumbukwe kwamba msimu uliopita Simba SC ilipishana na taji la ligi ambalo lipo mkononi mwa Yanga SC.

“Tangu maandalizi yameanza kila kitu kinakwenda vizuri. Tunamshukuru Mungu. Sina shaka kila mtu anajitolea na kuonyesha uwezo wake kwa mwalimu.

“Mara nyingi wachezaji wenyeji huwa tunawapokea vizuri wageni. Wenyewe wanaupokea uwenyeji wetu vizuri. Mwalimu anazidi kutuunganisha pamoja. Tangu tumekuwa hapa ile nguvu ya pamoja inaenda vizuri.

“Nina amini tukiendelea kupush tutakuwa na mwendo mzuri. Msimu ujao hautakuwa mwepesi ila maandalizi ambayo tunayafanya yanatupa picha kuwa tutafanya vizuri. Tutapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,”.

Hitimisho

Simba SC ilikosa mataji msimu wa 2024/25 na kambi ilikuwa Misri. Hesabu kubwa kwa msimu mpya ni kupambania mataji. Kwenye anga la kimataifa walishika nafasi ya pili na bingwa alikuwa RS Berkane.

image
Share this: