Aziz AndambwileAziz Andambwile
  • Aziz yupo sana Jangwani mpaka 2027 kutimiza majukumu yake kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.
  • Yanga SC ina orodha ya wachezaji wapya zaidi ya wawili na wengine wameongeza mikataba kuwa Jangwani.
  • Jina la Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyekuwa nahodha wa Simba SC 2024/25 linasubiriwa kwa shauku kubwa.

Aziz Andambwile bado yupo sana Jangwani baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili. Andambwile ana kazi kubwa kupambania namba ndani ya Yanga SC msimu wa 2025/26. Msimu uliopita hakuwa chaguo la kwanza kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu. Wengine wanatarajiwa kuendelea kutambulishwa.

Paisha kindege uvune mamilioni

Marubani ushindi ni furaha yao hasa wanapokamilisha safari kwa ushindi. Ni muda wa kuvuna mamilioni sasa ukipaisha kindege hewani. Cheza kila siku Aviator uwe mshindi.

Aviator banner


Novemba 6 2024 zama za Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwenye mchezo dhidi ya Tabora United alipata maumivu. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa alikwama kukomba dakika 90. Mchezo huo ulikamilika kwa ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Yanga 1-3 Tabora United.

Aziz --
Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC

Soma hii: Yanga SC wanazitaka pointi tatu za Tanzania Prisons Juni 18 2025

Jina lake ni Aziz Andambwile 2024/25

Ni Aziz Andambilwe alicheza jumla ya mechi tano za ligi msimu wa 2024/25. Kwenye mechi hizo alitumia dakika 125. Hakufunga wala kutoa pasi ya bao kiungo huyo wa Yanga SC.

Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alikomba dakika 90. Unakuwa ni mchezo pekee aliovuja jasho mwanzo mwisho ndani ya ligi. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Mchezo huo ulichezwa Oktoba 22 2024, mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga. Yanga SC ilivuna pointi tatu jumlajumla. Ameongeza mkataba wa miaka miwili bado yupo Jangwani mpaka 2027.

Wapya wengine hawa hapa ndani ya Yanga SC

Paul

Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26. Huyu ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Manu Rodriguez

Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Huyu ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.

Lassine Kouma

Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Balla Conte

Kouma
Kouma

Soma hii: Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC

Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Offen Chikola

 Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.

Casemiro

 Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Ninju

Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025.

Walioongeza mikataba wengine Yanga SC

Israel Mwenda

Julai 29 2025 Yanga SC ilimtambulisha Israel Mwenda kuongeza mkataba. Mwenda alitambulishwa kuongeza kandarasi ya miaka miwili Jangwani. Yupo Jangwani msimu wa 2025/26.

Mudathir Yahya

Mudathir Yahya kiungo mkabaji bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC. Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027.

Dennis Nkane

Kiungo Dennis Nkane aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu ujao kwenye benchi jipya.

Kiungo huyu alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.

Pacome

Ni kiungo alikamilisha msimu wa 2024/25 akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati. Jina ni Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025.

Kiungo huyu mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Kafunga mabao 7 kati ya 12 aliyofunga. Mguu wa kushoto katupia mabao manne. Ni pigo la kichwa alifunga bao moja mchezo dhidi ya Coastal Union.

Abuya

Duke Abuya winga wa Yanga SC ameongeza mkataba wa miaka miwili. Yupo Jangwani mpaka 2027. Julai 27 2025 alitangazwa kuongeza mkataba.

Maxi

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli kiungo wa Yanga SC.

Soma hii: Maxi aungana na Pacome Yanga SC: Tetesi wanaofuata kutambulishwa hawa hapa, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Maxi Nzengeli aliongeza mkataba Julai 28 2025 wa miaka miwili. Yupo hapo mpaka 2027. Huyu ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/24 alifunga dhidi ya Kagera Sugar.

Hitimisho

Jina ambalo linasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa Yanga SC ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Inaelezwa kuwa mchezaji huyo amesaini dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa ni nahodha wa Simba SC na tayari ameshawaaga mashabiki na viongozi wa Simba SC.

image
Share this: