- Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa, taarifa ambayo imekuwa zaidi ya stori bali gumzo kubwa kwenye dirisha hii la usajili.
- Ikumbukwe Yanga SC na Simba SC zote zilikuwa vitani usajili wa Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26.
- Conte ni staa wa kimataifa wa Guinea ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili na Yanga SC.
Pesa inaongea na moto unazidi kuwaka kuhusu tetesi za usajili Ligi Kuu NBC 2025/26, ambapo baada ya kuwepo kwa sokoni taarifa inayosumbua kuhusu klabu konmgwe za Yanga SC na Simba SC kuwania Saini ya staa wa kimataifa wa Guinea Balla Moussa Conte, hatimaye Balla Conte amesaini rasmi Yanga na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26.
Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa
Ukiwa unaendelea kuhabarika na makala hii, una nafasi ya kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu vita ya Yanga SC na Simba SC juu ya Conte

Habari ni nyingi na mud ani mchache kwani, ukiachana na majina makubwa yanayotamba sokoni kwa sasa likiwemo la kiungo Mzambia, Clatous Chama kujiunga na Azam habari kubwa ilikuwa kuhusu wakongwe hao wa Kariakoo kuingia vitani kwa ajili ya kuisaka saini ya staa wa kimataifa wa Guinea na CS Sfaxien ya Tunisia, Balla Moussa Conte.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26. Yanga watangaza Tofali la ubingwa
Yanga SC yamfuata, Simba SC yapandia juu
Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael ameweka wazi kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.
“Kulikuwepo na makubaliano kati ya klabu na klabu (CS Sfaxien na Yanga), ambapo Yanga walipewa Ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga hayajakamilika ndipo usiku Simba walienda na ofa kubwa.
“Kocha mkuu wa Simba, Fadlu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya Simu. Ofa ya Simba kwenda CS Sfaxien ni kubwa sana kuliko Yanga na Fadlu anawapush viongozi wake kumpata kijana kwani ndio chaguo namba moja sokoni.
“Yanga nao wanapush kukubaliana na mchezaji, Ila Balla Moussa Conté, amelalia Simba hii ni Baada ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Fadlu, lakini ghafla mabosi wa Yanga wakalazimika kupeleka ofa kubwa zaidi,” amesema Hans.
Nguvu ya Tofali la ubingwa

Katika hatua inaelezwa usajili huu ni sehemu ya matokeo makubwa na ya muda mrefu, ya Kampeni ya Yanga kujiimarisha kiuchumi na kuongeza msuli wa kifedha kupitia mtaji wa Wanachama, ambayo inaenda kwa jina la Tofali la Ubingwa.
Kampeni hii ilizinduliwa na Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe ambaye alisema: “Nyumba yetu ya mwaka 2024/25 imeshamalizika na sasa tunataka kujenga nyumba mpya ya Ubingwa ya 2025/26, Nyumba hii haiwezi kujengwa kwa kitu kingine isipokuwa nguvu kubwa ya Kiuchumi na ndiyo maana tunazindua kampeni ya Tofali la UBINGWA.
“Tofali hili la Ubingwa ni Ada yako ya Uanachama Mwananchi mwenzangu na huu ndiyo wakati wa kulipa Ada zetu ili kuijenga Yanga imara. Kipindi hiki ndiyo kipindi muhimu kwelikweli kwenye kuijenga Timu yetu, hiki ndicho kipindi cha kuseti mafanikio ya Ubingwa wa mwaka 2025/26.
“Kwa mantiki hiyo klabu yetu inapaswa kuwa na misuli mikubwa ya kifedha, hili ni Jukumu letu sote Wananchi kwa kulipa Ada zetu za mwaka za Uanachama, hakuna muujiza utakaotokea pasipo na sisi kujiandaa vizuri.
“Na hii ndiyo sababu sisi kama klabu kuanzisha kampeni hii ya Tofali la Ubingwa, kwahiyo kila mtu aweke Tofali lake ili tuijenge Nyumba tunayoitaka, kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25.
SOMA HII PIA: Simba SC waivuruga Yanga SC dili la Balla Conte | Tetesi za usajili | Feisal Salum ngoma nzito
Tofali la ubingwa kuvuka mipaka ya Afrika
Kamwe ameendelea: “Kampeni hii ndugu zangu siyo ya Dar Es salaam, siyo Dodoma, siyo Kigoma pekee, ni Kampeni ya duniani kote kuhakikisha tunaipa nguvu klabu yetu ili tuweze kufikia malengo tunayojiwekea.
“Tukikosea hapa mwanzoni kwenye kuijenga timu yetu basi tutakuwa tumekosea msimu mzima, hiki ni kipindi muhimu sana Mwananchi, nafasi ya kuijenga Yanga bora ndiyo hii ndugu zangu basi kila mtu aitumie nafasi hii kuandaa Parade lijalo la Ubingwa.
“Tofali la ubingwa la mwaka 2025/26 linauzwa shilingi 24,000/= pekee, lengo letu ni kukusanya matofali milioni 1 ndani ya miezi hii miwili, najua tupo Wananchi wengi hapa duniani, tukianza na Tanzania tu tunaweza kufika mpaka Milioni 40.”
Hitimisho Balla Conte kuungana na kikosi cha Yanga safari ya ‘Pre-season’

Kamwe alisendelea kusema: “Tukifanikisha matofali haya maana yake tutakuwa na Yanga imara itakayofanya maandalizi bora kuanzia Pre Season mpaka kutimiza malengo yetu kwa msimu mzima. Nataka kuwaambia kuwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatetea ubingwa msimu ujao.
“Tayari tumepata mwaliko wa kwenda Rwanda kwa ajili ya kushiriki siku ya kilele cha klabu ya Rayo Sports na napenda kuwahakikishia kuwa tutashiriki, na tutawatangazia mapema wanachama safari hiyo ambayo itahusisha mastaa wote wa zamani na wa sasa.”
SOMA HII PIA: Yanga SC imekomalia saini ya Balla Conte | Simba SC vs Yanga SC vitani | Usajili | Wachezaji wapya na wanaoachwa

