- Tetesi za soka usajili Gyokeres kwenda Arsenal, Man United yatajwa kutibua dili kumvuta Old Trafford.
- Gwiji wa taarifa za uhamisho wa wachezaji barani Ulaya, Fabrizio Romano atoa ufafanuzi.
- Gyokeres aendelea kugomea mazoezi Sporting CP kushinikiza uhamisho wake.
Taarifa za uhamisho wa straika, Viktor Gyökeres zinaendelea kuwa za kusisimua, ambapo tetesi usajili wa Gyokeres Kwenda Arsenal zimeripoti kuwepo kwa mpango wa klabu ya Manchester United kuingilia dili hilo, huku gwiji wa taarifa za uhamisho wa wachezaji barani Ulaya, Fabrizio Romano akitolea ufafanuzi mpango mzima ulivyo.
Shinda mamilioni ya kindege ‘aviator’ ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

Kuhusu tetesi usajili wa Gyokeres Kwenda Arsenal

Kama ilivyoelezwa na Fabrizio Romano katika akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii kama YouTube, Instagram na X (Twitter), kuwa Gyökeres tayari amefanya makubaliano binafsi ya kimkataba na Arsenal wiki mbili zilizopita huku nyota huyo akionyesha msimamo wa dhati wa kujiunga na klabu hiyo kutokea jiji la London.
Wakala wa Gyökeres na mchezaji mwenyewe wameonyesha msimamo wa wazi katika mpango wa kuhamia ndani ya kikosi cha Arsenal, licha ya nyakati tofauti kuelezwa kuwepo kwa mazungumzo ya upande wa mawakala na United au hata zilipotokea timu kutokea Saudi Arabia.
SOMA HII PIA: PSG 2-1 Arsenal UEFA Champions League: Fainali ni PSG vs Inter Milan
Ishu ya Man United kuingilia dili

Licha ya kuwepo vyanzo kadhaa ambavyo vimethibitisha kuwa Man United wameingilia dili hilo, lakini Fabrizio amethibitisha kuwa hakuna ofisi rasmi au mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Manchester United na Sporting CP kuhusu Gyökeres, na United hawajawasilisha ofa rasmi kwa klabu ya Sporting CP.
Imebainika kwamba Sporting CP wameanza mazungumzo ya mwisho na Arsenal juu ya vipengele vya kifedha, ikiwemo malipo ya fedha za usajili zinazokadiliwa kufikia €63.5 m na ziada ya €10, huku Arsenal ikionekana tayari kuongeza hadi €70 m ili kufikia mahitaji ya Sporting.
SOMA HII PIA: Manchester City vs. Arsenal: A Premier League Showdown
Gyökeres aendelea kugomea mazoezi
Ili kufanikisha dili hilo kwa wakati, Gyökeres amekua na msimamo wazi na thabiti na amewaambia Sporting na viongozi wake kuwa hana nia ya kuendelea na programu za mazoezi ya Pamoja ya kujiandaa na msimu mpya nchini Ureno ili kushinikiza mchakato wa kujiunga na Arsenal licha ya ushawishi mkubwa wa fedha kutoka Saudi.
Sporting wapunguza Msimamo
Licha ya mwanzo Sporting CP kuonyesha ugumu wa kumuachia straika huyo, hali ya mambo inaonekana kuwa tofauti kwani, kama hehemu ya kuanza kujiandaa na maisha bila Gyokeres Sporting CP wameanza mchakato wa kufanya mazungumzo na klabu ya Almería juu ya kumnunua staa wa Colombia, Luis Suarez kama mbadala wa Gyökeres.
Ingawaje Sporting walikuwa wakitaka €80 m kama ada ya uhamisho wa Gyökeres, wamepunguza hadi €63.5 m + €10 m ya malipo ya ziada ikiwa na malipo ya awali rahisi kutekelezeka kungojewa juu ya ushawishi wa kuongeza dola hadi €70 m
Athari za saga ya usajili wa Gyokeres kwa pande zote
Arsenal
Kwa Arsenal hii ni fursa kubwa Gyökeres anaonekana kuwa kipaumbele kikuu cha timu hiyo katika dirisha hili la usajili na kocha wa timu hiyo Mikel Arteta anataka mshambuliaji wa kiwango cha juu kabla ya kuanza Ligi Kuu England, hivyo ikiwa dili hili litafanikiwa, itasaidia kurekebisha tatizo lao la ufanisi katika ufungaji wa magoli na kuongeza ushindani kwenye kushindania ubingwa.
Manchester United
United kweli wanahitaji mshambuaji lakini haionekani kujaribu kumpambania Gyökeres hadi sasa kutokana na kipaumbele cha nyota huyo anayetaka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inaonekana United watabaki kuwafuatilia mastaa wengine kama Sesko, Jackson kama mbadala wa Gyökeres.
Sporting CP
Wanaonekana kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwani wanamuhitaji Gyokeres lakini pia wangetamani kupata pesa za mauzo yake kama sehemu ya kuongeza nguvu yao ya kiuchumi. Ni wazi kama watakamilisha mauzo hayo basi watakuwa na fedha ya kutosha kumsajili Luis Suarez kutoka Almeria kama mbadala wake.
Hitimisho

Kwa mujibu wa Gwiji wa taarifa za usajili Fabrizio Romano ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna ofa rasmi na hakuna mazungumzo kati ya United na Sporting, kumhusu Gyökeres ambaye anaonekana kuitaka Arsenal pekee na kuweka wazi msimamo huo.
Mpaka sasa Arsenal na Sporting wako katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kifedha, na Sporting wanaonekana kuanzisha mikakati ya kushawishi kwa kuongeza viwango au kutafuta mbadala, lakini kama Sporting itaongeza bei au kubadilisha masharti United wanaweza kujaribu tena.

