- Ellie Mpanzu Kibisawala mwamba ndani ya kikosi cha Simba SC kusaini kwa Waarabu RS Berkane ama Yanga SC ikiwa utaratibu utafuatwa.
- Simba SC wametoa masharti mazito kwa timu ambayo inahitaji saini ya nyota huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wa kulia kupiga makombora.
- Yanga SC watani wa jadi wa Simba SC wanatajwa kwa ukaribu kuivizia saini ya winga huyo machachari.
Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC ikiwa utaratibu utafuatwa. Waarabu hao wa Morocco wamekoshwa na uwezo wa nyota huyo katika anga la kitaifa na kimataifa jambo linalotajwa kuwaleta Tanzania kufanya mazungumzo na Simba SC. Ipo wazi kuwa nyota huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Soma hii: Stellenbosch FC vs Simba SC dakika 90 za maamuzi CAF
Shinda mamilioni leo hii muda huu
Shinda mamilioni leo hii kwa kupaisha kindege. Muda ni sasa na mamilioni yanakusubiri. Ni rahisi sana paisha kindege uvune mamilioni.

Mpanzu alikotoka mpaka kutambulishwa Simba SC

Soma hii: Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC i
Mpanzu ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye dirisha dogo ambapo aliibuka hapo akitokea Klabu ya AJ Vainqueur. Timu hiyo inacheza ligi ya Epfkin ( Ligi ya tatu Congo). Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa kwa wanaomtaka mchezaji huyo lazima wawasiliane na Simba SC ambao ni wamiliki halali wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo aliwahi kucheza AS Vita ya Dr Congo ambayo ilimpa utambulisho. Wengi wanatambua kwamba anatokea kwenye timu hiyo jambo ambalo limezua gumzo. Tetesi zinaeleza kuwa watani zao wa jadi Yanga SC nao wanaiwinda saini ya winga huyo kama ilivyo kwa RS Berkane.
“Mpanzu alisaini mkataba wa miaka miwili na ametumia miezi minne kwa sasa hivyo bado mwaka mmoja na miezi mingine mingi kwelikweli. Kama wanamuhitaji Mpanzu ana miaka 22 watapaswa kusubiri kwa muda wa miaka 13 mpaka atakapofikisha miaka 35.
“Ni vilevile ambavyo walimvumilia Jonas Mkude alipotimiza miaka mingi ndani ya Simba SC alipotimiza miaka mingi wao wakamchukua ilikuwa hivyo kwa Clatous Chama alipocheza kwa miaka mingi Simba SC wao wakamchukua.
“Waache kujitekenya kwa sasa sijui Mpanzu sijui nini, hapana wao kama wanamtaka Mpanzu wasihangaike kwenda Dr Congo mmiliki wa Mpanzu ni sisi Simba SC tutawauzia kama hiyo hela watakuwa nayo. Lakini wavumilie miaka 13 sio mingi kwa sababu Mpanzu ana mkataba wa miaka miwili, sisi ndio wenye Mpanzu wanapaswa kuwa makini wasubiri. Mpanzu sio mchezaji wa AS Vita wakienda huko watatapelewa.
“Huyo mchezaji sio mchezaji wa hiyo timu ambayo wanaijua hivyo wakienda kwenye hiyo timu watatapeliwa kwa kuwa sisi tunajua chimbo ambalo tulimpata sisi. Hivyo ikiwa watakwenda huko watatapelewa kwa kweli.
“Hakuna ambaye ataweza hiyo hela ya Mpanzu kwa sasa kwa mchezaji wetu gharama yake ni kubwa na hata wakijichanga ile timu wakachangisha kila mmoja kwa mashabiki watashindwa kumpata kwa kuwa hela yake ni kubwa,” alisema Ahmed.
Kimataifa Mpanzu alikuwa moto

Soma hii: SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yatajwa
Nyota Ellie Mpanzu wa Simba SC kwenye mechi za kimataifa alikuwa moto. Ni Kombe la Shirikisho Afrika Simba SC ilikuwa inapeperusha bendera. Ilicheza fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Kwenye mechi zote ambazo alikuwa anapewa nafasi ya kuanza Mpanzu alikuwa akiwapa tabu wapinzani. RS Berkane walifanya kazi kubwa kumzuia ugenini na nyumbani. Simba SC iligotea nafasi ya pili kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane.
Bao la dhahabu mbele ya Al Masry
Kwenye mchezo dhidi ya Al Masry hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa Mpanzu alifunga bao la dhahabu. Bao hilo alifunga akiwa nje ya 18 liliwanyanyua mashabiki wa Simba SC waliokuwa wakisaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali. Bao la pili likafungwa na Steven Mukwala kwa pasi ya Mohamed Hussen.
Simba SC ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Masry. Kwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 ikwa ni 2-2. Mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati, Simba SC 4-1 Al Masry.
Nusu fainali kwa Simba SC
Mpanzu alikuwa mchezaji muhimu katika mechi za kila hatua ikiwa ni ile ya nusu fainali dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Kwenye mechi zote mbili ambazo ni dakika 180 Simba SC haikufungwa. Wakiwa nyumbani Uwanja wa New Amaan walipata ushindi wa bao 1-0 na ugenini hawakupoteza wala kuruhusu bao.
Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza Aprili 20 2025 kiungo Jean Ahoua alifunga bao pekee la ushindi. Licha ya Ahoua kufunga bao moja kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 alikosa nafasi ya wazi kufunga bao dakika ya 90. Nafasi hiyo ya dhahabu alitengenezewa na winga Ellie Mpanzu.
Ugenini dhidi ya Stellenbosch FC Aprili 27 2025 Mpanzu alikomba dakika 86. Nafasi yake ilichukuliwa na beki Che Malone ambaye alikuwa nje kwa muda. Dakika 4 zilikuwa maalumu kumrejesha Che Malone kwenye ubora baada ya kutoka kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.
Hitimisho
Simba SC bado ina mkataba na Ellie Mpanzu ambaye ndani ya ligi kafunga mabao manne. Mbali na kufunga mabao hayo katengeneza jumla ya pasi tatu za mabao. Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 17 akitumia dakika 1,239 uwanjani kwenye mechi za NBC ambapo mabingwa ni Yanga SC.


