- Yanga SC kupeleka Kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Ikulu baada ya kuikanda Simba kwa mkapa.
- Yanga SC waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutangazwa mabingwa kwa mara ya 4 mfululizo.
- Uongozi wa timu hiyo umeweka wazi sababu ni kuridhishwa na uongozi wa Rais Samia.
Wakijiandaa kuvaana na Singida Black Stars katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB itakayopigwa kesho Jumapili, uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kuwa na mpango wa kupeleka Kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Ikulu, kama sehemu ya kutambua mchango wa uongozi wa Rais Samia.
Kuhusu Yanga na ubingwa wa ligi ya NBC

Jumatano ya Julai 25, mwaka huu Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ushindi huo uliifanya Yanga SC kutangazwa mabingwa wa mashindano hayo.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB, Baada ya kuiua Simba Yanga yafanya umafia mzito Zanzibar
Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo ulikuwaje?
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida, huku timu zote zikisomana zikiwa zimechukua tahadhari kubwa kuhakikisha hazifanyi makosa yatakayowafanya kuruhusu bao. Dakika 15 za mwanzo Simba ilifika zaidi langoni mwa Yanga kabla na wao kujibu mapigo kwenye dakika 15 za pili.
Pacome Zouzoua aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati, baada ya mlinda mlango Moussa Camara wa Simba kumfanyia madhambi nyota huyo ndani ya 18 katika harakati za kuokoa mpira.
Baada ya goli hilo timu zote mbili ziliendelea kusaka mabao kabla hya mshambuliaji, Clement Mzize kuwapatia Yanga bao la pili dakika ya 85 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Pacome Zouzoua.
Vikosi vilivyoshiriki mchezo huo
Diara, Mwenda, Boka, Bacca, Job, Aucho, Nzengeli (Nzengeli 70′), Abuya, Dube (Mzize 45′), Mudathir (Ikangalombo 90′), Pacome huku Waliionyeshwa kadi wakiwa ni: Pacome 21′ Mzize 85′ Boka 90+1.
Kwa upande wa Simba kikosi chao kiliundwa na Camara, Kapombe (Nouma 79′), Zimbwe Jr, Chamou (Awesu 66′) Che Malone, Kagoma (Hamza 66′), Mutale (Kibu 45′) Ngoma, Mukwala (Ateba 54′) Ahoua, Mpanzu huku Zimbwe Jr akionyeshwa kadi ya njano.
Mchezo huu umekamilisha rasmi msimu wa ligi 2024/25 ambapo ingawa Simba wamekosa taji, huku Yanga wakitawazwa mabingwa, lakini timu zote mbili zimepata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Yanga kupeleka ubingwa wa NBC Ikulu

Mara baada ya mechi ya ushindi ya Yanga SC 2-0 Simba SC na wananchi kutangaza ubingwa wao wanne mfululizo wa Ligi Kuu Bara, Uongozi wa Yanga umetangaza kupeleka ubingwa huo Ikulu na pia kuzishukuru taasisi mbalimbali zilizochangia mafanikio hayo ikiwemo Kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa.
SOMA HII PIA: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP/ Pacome na Jean Ahoua kitaumana
Alichosema Semaji la Yanga Ali Kamwe

Akizungumzia mpango huo, Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema: “Shukrani za kipekee ni kwa wachezaji wetu ambao walimwaga jasho na damu, benchi la ufundi wamejitoa kwa namna ya kipekee. Tunawapongeza pia wapinzani wetu wote 14 kwa kutupa ushindani wa kutosha.
“Tuna furaha kubwa sana msimu huu. Mtakumbuka pale uwanja wa KMC, Msemaji wa ‘Aviola’ alitangaza kuwa wao wanacheza mechi za Yanga. Ile kauli ilituamsha sana, wananchi Niwaambie ukweli, kauli ile ndiyo iliyokuwa kifo chao.
“Kubeba ubingwa ni jambo zuri, lakini aviola kutoka kapa ni furaha kubwa zaidi. Msimu huu tumepitia mengi sana kama Klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio, Licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia.
“Viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama. Bila kusahau mchango wa Viongozi wote wa Matawi, Mashabiki na Wanachama tunasema Asante sana.
“Kijana yoyote anayemaliza kidato cha nne mwaka huu basi atakuwa amepata fursa ya kushuhudia klabu ya Yanga ikishinda mataji manne mfululizo, tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia ushindi huu mkubwa.
SOMA HII PIA: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga
Shinda mamilioni na kindege cha SportPesa
Unaweza kushinda mamilioni kwa kucheza mchezo wa kindege ‘Aviator’ ya SportPesa kwa kuigusa picha hii chini.

Kuhusu kumshukuru Rais Samia
“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia kwa uongozi wake thabiti kwa taifa letu. Usalama na amani umesaidia sisi kucheza mpira katika mazingira rafiki, Ubingwa huu ni zawadi kwa Mheshimiwa Rais. Tunalenga kupeleka ubingwa huu ikulu kuonesha kuwa tumeridhishwa sana na uongozi wake.”
Hitimisho
Hatimaye msimu wa Ligi Kuu Bara umefikia tamati kwa Yanga kushinda ubingwa, huku Wananchi wakiishukuru SportPesa mdhamini kuu namfadhili wao, Ghalib Said Mohammed (GSM), na kujipanga kumzawadia ubingwa Rais Samia.

