Ellie MpanzuEllie Mpanzu
  • Mpanzu atua kwa kishindo Misri, uongozi wa Simba waibuka watoa tamko zito.
  • Ishu ya kutajwa kuibukia Yanga yawa gumzo, yazua vita mtandaoni.
  • Simba wajichimbia Misri kwa mwezi mmoja kupanga mashambulizi ya Ligi Kuu NBC 2025/26

Baada ya kuwepo kwa sintofahamu kubwa kumhusu kiungo mshambuliaji wa Simba, Ellie Mpanzu hatimaye imefikia mwisho. Hii ni baada ya uongozi wa Simba kuthibitisha rasmi kuwa staa huyo bado yupo sana Simba. Mpanzu amewasili leo Jumanne kwa kishindo nchini Misri kwenye kambi ya kujiandaa na msimu ‘pre-season’.

Unajua kuwa ‘Kindege’ cha Sportpesa kinakupa mamilioni leo?

Huku ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Kuhusu tetesi za Mpanzu kuondoka Simba SC na kutua Yanga SC

Hivi karibuni taarifa za uchunguzi kutoka vyanzo mbalimbali ziliripoti kuwa, Yanga walikuwa kwenye mpango thabiti wa kumtaka Mpanzu. Taarifa hiyo ilieleza kuwa mabosi wa Yanga walianza mpango wa kumnasa nyota huyo. Baadhi ya machapisho mbalimbali ya viongozi wa Yanga kwenye mitandao ya kijamii nayo yalizua gumzo.

Vita ya maneno yaibuka mitandaoni

Kufuatia machapisho hayo, iliibuka vita ya maneno isiyo rasmi mitandaoni. Vita hii iliwahusisha baadhi ya viongozi wa Simba SC na Yanga SC ambao walirushiana maneno. Hali hii iliwaweka kwenye sintofahamu mashabiki wa timu zote mbili juu ya nini cha kuamini.

Semaji la Simba Ahmed Ally lacharuka!

Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC
Ahmed Ally

Kufuatia nyota huyo kutinga kambini leo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema: “Wapinzani wetu wamepambana sana kumpata Elia Mpanzu. Wamehangaika kumrubuni kwa kumuahidi ahadi nyingi za uongo.

“Mbaya zaidi walidanganywa kuvunja mkataba wake ni Milioni 300. Hivyo wakapata imani ya kumpata na hapo wakaanza tambo na matangazo. Watabe tukawa tunawaangalia tuu wanavyohangaika. Baada ya kuona wameshindwa kumsajili, wakaanza kulazimisha taarifa za Mpanzu kuwasili kambini, kimsingi jaribio lao limegonga mwamba na huo ni mwendelezo wetu kulinda wachezaji wetu tunaowahitaji.”

SOMA HII ZAIDI: Bosi Simba SC: Ogopa matapeli Ellie Mpanzu hauzwi, RS Berkane kunyonyolewa Mei 17 2025 CAF

Utambulisho wa mstaa wapya unaendelea

Mpanzu atua kwa kishindo Misri
De Reuck

Kuelekea msimu ujao wa 2025/26, Simba SC wameendelea kuboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wapya waliokamilisha usajili. Tayari majina kama Sowah, Morice na wengine yametambulishwa. Lakini mabosi wa msimbazi wamesema kazi bado inaendelea.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji kadhaa na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII PIA: Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC | Simba SC yatoa masharti mazito | Magoli na rekodi zake CAF

Kuhusu mazoezi na kambi yao nchini Misri

Rushine Kambini
Rushine Kambini

Tayari sehemu kubwa ya mastaa wa Simba SC wamewasili nchini Misri tayari kuendelea na kambi ya kabla ya msimu. Kikosi cha Simba SC kiliondoka nchini kwa mafungu mawili mwishoni mwa wiki iliyopita. Kambi hiyo inahusisha wachezaji wote isipokuwa tu, wale ambao wako kwenye majukumu ya Chan.

Ahmed akizungumzia kambi yao amesema: “Kikosi chetu kimeweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu mchini Misri. Kambi inatarajiwa kuwa na nyota wetu wote isipokuwa waliopo kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN. Kikosi kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 28, mwaka huu, mara baada ya kurudi Simba tutaanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026.”

SOMA HII PIA: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26: Straika mpya Yanga huyu hapa, Chama ‘Out’

Hitimisho: Nyota hawa wameachwa na Simba SC mpaka sasa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao Simba SC tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thank you’, Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni: Che Malone aliyetimkia USMA, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.