- Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaondoka katika kikosi hicho kupata changamoto mpya msimu wa 2025/26 ikiwa ataamua kufanya hivyo kwa kuwa ana ofa zaidi ya tatu.
- Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amefichua siri kuhusu ofa za Mzize na ahadi aliyopewa na Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said.
- Mabao aliyofunga Mzize kwenye ligi ni 14 akicheza mechi zote 30 za NBC 2024/25.
Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaondoka ikiwa ataamua kwa kuwa ana ofa zaidi ya tatu. Ikumbukwe kwamba Mzize alicheza mechi 30 za ligi msimu wa 2024/25 na timu hiyo ilitwaa ubingwa ikiwa na pointi 82. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema kuwa uchaguzi upo kwa mchezaji mwenyewe kuamua kubaki Yanga SC ama kuondoka.

Soma hii: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki
Muda wa kuvuna mamilioni ni sasa, cheza Aviator ujipatie mkwanja
Ukipaisha kindege sasa unavuna mamilioni. Ni rahisi sana kuwa milionea, cheza sasa uvune mamilioni sasa hivi. Cheza kila siku uwahi mgao wa mamilioni ambayo yanakusubiri.

Rekodi za Mzize Yanga SC
Rekodi zinaonyesha kuwa Mzize alicheza jumla ya mechi 30 za ligi. Ni dakika 1,877 alizitumia uwanjani kwenye mechi za ushindi. Mshambuliaji huyo mzawa alifunga jumla ya mabao 14.
Mzize ni mshambuliaji mzawa aliyefunga mabao mengi ndani ya ligi. Kinara wa utupiaji ndani ya ligi ni Jean Ahoua ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Ahoua alifunga jumla ya mabao 16 kwenye msimu ni rai awa Ivory Coast.
Katika mabao 69 ambayo Simba SC ilifunga, yeye alihusika kwenye mabao 25. Ni pasi 9 za mabao alitoa Ahoua ambaye mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Ahoua ambaye alitambulishwa Simba SC Julai 3 2024 mkataba wake umebaki mwaka mmoja yeye ni rai awa Ivory Coast.
Huyu hapa Ali Kamwe kuhusu ofa za Mzize

Soma hii: Chama kutua Yanga, Ali Kamwe atangaza kuna mtu atakula 10
“Mzize ni kweli ana ofa nyingi sana. Kuna ahadi ambayo Rais wa Yanga SC, (Hersi Said) alitoa tukiwa Afrika Kusini. Hiyo ilikuwa wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.
“Kwenye makubaliano hayo Mzize aliomba kuondoka ikiwa kutapatikana ofa nyingine. Mchezaji anaamua wapi atakwenda kucheza. Mchezaji akiwa tayari kwenda kucheza timu ambayo anahitaji tutazungumza naye.
“Tumepokea ofa nyingi sana ambazo zinamuhusu Clement Mzize. Wakati Mzize anaboresha mkataba wake aliambiwa anapaswa kupambana ndani ya msimu mpya. Hilo amelifanya na kazi yake imeonekana.
“Kuna taratibu linapofikia suala la mchezaji kwenda kwenye timu nyingine. Ofa za mchezaji zikifika mezani inakuwa mazungumzo ya mchezaji na klabu. Tunamwabia kuna ofa kadhaa zimekuja mchezaji anaamua wapi ambapo atakwenda kucheza.
“Baada ya hapo tunaruhusu mchezaji kuzungumza na timu kwenye masuala ya malipo. Yeye mwenyewe mchezaji ataona kwa hizi ofa niondoke ama nibaki Yanga SC. Hakuna ambaye atampagia mchezaji yeye mwenyewe ataamua,” alisema Kamwe.
Mbali na Mzize kutajwa kuondoka ndani ya Yanga SC kuna wachezaji wengine ambao inaelezwa kuwa wataondoka. Miongoni mwa hao ni kipa namba moja wa Yanga SC. Mdaka mishale Djigui Diarra.
Dijigui amekuwa kwenye ubora wake katika mechi za ushindani. Msimu wa 2024/25 ni kipa namba mbili kukusanya hati safi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC. Ni hati safi 17 alikusanya ndani ya mechi za ushindani.
Rekodi za Diarra Yanga SC kwenye ligi
Djigui Diara alikaa langoni kwenye jumla ya mechi 23 alikomba dakika 2,070. Katika mechi hizo ambazo alikaa langoni ni mabao 8 alifungwa. Alikuwa chaguo la kwanza chini ya Miloud Hamdi ambaye alikuwa anakinoa kikosi cha Yanga SC.
Kipa huyo alikosekana kwenye mechi 7 pekee za Yanga SC iliyocheza mechi 30. Ikumbukwe kwamba ndani ya dakika 2,700 Yanga SC ilivuna jumla ya pointi 82. Ilitwaa taji la ligi ikifikisha jumla ya mataji 31.
Inatajwa kuwa kuna timu ambazo zinafuatilia saini ya kipa huyo. Sifa yake kubwa ni kuwa kipa anayetoa maelekezo kwa wachezaji wengine akiwa uwanjani. Hali yake ya kujiamini na kupiga pasi za uhakika jambo ambalo lilifanya kuwe na mabadiliko kwa makipa wengi Bongo.
Kuhusu Diarra kuondoka Yanga SC

Soma hii: Mdaka mishale Diarra kabadili upepo, rekodi zake hizi hapa – SportPesa Tanzania
Kuhusu Diarra kuondoka Yanga SC, Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC alibainisha kuwa bado hawajafikiria jambo hilo. Kamwe aliweka wazi kuwa wana mpango na kipa huyo hivyo kwa sasa yupo ndani ya Yanga SC.
“Diarra ni kipa bora na yeye mwenyewe anajua. Ikiwa angetaka kuwa na hati safi zaidi ya 17 alizonazo alikuwa na nafasi ila aliamua mwenyewe. Bado tuna mpango naye hivyo yupo sana ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Hitimisho
Kwa upande wa kipa namba moja kukusanya hati safi ni Moussa Camara wa Simba SC. Alikusanya jumla ya hati safi 19 msimu wa 2024/25. Camara alikaa langoni kwenye mechi 28 kati ya 30 ambazo Simba SC watani wa jadi wa Yanga SC walicheza.


