Allasane KanteAllasane Kante
  • Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante rasmi usiku kibabe.
  • Ni yule kiungo wa kati aliyewatoa machozi Watunisia, ambaye anajiunga na Simba kutokea CA Bizertin ya Tunisia.
  • Staa huyo anatarajiwa kuungana na mastaa wengine wapya wa kikosi hiko ambao wataondoka Ijumaa kwenda kambini Ismailia, Misri kwa ajili ya ‘Pre-season’.

Mnyama Simba hapoi, kwani Baada ya jana usiku kumtambulisha rasmi mlinzi wao Rushine. Hatimaye leo wamemtangaza kiungo wao mpya wa kati Allasane Kante. Kante amejiunga na Simba mara baada ya kumalizana na timu ya CA Bizertin ya Tunisia kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu NBC 2025/26

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha Sportpesa

Huku ukiendelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Awatoa machozi Watunisia akiaga

Kante aligeuka gumzo nchini Tanzania mara baada ya video yake akiwaaga mashabiki wa Bizertin kusambaa, ikionyesha mashabiki hao wanabubujikwa machozi. Mchezaji huyo anamudu kucheza kwa ufasaha kama kiungo wa ulindi au ‘box to box’ hivyo anaweza kucheza kwenye nafasi zaidi ya 3 uwanjani. Hii inatarajiwa kuwapa Simba wigo mpana wa kumtumia katika maeneo mbalimbali uwanjani.

Kuhusu safari ya kwenda Misri

Simba safari ya Ismailia
Simba safari ya Ismailia

Kundi la kwanza la kikosi cha Simba limeondoka Tanzania leo Jumatano kuelekea nchini Misri. Safari hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu wa mashindano (Pre Season) kwa takribani mwezi mmoja. Timu hiyo inatarajiwa kwenda kuweka kambi katika mji wa Ismailia.

Inatazamiwa kundi la pili nalo litaondoka nchini ndani ya siku mbili yaani Alhamisi na Ijumaa ili kuungana na wenzao. Ikumbukwe kambi hiyo ya Misri ilitumiwa na Simba pia msimu uliopita. Kambi hiyo inatarajiwa kuhusisha wachezaji ambao wamesalia na mastaa wote wapya.

Ahmed akizungumzia hilo amesema: “Sehemu ya kikosi chetu imeondoka leo kuelekea Misri. Hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu. Kambi inatarajiwa kuwa na nyota wetu wote isipokuwa waliopo kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN.

“Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 28, mwaka huu. Mara baada ya kurudi Simba tutaanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.”

SOMA HII ZAIDI: Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC: Mashine nyingine 6 kutangazwa tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Zoezi la kutambulisha mashine mpya linaendelea

Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante
Fadlu

Kuhusu zoezi la kutambulisha mastaa wapya waliowasajili kwenye dirisha hili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa na wametamba kuendelea kushusha vyuma.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr

Kuhusu maboresho ya kikosi chao Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thank you’ na Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni: Che Malone aliyetimkia USMA, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

SOMA HII PIA: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

Hitimisho: Haya hapa majina mapya yanayotarajiwa kutambulishwa na Simba

Ukiachana na Rushine na Kante ambao tayari wametambulishwa, Simba inaelezwa kumalizana na mastaa wakubwa. Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.