- Lamine Yamal akabidhiwa jezi namba 10 ya Messi Barcelona, amwaga wino mpaka 2031.
- Miaka 18 tu, tayari Yamal sasa ni miongoni mwa mastaa wanaovuta pesa ndefu Barcelona.
- Yamal amekulia kwenye ‘academy’ ya Barcelona ‘La-masia’ alijiunga akiwa na miaka 7 tu.
Hatimaye kinda wa Barcelona Lamine Yamal, kijana mwenye kipaji kikubwa kutoka Uhispania ameongeza mkataba wake na klabu ya FC Barcelona hadi 30 Juni 2031. Tangazo hili limefanywa rasmi na klabu hiyo leo Jumanne huku akikabidhiwa rasmi jezi namba 10 ambayo imewahi kutumiwa na gwiji wa timu hiyo, Lionel Messi.
Shinda mamilioni kwa kucheza mchezo wa kindege ‘Aviator’ ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

Kuhusu Yamal akabidhiwa jezi namba 10 ya Messi Barcelona
Yamal ambaye alitimiza miaka 18 hivi karibuni, ameweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa umri wake kufanya mambo makubwa katika Ligi Kuu Hispania La Liga na pia katika michuano ya kimataifa, ikiwemo Euro 2024.
Mara baada ya kusaini mkataba huo Yamal alikabidhiwa jezi namba 10 ambayo imewahi kutumiwa na Ronaldinho, Messi na Ansu Fati. Katika mahojiano ya kipekee aliyofanya baada ya tukio hilo, Yamal alisema kwa kujiamini: “Barça ni klabu ya maisha yangu. Ndoto yangu imetimia. Nafurahi kuona familia yangu hapa.
Yamal asindikizwa na bibi yake

Mkataba huo mpya ulisainiwa kwenye ofisi za klabu ya Barcelona mbele ya rais wao, Joan Laporta na mkurugenzi wa michezo Deco huku akisindikizwa na bibi yake. Ingawa klabu haikutoa maelezo ya kina kuhusu kifedha, vyombo kadhaa vya habari nchini Uhispania vinaripoti kuwa Yamal ataingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi kikosini.
Mshahara wake unaweza kuwa kati ya euro milioni 8-19 kwa mwaka (takribani zaidi ya dola milioni 21.5) baada ya kodi. Baba yake Yamal, Mounir Nasraoui, alionekana kudokeza kiwango hicho cha mshahara kupitia Instagram Stories yake aliposhiriki chapisho la kusherehekea mkataba huo mpya na kuandika juu yake namba “19.3” ishara inayodhaniwa kuwa ni thamani ya mshahara wa mwanae kwa mwaka.
SOMA HII PIA: Dembele au Yamal nani atashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025?
Ubingwa wa EURO 2024 wamuibua
Lamine Yamal aliibuka na kuelezewa kama kipaji cha kipekee msimu uliopita katika La Liga, akiweka rekodi mbalimbali akiwa bado na umri mdogo. Hata hivyo ni katika mashindano ya Euro 2024 ambapo aliwaka sana, akivunja rekodi nyingi na kusaidia timu ya taifa ya Uhispania kushinda taji lao la nne la Ulaya.
Uchezaji wake wa hali ya juu ulimletea sifa kubwa kimataifa na kuanza kulinganishwa na wachezaji bora duniani. Katika msimu wa 2024/25, Yamal aliendelea kung’ara, hasa katika mechi dhidi ya Inter Milan kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ingawa Barcelona walitolewa kwenye hatua hiyo katika mechi iliyotajwa kuwa moja ya za kihistoria, Yamal alionyesha kiwango kikubwa kilichowafanya wengi wamwone kama mchezaji bora zaidi uwanjani.
Yamal atamaliza mkataba akiwa na miaka 23

Mara baada ya kusaini mkataba huu mpya, Barcelona imejihakikishia inamhifadhi kijana huyu mahiri hadi atakapokomaa kabisa kisoka. Wakati wachezaji wengi huanza kuingia kwenye kiwango chao bora wanapofikisha miaka 23, Yamal tayari ameonyesha uwezo ambao wengi huufikia baadaye.
SOMA HII PIA: Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025: H2H,vikosi huku Ronaldo, kule Yamal
Ashinda makombe mawili na Barcelona msimu huu
Yamal pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichoshinda makombe mawili ya ndani msimu huu, hatua inayodokeza kuwa hatima ya klabu hiyo uko katika mikono salama. Hata hivyo, licha ya mafanikio haya, Yamal ameonekana kuwa na ndoto za mafanikio makubwa.
Alichosema Lamine Yamal baada ya kusaini mkataba mpya

Akizungumzia hatua hiyo Yamal amesema: “Ni kweli mambo yamekuwa yakitokea haraka sana. Sidhani kama ni kawaida kwa kijana wa miaka 16 au 17 kupitia yote haya. Lakini pia ni jambo zuri kuwa kijana wa kwanza kufanya mambo haya.”
“Mwisho wa siku, nafikiria tu kuhusu maisha ya baadaye hususani kushinda. Naamini tutafurahi sana Pamoja na nafikiria mambo mazuri yanayotokea na basi. Mama yangu huniambia, ‘Furahia kila wakati, kwa sababu maisha hupita haraka sana.”
SOMA ZAIDI HII: Inter Milan Vs FC Barcelona ‘live’: Vikosi, uchambuzi, utabiri
Hitimisho
Kwa sasa, mashabiki wa Barcelona wana kila sababu ya kuwa na matumaini makubwa, kwani wana mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa zaidi duniani katika kikosi chao na sasa mkataba wake unawapa hakikisho la kuendelea kumfurahia kwa miaka mingi ijayo.
Katika ulimwengu wa soka ambapo wachezaji vijana huwindwa na klabu kubwa zenye fedha nyingi, hatua ya Yamal kusaini mkataba mrefu ni ishara ya uaminifu na mapenzi ya kweli kwa klabu aliyokulia. Ni mwanzo mpya wa enzi ya Yamal katika historia ya FC Barcelona, na dunia nzima ya soka inaangalia kwa makini kuona jinsi kijana huyu atakavyoendelea kung’ara.

