Yanga SC vs WilieteYanga SC vs Wiliete
  • Ratiba ya Caf Champions League 2025/26 imezinduliwa rasmi.
  • Droo hii ilifanyika kwenye ukumbi wa Azam Media Studio, Dar es Salaam Tanzania mnamo Agosti 9, 2025.
  • Simba SC yapangwa kucheza dhidi ya Gaborone United, huku Yanga SC wakipangwa kumenyana na Wiliete Benguela.

Historia imeandikwa leo Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam. Hii ni baada ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), kufanya tukio muhimu la droo ya hatua ya awali. Droo hiyo ya Caf Champions League itahusisha timu 62 kwa ujumla. Raundi ya kwanza itapigwa kati ya tarehe 19–21 Septemba, huku mechi za marudiano zikipigwa kati ya tarehe 26–28, Septemba.

Unahitaji pesa? Shinda mamilioni ya kindege ‘Aviator’ cha SportPesa sasa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani Aviator ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda sasa kirahisi kwa kubonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Kuhusu droo ya CAF Champions League 2025/26

Mkeka wa droo CAF
Mkeka wa droo CAF

Droo hii ilifanyika kwenye ofisi za Kampuni ya Azam Media, ambao ni wabia wa CAF katika haki za matangazo. Droo zilianza saa 7 mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Viongozi na magwiji mbalimbali wa soka walialikwa kushiriki tukio hilo.

SOMA HII PIA: Yanga SC kuitikisa Rwanda Pre-Season kuvaana na Rayon

Sunday Manara aongoza shoo

Manara akinogesha droo
Manara aongoza droo

Staa wazamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu mbalimbali ikiwemo mabingwa wa Tanzania Yanga SC, Sunday Manara alipewa heshima kushiriki tukio hilo. Manara alitarajiwa kushirikiana na nyota wa zamani wa Simba SC, Abdalla Kibadeni. Ikumbukwe Magwiji hao wana heshima kubwa Tanzania, Kibadeni kwa hat-trick yake ya Kariakoo Derby mwaka wa 1977, Huku Sunday akiwa shujaa wa kwanza wa Tanzania kucheza Ulaya.

SOMA HII PIA: Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC: Mashine nyingine 6 kutangazwa tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Ligi ya mabingwa timu 62 kuanzia hatua ya awali

Kwa upande wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu 62 zimepangwa kuanzia hatua ya awali. Baadhi ya timu ambazo hazitaanzia hatua hiyo ni Al Ahly (Misri), na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini). Timu hizi zinatarajiwa kuanzia hatua ya pili ya awali.

Mfumo wa ‘pot’ watumika

Simba SC vs Gaborone United kule Yanga SC vs Wiliete Benguela: Droo ya CAF
Rais Yanga Hersi Said

Timu ziligawanywa katika mfumo wa vibakuli ‘pots’ 1, 2 na 3 kuendana na mabadiliko ya viwango vyao. Kupitia mfumo wa ‘pots’ kulichaguliwa makundi kwa kuzingatia mamlaka ya klabu na ukaribu kikanda. Hii ilitoa taswira ya mpangilio wa mechi za awali.

SOMA HII ZAIDI: Jonathan Sowah atoa ahadi nzito Simba SC / Magoli aliyofunga / Kambi Misri kinachoendelea

Azam FC na Singida Black Stars kuibeba Tanzania Shirikisho

Ukiziacha Simba SC na Yanga SC zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Tanzania pia inatarajiwa kuwakilishwa na Azam FC na Singida Black Stars katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Timu zote hizo zimetamba kujipanga vizuri kuendeleza rekodi ya kufanya vizuri katika mashindano hayo makubwa Afrika.

Ratiba rasmi ya mashindano ilikuwa kama ifuatavyo:

Raundi ya kwanza ya awali ya mashindano haya inatarajiwa kupigwa kati ya 19–21 Septemba. Huku michezo ya marudiano ikitarajiwa kupigwa kati ya 26–28 Septemba. Raundi ya Pili ya awali (Second Preliminary Round), nayo kwa mechi za kwanza zinatarajiwa kupigwa kati ya 17–19 Oktoba na mechi za marudiano itakuwa kati ya 24–26 Oktoba.

Hatua ya makundi inatarajiwa kuanza Novemba 21, 2025. Baada ya kumalizika kwa hatua hiyo itafuatiwa nah atua ya mtoano. Hatua ya mtoano inatarajiwa kuanza 13, Machi 2026.

Maneno halisi kutoka kwa Viongozi TFF, Simba SC na Yanga SC

Rais TFF Wallace Karia
Rais TFF Wallace Karia

Kufuatia droo hiyo viongozi mbalimbali wa soka nchini ambao walihudhuria walitoa maoni yao kama ifuatavyo;

Kwa niaba ya Azam FC, Afisa Habari wao Hashim Ibwe amesema: “Timu tulizopangwanazo hatuzichukulii kawaida hata kidogo, kwa sababu hazikufika hapa kwa bahati mbaya.” Azam FC imepangwa na El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini. Ibwe pia ameweka wazi kuwa kwa kuwa wataanzia ugenini, hiyo itawasaidia kujua ramani ilivyo.

Simba ikiwakilishwa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema, anaamini hawatokuwa na kazi ngumu ya kuvuka. Hii ni baada ya kukutana na Gaborone United ya Botswana. Try Again anasema wamefanya usajili mzuri ambao wanaamini watawafikisha mahali wanapopataka msimu ujao.

“Kwa miaka mitano, sita Simba SC imekuwa kwenye ubora wake uleule katika mashindano ya kimataifa. Tunajua ni mashindano magumu. Lakini tunaamini uzoefu wetu utatubeba kushindana na wapinzani wetu,” amesema Try Again.

Nao Yanga SC kupitia kwa Rais wa klabu hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti Chama cha Klabu Afrika (ACA), Hersi Said amesema timu yake imejipanga. Hersi amesema wanaendelea kujipanga vema, kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe Yanga SC wamepangwa kucheza dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola.

Hersi amesema wana malengo mazuri msimu huu, jambo la msingi ni kumuomba Mungu. Hii ni ili waweze kufanya vema katika mashindano watakayoshiriki. Hersi amesema: “Tutajiandaa vizuri kwa ajili ya kwenda katika mchezo wetu wa kwanza ambao utakuwa Angola.”

Naye Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Wallace Karia amesema: “Tumeweka historia, kizazi chetu kimeweka historia nyingine. Droo hii inafanyika kwetu, sio kwamba tumependelewa. Tunastahili kupata hivi vinavyofanyika hapa, huku akitaja michuano ya CHAN 2024 ambayo bado inaendelea.

Hitimisho

Kufanyika kwa droo ya Caf Champions League 2025/26 ni kipyenga rasmi cha ufunguzi wa mashindano haya. Ni wazi, kila timu sasa inao wajibu wa kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuonyesha matokeo bora. Ikumbukwe Simba SC na Yanga SC, zinabeba matumaini ya mashabiki wa Tanzania katika mashindano haya.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.