FailasufiFailasufi
  • Simba SC waivuruga Yanga SC dili la Balla Conte kiungo ambaye anatajwa kumalizana na watani zao wa jadi kwa asilimia kubwa wamemfuata.
  • Feisal Salum ngoma nzito kuondoka Azam FC kuibukia Simba SC.
  • Clatous Chama milango imefungwa Simba SC huku Yanga SC wakimchunia akitajwa rada za Azam FC.

Simba SC waivuruga Yanga SC kwenye dili la kiungo kimataifa wa Guinea, Balla Moussa Conte. Tetesi zinaeleza kuwa baada ya Yanga SC kuzungumza na mchezaji, mabosi wa Simba SC wakazungumza na timu. Kuna vita kubwa inaendelea kwa wababe hawa wawili kusaka saini ya kiungo huyo mali ya CS Sfaxien ya Tunisia.

Baada ya Conte Yanga yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC
Conte nyota anayetajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC.

Soma hii: Baada ya Conte Yanga SC yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Muda wa kupaisha kindege uvune mamilioni

Muda wa kupaisha kindege ni sasa na unapata mgao wa mamilioni. Ukicheza Aviator ni rahisi sana. Washindi ni wengi na wewe unastahili kuwa miongoni mwao.

SEO Banner LV

Mwendo wa wababe hawa kwa mchezaji huu ni mzito hivyo mwenye kisu kikali atakula nyama. Ikumbukwa kwamba Conte ana mkataba wa mwaka mmoja kwenye timu yake. Ni Yanga SC wanatajwa walianza kumfuatilia kiungo huyo kisha Simba SC wakaibuka nao wakihitaji saini yake.

Mbali na Conte kuna tetesi ambazo zinaendelea ikiwa ni wakati wa dirisha kubwa la usajili. Timu nyingi zipo sokoni kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Hapa tunakuletea tetesi zilivyo kwa sasa namna hii:-

Clatous Chama-Azam FC

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC na Zesco United ya Zambia. Chama mkataba wake na Yanga SC umeisha tayari na hajaongezewa mkataba. Taarifa zinaeleza kuwa Simba SC kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha kiungo huyo.

Ikumbukwe kwamba Chama aliibuka Yanga SC akitokea Simba SC. Julai Mosi 2024 alitambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga SC. Hakuwa chaguo la kwanza kwenye mechi za ushindani akiwa na uzi wa Yanga SC aligotea kufunga mabao sita na pasi tatu za mabao.

Dickson Job wa Yanga SC

Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa kuitwa mezani kuzungumza kuhusu suala la kuongeza mkataba.  Job mkataba wake umefika ukingoni baada ya msimu kuisha. Job alitambulishwa ndani ya Yanga SC akitokea Mtibwa Sugar.

Kwa sasa Job yupo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ipo Misri. Stars inajiandaa na CHAN ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 2. Tanzania itacheza na Burkina Faso, Uwanja wa Mkapa.

Feisal Salum anatajwa Simba SC

Feisal Salum, kiungo mshambuliaji wa Azam FC anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Feisal ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho. Msimu wa 2024/25 katengeneza pasi 13 na kufunga mabao manne yote akitumia mguu wa kulia.

Taarifa zinaeleza kuwa Simba SC ipo sokoni kuiwinda saini ya Feisal. Nyota huyo bado ana kandarasi yam waka mmoja na Azam FC hivyo Simba SC ikiwa watakuwa wanahitaji saini yake lazima wavunje benki kuvunja mkataba. Inaelezwa kuwa Azam FC hawapo tayari kwa sasa kumuachia kiungo huyo.

Edmund John wa Singida Black Stars – Yanga SC

Wing awa Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti kwenye mechi za ushindani anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Nyota huyo inaelezwa kuwa tayari mazungumzo yameanza kufanyika. Ni suala la makubaliano na kutambulishwa ndani ya Yanga SC kinachosubiriwa.

Ladack Chasambi anatajwa Azam FC

Baada ya matajiri wa Dar, Azam FC kupata saini ya Aishi Manula ambaye ni kipa kutoka Simba SC, Chasambi anafuata. Inaelezwa kuwa Chasambi ambaye ni kiungo mshambuliaji anahitajika na mabosi wa Azam FC. Kiungo huyo wa maajabu mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Shomari Kapombe anatajwa Azam FC

Kapombe na Mutale
Shomari Kapombe na Joshua Mutale kwenye moja ya mchezo wa ligi 2024/25. Source: Simba SC

Soma hii: Kimataifa Simba 2024/25 hawajakata tamaa kukomaa

Beki wa kulia ndani ya kikosi cha Simba SC, Shomari Kapombe anatajwa kuwa katika rada za Azam FC. Kapombe ni chaguo la kwanza la Fadlu Davids kwa msimu wa 2024/25. Rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi 27 alicheza kati ya 30 akikosekana kwenye mechi tatu.

Ni mabao matatu alifunga na kutoa pasi tatu za mabao. Katika mabao 69 yaliyofungwa na Simba SC alihusika kwenye mabao 6. Mkataba wake umeisha na hajaongeza mkataba mwingine. Taarifa zinaeleza kuwa kuna asilimia 70 kuongeza mkataba mwingine Simba SC na ikishindikana ataibukia Azam FC.

Jonathan Sowah- Yanga SC

Jonathan Sowah mshambuliaji wa Singida Black Stars anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Mshambuliaji huyo aliyeingia dirisha dogo anaingia kwenye orodha ya nyota waliowafunga makipa wote wa Simba SC na Yanga SC. Sowah alimfunga Djigui Diarra wa Yanga SC kwenye Ligi Kuu Bara ya NBC na alimfunga Moussa Camara wa Simba SC kwenye CRDB Federation Cup.

Mohamed Hussen- Yanga SC

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Mohamed Hussen Zimbwe Jr amefuta utambulisho wa Simba SC

Nahodha wa Simba SC, msimu wa 2024/25 Mohamed Hussen Zimbwe Jr anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Mkataba wa Zimbwe na Simba SC umekwisha. Simba SC wapo kwenye mzungumzo kuongeza mkataba mpya ikiwa dili litakwama ataondoka bure kwenye changamoto mpya.

Hitimisho

Dirisha kubwa la usajili ni kipindi ambacho timu hufanya maboresho makubwa katika vikosi kwa ajili ya msimu mpya. Simba SC imeanza kuwaaga baadhi ya wachezaji ikiwa ni Aishi Manula, Kelvin Kijli ambao wamepata timu mpya. Baada ya usajili kukamilika kuna maandalizi ya msimu na kuanza msimu mpya.

image

 

Share this: