- Yanga SC kuitikisa Rwanda Pre-Season kuvaana na Rayon Agosti 13, mwaka huu.
- Kikosi kipya cha Wananchi kinaendelea kusukwa, na aliyewahi kuwa kocha msaidizi Sundowns, Roman Folz.
- Rais wa Yanga Sc Eng. Hersi Said amewatangazia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo kuwa, Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika 07/09/2025.
Kikosi cha Yanga wikiendi hii au mwanzoni mwa wiki ijayo kinatarajiwa kuondoka nchini na kuelekea Rwanda. Timu hiyo inaenda Rwanda kwa mwaliko maalum kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Mchezo huo unatarajiwa kuwa dhidi ya kikosi cha Rayon Sports.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa
Endelea kuhabarika na makala hii, lakini kumbuka una nafasi ya kushinda mamilioni. Hii ni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege. Kushinda fedha nyingi cheza na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kamwe atoa tamko zito safari ya Rwanda

Huku wakiendelea na maandalizi ya safari hiyo Ofisa Habari wa Yanga SC Ali Kamwe ameelezea mchongo mzima akisema: “Hivi karibuni tulizindua kampeni ya Tofali la ubingwa. Hii ililenga kuwapa wanachama nafasi ya kuchangia timu yao kwa ajili ya kuipa misuli ya kifedha.
“Misuli hii ya kifedha ni muhimu kwa ajili ya kipindi hiki, ambacho timu ina mahitaji makubwa ya fedha. Mahitaji haya ni kwa ajili ya kufanikisha usajili na maandalizi ya kambi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’. Ikumbukwe maandalizi ni bora ili kuweza kutimiza malengo yetu ya ubingwa kwa msimu mzima.
“Tayari tumepata mwaliko wa kwenda Rwanda kwa ajili ya kushiriki siku ya kilele cha klabu ya Rayon Sports na napenda kuwahakikishia kuwa tutashiriki, na tutawatangaziautaratibu mzima wa safari.”
SOMA HII PIA: Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Kikosi kipya kusukwa chini ya kocha mpya Msauzi, Roman Folz

Kikosi kipya cha Wananchi kinaendelea kusukwa, na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns Roman Folz. Kocha huyo ni miongoni mwa wakufunzi wenye wasifu mkubwa na uzoefu na sola la Afrika. Hali hii inaonekana kutarajiwa kuwapa faida Yanga katika kuunda kikosi kuelekea msimu ujao wa 2025/26.
Folz na benchi lake jipya la ushindi tayari wameanza rasmi majukumu yao ya kuinoa Yanga. Hii ni kupitia kambi ya maandalizi kabla ya msimu ‘Pre-season’ inayoendelea kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.
SOMA HII ZAIDI: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26
Kuhusu usajili kuelekea 2025/26

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa bado hawajamaliza utaratibu wa kutambulisha mastaa wao wapya. Hii ni licha ya kutangaza kumalizana na mastaa zaidi ya watano wapya mpaka sasa. Uongozi wa Yanga SC umeendelea na ujenzi wa kikosi chao. Bado kuna listi ya mastaa wengine wakubwa wanasubiri utambulisho.
Ogopa matapeli hawa wamekula dili mpya
Pamoja na kushusha mashine mpya, lakini mabosi wa timu hiyo wameendelea kufanya kazi kubwa ya kuwaongezea mikayaba mastaa wao. Viungo Pacome, Maxi na Abuya wote wameongeza mikataba ya miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya Yanga. Hivyo mastaa hao wanatarajia kumaliza rasmi mikataba yao mwaka 2027.
Wengine walioongezewa mikataba Yanga mpaka sasa

Mpaka sasa Yanga SC tayari imefanikiwa kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wao kadhaa. Miongoni mwa mastaa hao ni Pamoja na nahodha wao msaidizi, Dickson Job, Kiungo Denis Nkane na Mudathir Yahya. Imeelezwa kuwa Yanga wanaendelea kufanya maboresho ya mikataba ya mastaa wengine.
SOMA HII PIA: Mohamed Hussen Zimbwe Jr rasmi ni mali ya Yanga SC | Rekodi zake na timu alizocheza | Mafanikio
Hitimisho: Rais Hersi atangaza Mkutano mkuu
Rais wa klabu ya Yanga Sc Eng. Hersi Said amewatangazia wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo kuwa. Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 07/09/2025 kuanzia saa nne kamili asubuhi. Mkutano huo utakaofanyika kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2021.
Uratibu wa mkutano huo unaonyesha kuwa, utafanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), uliopo posta jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 8, 2025 iliyotolewa na Rais Eng. Hersi imeorodhesha ajenda za Mkutano huo ambazo ni pamoja na;
1. Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa wajumbe wanaohudhuria mkutano.
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.
5. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji.
8. Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia, pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya Klabu.
9. Kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofata.
10. Kufunga Mkutano

